hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, September 15, 2014

KIVAZI CHA JINI KABULA AIBU 100%

AIBU 100%! Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kutinga kivazi kilichomuacha wazi mwili wake.
Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’.
Jini Kabula alitinga kivazi hicho kwenye bethidei ya mtoto wa mwigizaji mwenzake, Riyama Ally ambayo aliiunganisha na ya kwake na kufanya bonge la sherehe katika Ukumbi wa Chamuruma uliopo Mabibo jijini Dar, ambapo mwanadada huyo bila kujali macho ya watu alitinga blauzi nyepesi inayoonesha maungo yake ya ndani yalivyo hivyo kuzua minong’ono kwa baadhi ya waalikwa.‘Jini Kabula’ akiwa kwenye bethidei ya Riyama.
“Duh, huyu msanii Kabula ndiyo kavaaje sasa? Angalia blauzi yenyewe ni kama hajavaa chochote kwani mpaka rangi ya braa ndani inaonekana, ni aibu kubwa kwa msanii kama yeye.
Mwanahabari wetu alipomfuata Jini Kabula na kumuuliza kulikoni kuvaa hivyo alisema haoni shida.

No comments:

Post a Comment