hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, September 15, 2014

MUME ADAI KUKIMBIWA NA MKE

Kweli? Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Ally Musa, mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro anadai kukimbiwa na mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Sauda.
Bw. Ally Musa anyedai kukimbiwa na mkewe(Sauda).
Akizungumza na gazeti hili, mume wa Sauda alisema kwamba, mkewe huyo ambaye alifunga naye pingu za maisha mwaka 2009, siku zote za maisha yao ya ndoa walikuwa wakiishi kwa amani na furaha tele lakini mwishoni mwa mwaka jana ndipo alipomkimbia.
Kwenye kitambulisho ni mume wa mtu(Bakari Mohamed) anayedaiwa kuchepuka na Sauda.
“Nasikitika sana, tulifunga ndoa kubwa ya kifahari na siku zote tuliishi kwa upendo na furaha tele, cha ajabu nilianza kumuona anabadilika tabia kutokana na marafiki wa ajabuajabu aliokuwa nao, akaanza kunidharau mwisho akanikimbia,” alisema.
Bw. Ally Musa akiwa na mkewe Sauda wakati wa harusi.
Baada ya kusikia upande wa mwanaume huyo, ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimsaka Sauda kwa njia ya simu ambapo ilikuwa ikiita bila kupokelewa na hata alipotumiwa sms hakujibu hivyo bado linamsaka.

No comments:

Post a Comment