hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, September 15, 2014

MAIDANA ACHAPWA KWA MARA YA PILI NA MAYWEATHER

 Floyd Mayweather (kushoto) akimtupia konde mpinzani wake Marcos Maidana.
Floyd Mayweather Jr. amemdunda kwa mara nyingine tena bondia wa Argentina, Marcos Maidana katika pambano lililofanyika Alfajiri ya leo jijini Las Vegas.
Mayweather ameshinda kwa pointi. Wawili hao walizichapa kwa mara ya kwanza May 4, na Mayweather kushinda kwa pointi pia. Mayweather alikuwa akitetea mikanda yake ya World Boxing Association na World Boxing Council.
 Mechi hiyo ya raundi 12 imefanyika kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena jijini Las Vegas. Hata hivyo Mayweather ambaye ameingiza dola milioni 32 kwenye pambano hilo, amedai kuwa Maidana alimng’ata katika raundi ya 8. Mayweather ameingiza zaidi ya dola 100 kwa mwaka huu peke yake kutokana na mapambano yake.
 Mayweather akimshambulia mpinzani wake.
 Maidana akijibu mashambulizi wakati wa pambano hilo.
Mayweather akiwasili katika Ukumbi wa MGM Grand Garden jijini Las Vegas kwa pambano hilo.
.

No comments:

Post a Comment