Tuesday, January 20, 2015

LICHA YA DIAMOND KUCHEKELEA MIMBA..MUME WA ZARI ADAI DIAMOND HAWEZI KUZAA NA ZARI


Staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan,  'Zari'.
 
Oohoo! Wakati staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akichekelea kitendo cha mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ kunasa mimba yake, habari ya mjini huko Kampala, Uganda ni juu ya aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, Ivan Ssemwanga kufunguka na kusema: “Naapa Zari hawezi kuzaa na Diamond.”HABARI YA MJINI
Wikiendi iliyopita, vyombo vya habari na mitandao nchini Uganda ambako kuna makazi mengine ya Zari mbali na Afrika Kusini, kulipambwa na habari hizo baada ya mwanaume huyo aliyezaa na mwanamama huyo watoto watatu kuanika siri nzito juu ya ishu hiyo.
‘Ubuyu’ huo ulidadavua kwamba, kwanza jamaa huyo mwenye utajiri wa kutupwa alianza kwa kuelezea namna alivyoshtuka aliposikia Zari ni mjamzito.

ASHANGAA KUSIKIA ZARI MJAMZITO
Alisema kwamba alishangaa kusikia Zari ni mjamzito wakati ana umri wa karibia miaka 40 na watoto watatu ambao amekuwa akiwapuuza na kuendelea kuzurura na mpenzi wake mpya, Diamond sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.
Ivan Ssemwanga akiwa na 'Zari'
TATIZO UMRI?
Ilielezwa kwamba Ivan aliweka wazi kuwa amekuwa na hofu kwa kuwa Zari ni mwanamke ambaye umri umemtupa mkono hivyo anaweza akashindwa na ‘stresi’ za malezi ya mtoto mchanga.
Maoni ya Ivan ameyatoa baada ya Diamond kufichua kwamba Zari ni mjamzito huku akitupia vielelezo vya vipimo mitandaoni vikionesha kiumbe anayekua tumboni kwa mwanamke, jambo lililosababisha jamii kuamini kuwa ni Zari kwa kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana kimahaba na kulala chumba kimoja kwenye hoteli mbalimbali.

Jamaa huyo alisema yeye ameshazaa na Zari watoto watatu na kwa pamoja walikubaliana kwamba Zari asilete kiumbe mwingine duniani.
NI AJABU?
Kwa mujibu wa Ivan, aligundua kwamba Zari hawezi kuwatunza vizuri watoto wake hivyo ni ajabu kuona anaongeza mwingine.
“Kwa ninavyomjua Zari, naapa hawezi kuzaa na Diamond,” alikaririwa jamaa huyo bila kufafanua kama mimba ambayo tayari Zari anayo itakwenda wapi.http://api.ning.com/files/BKB8rO763wH230bC6SV0Z9roW*ANLQaP38J5fIkWgTR71mmZHE3N1Cj3Btdf6KCudDqg1hFzW9On1-f3ugxzpvD5FhHW6KlS/oooi.jpg

Watoto wa Ivan Ssemwanga na 'Zari'.
UMRI WA MWISHO KUZAA NI UPI?
Kutokana na maelezo ya Ivan, Ijumaa Wikienda liliingia mzigo kutaka kujua umri wa mwisho wa mwanamke kuzaa ni upi?

Kwa mujibu wa mtaalamu wetu, umri wa miaka 41 bado mwanamke ana uwezo wa kushika mimba kama hana matatizo yoyote ya kiafya ambayo yanaweza kuzuia kwa namna moja au nyingine asishike mimba.
Mara nyingi muda hasa wa mwisho kabisa ni umri wa miaka 45 endapo pia mwanamke anakuwa hana tatizo la kiafya.

Hata hivyo, umri mzuri wa mwisho wa kuzaa kwa mwanamke unaoshauriwa ni miaka 40 kwani nyonga zinakuwa zimeanza kuchoka hasa kama mama atakuwa amezaa kabla.
TURUDI KWA ZARI
Kwa maelezo ya mtaalam wetu, hata kama mwanamama huyo anakaribia umri wa miaka 40 si kigezo cha kushindwa kumzalia Diamond hivyo kinachohitajika ni uangalizi wa hali ya juu.

HYPERMAN HK ATEMBELEA BABUU SHEBUU BARBER SHOP AND CAR WASH KURASINI

 Katika sehemu nzuri yakufanya usafi wa mwili wako na mali zako ni sehemu moja tu. dsm BABUU SHEBUU BARBER SHOP AND CAR WASH Iliyopo maeneo ya kurasini katika kituo cha pentagoni
hapo utaonyeshewa gari yako kwa bei poa na kwa usafi wa hali ya juu pamoja na kunyolewa nywele zako kwa style mbalimbali.. ina wahudumu vijana wenye kuijua uzuri kazi yao. Hyperman hk akiwa nje ya Babuu shebuu barber shop

 Hapa akiwa na moja ya vinyozi mahiri wa babuu shebuu barber shop

 Moja kati ya kina dada warembo wa Babuu shebuu barbaer shop. huyu ni maalum kwa ajili yakukuosha na kukusafisha baada ya kunyoa na mambo mengine mbalimbali.

 Na hizi ndio bei za BABUU SHEBUU CAR WASH


I Hope umenipata usicheze mbali na vitu vizuri karibu sana BABUU SHEBUU BARBER SHOP AND CAR WASH KURASINI....

Monday, January 12, 2015

PICHA: YALIYOJIRI KWENYE SHOO YA USIKU WA UNYAMA UNYAMANI ( TID NA CHID BENZ)

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' akiwa kwenye red Carpet kwenye shoo ya yake iliyofanyika ndani ya New Maisha Club ya jijini Dar
Msanii wa Hip Hop, wakazi akitoa burudani
Msanii wa Hip Hop, Kalapina akitoa burudani kwenye shoo ya T.I.D 
Msanii Khalid Mohamed aka TID (Top in Dar) akitoa burudani ya nguvu ndani ya Club ya New Maisha jijini Dar
 TID akiimba pamoja na mashabiki wake
Msanii TID akiendelea kutoa burudani ya nguvu na kushoto ni  Msanii wa Bongo Jay Moe
 Msanii wa Bongo Jay Moe akitoa burudani kwa mashabiki kwa kuwaimbia nyimbo za zamani
TID akiimba na mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Yakuza Mob, Gilla the Boss
Gilla the Boss akiendelea kutoa burudani
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidi Benz akitoa burudani ya nguvu kwenye stage ya New Maisha Club jijini Dar
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Chidi Benz (kulia) akiimba na msanii mwenzake TID
Msanii mahiri wa muziki wa kitambo kwenye muziki wa Bongo Flaver, Khaleed Mohamed 'TID' (wa kwanza kulia) akiwa na Dully Sykes(wa pili kutoka Kulia), Msanii wa Bongo Jay Moe (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Solo Thang (kushoto)
Baadhi ya mashabiki waliofika kutizama shoo hiyo wakifuatilia kwa umakini

Sunday, December 28, 2014

USIKU WA USWAZI NA WASWAZI WENYEWE YAFANYIKA DAR LIVE

Kundi la Umeme wakifanya yao stejini kwenye shoo ya usiku wa waswazi.Picha na Pamoja Blog
Kundi la Yakuza Mobb wakitoa burudani ya nguvu.
TID a.k.a "Mnyama" akitoa burudani ya nguvu kwenye shoo ya usiku ya uswazi na waswazi wenyewe
Chid Benz  akiimba na mashabiki wake 
Kala Pina a.k.a “Mbuge Mtarajiwa’’ akitoa burudani ya nguvu ndani ya Dar Live
Msanii Inspector Haroun a.k.a Babu akiwapagawisha mashabiki wake kwa ngoma za kitambo.
Mkaanga Sumu akifanya ya kwake kwenye stage
Baadhi ya mashabiki waliofika kwenye shoo ya Usiku wa Uswazi na wasaswazi wenyewe
Wadau wetu wakiwa kwenye picha za pamoja