Ndani
ya ndege kila mtu alionekana kuwa na furaha, waigizaji walikuwa wakipiga stori
huku safari ikiendelea. Hiyo ndio iikuwa safari ya kwanza kuja Afrika kwa kazi
ya kuigiza. Kwao, safari hii ilionekana kuwa na baraka nyingi na walitumaini
kuuza kazi hiyo zaidi ya kazi zote ambazo zilikuwa zimepita.
Katie alikuwa bize na kusoma jarida maalumu
ambalo lilikuwa likielezea nchi ya Tanzania kuanzia uoto wa asili na mambo
mengine mengi. Maeneo mengi yakaonekana kumvutia, tayari akilini mwake
ikajengeka picha kwamba nchi ya Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi zilizokuwa
na mazingira mazuri hasa kimisitu.
Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na waigizaji wote
ambao walikuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kuigiza filamu hiyo ya ngono ambayo
waliipa jina la MY NEIGHBOURHOOD CHICKS. Katika kipindi hicho walikuwa na kila
kitu, kamera kubwa zilizokuwa na uwezo mkubwa, wapiga picha na waongozaji, wote
walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo wala haikupitia jijini Dar es Salaam.
Kwa kuwa ilikuwa ni ndege yao wenyewe, ndege ya kampuni yao, ikapita moja kwa
moja mpaka katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume,
Zanzibar.
Hali ya hewa kwao ikaonekana kuwa nafuu. Nchini
Marekani, baridi lilikuwa likiwapiga kila siku, hawakuipenda hali ile ya hewa
lakini walikubaliana nayo. Joto ambalo walikutana nalo nchini Tanzania
likaonekana kuwafurahisha.
Kila kitu kilikuwa kimekwishapangwa. Mara baada
ya kushuka kutoka ndani ya ndege, wakapanda kwenye magari maalumu ya hoteli ya
Green Horse na kisha kuanza kwenda katika hoteli hiyo.
Njiani, kla mmoja alikuwa akiangalia nje,
majengo ya kizamani ambayo yalikuwa yametumiwa enzi za ukoloni yakaonekana kuwa
na mvuto machoni mwao. Kila wakati walikuwa wakitabasamu, hawakuamini kama
kulikuwa na majengo mazuri kama yake.
Gari lile likafika katika hoteli ya Grean House
ambayo ilikuwa pembezoni mwa bahari ya Hindi na kisha kuingia ndani. Muonekano
wa hoteli ile ulikuwa sawasawa na hoteli ambazo zilikuwa zimejengwa nchini
Marekani. Upepo mwanana wa bahari ambao ulikuwa ukiwapiga ukaonekana
kuwafurahisha.
Wakachukua vyumba ndani ya hoteli hiyo, kwa kuwa
walikuwa na fedha za kutosha, kila mmoja akakabidhiwa chumba chake ila kwa wale
ambao walitaka kulala wawili wawili walikuwa wakiruhusiwa.
Katie akatulia kitandani kwake, akachukua kitabu
cha Atlas ambacho kilikuwa mezani na kisha kuanza kukifungua na kuangalia mambo
mbalimbali kuhusiana na nchi ya Tanzania. Hapo ndipo alipogundua kwamba pale
walipokuwa walikuwa katika moja ya kisiwa cha Unguja.
Moyoni mwake, Katie akaanza kuvutiwa, akatamani
kuziona zile mbuga za wanyama ambazo zilikuwa zikionekana katika ramani ya nchi
ya Tanzania. Alichokifanywa kwa wakati huo ni kuifuata kompyuta ya mezani na
kisha kufungua Internet na website ya Google na kisha kuandika ‘Mikumi National
Park’
Picha za mbuga hiyo zikatokea, Katie akabaki
akitabasamu tu. Hamu ya kutamani kuelekea katika mbuga ile ikaonekana kumkamata
kupita kawaida. Katie hakuishia hapo, bado aliendelea kuangalia zaidi na zaidi,
akaandika Kilimanjaro.
Mlima mkubwa wa Kilimajaro ukatokea katika kioo
cha kompyuta ile. Akaanza kuuangalia mlima ule ambao juu ulikuwa na barafu
jingi. Katie akaachia tabasamu pana zaidi, alichokuwa akikitaka ni kuchukua
picha za mlima ule.
Akaenda kitandani na kisha kufungua begi lake na
kutoa kompyuta yake ya mapajani na kisha kuiunganisha na Internet isiyotumia
waya iliyokuwa katika hoteli ile. Akafungua website ya Google na kisha kuandika
Kilimanjaro. Ulipotokea mlima Kilimanjaro, akaanza kuzichukua zile picha na
kisha kuziweka katika kompyuta yake.
Baada ya siku mbili kupita, filamu hiyo ambayo
walipanga kuuigiza ikaanza. Kwao ikaonekana kuwa filamu nzuri, kila miuigizaji
ambaye alikuwa amepangwa kuigiza katika filamu hiyo alikuwa akiigiza kwa umakini
mkubwa na kujitolea hasa.
Kwa sababu Katie ndiye alikuwa muigizaji mkuu,
aliigiza kwa ustadi mkubwa kiasi ambacho hata muongozaji akashangaa. Filamu hiyo
wala haikuwa ndefu sana, walichukua kipindi cha mwezi mmoja ikawa
imekamilika.
Ni matukio ya ngono ndio ambayo yalikuwa
yametawala ndani ya filamu hiyo ambayo ingeonekana kuwavutia wale wote ambao
walikuwa wakipenda kuangalia filamu za aina hiyo duniani.
Baada ya kumaliza kuigiza filamu hiyo, Katie
akatoa wazo ambalo lilionekana kumvutia kila mtu. Alichoona yeye ilikuwa ni
vizuri kwa wao wote kuelekea katika mbuga yoyote ile ya wanyama kwa lengo kubwa
la kuona wanyama.
Kila mmoja akaonekana kuridhika na wazo lile,
lilionekana kuwa wazo zuri ambalo liliungwa mkono na kila mtu. Siku iliyofuata,
safari ya kuelekea Morogoro ikaanza huku wakitaka kuingia katika mbuga ya
wanyama ya Mikumi na kuangalia wanyama.
Kwa kuwa walikuwa wametumia ndege, walichukua
dakika arobaini na tano wakawa wamekwishafika Morogoro ambapo wakakutana na
magari ya mbuga hiyo na moja kwa moja kuanza kupelekwa katika mbuga hiyo
iliyokuwa na wanyama wengi na wa aina mbalimbali.
Walipofika mbugani, wakapelekwa katika hoteli ya
MIKUMI NATIONAL PARK na kisha kuchukua vyumba katika hoteli hiyo. Siku
iliyofuata, wakachukuliwa na magari ya mbugani na kisha kuanza kupelekwa sehemu
mbalimbali katika mbuga hiyo.
Muda mwingi Katie alikuwa kimya ndani ya gari
lile, macho yake yalikuwa yakimwangalia dereva ambaye alikuwa akiliendesha gari
lile, Gibson. Gibson kwake alionekana kuwa kijana wa tofauti, umbo lake kubwa
lilimvutia Katie.
Kwake, Gibson alionekana kuwa kijana mwenye
mvuto, fulana yake aliyokuwa ameivaa ambayo ilimbana sana mwili ilimfanya mwili
wake uliojazia kuonekana vizuri kabisa. Muda mwingi Katie alikuwa akiendelea
kuutumia muda wake kumwangalia Gibson ambaye alikuwa bize akiwatembeza huku
vijana wengine wawili wakitumia muda huo kuwaelekeza wazungu wale sehemu
mbalimbali na kuwaonyeshea wanyama mbalimbali.
Akili ya katie haikuwa sawa katika wakati huo,
mvuto ambao alikuwa nao Gibson ukaonekana kuusumbua moyo wake. Ni kweli kwamba
alikuwa amewaona wanaume wengi na kufanya mapenzi na wanaume wengi pia lakini
kwa Gibson hali ikaonekana kuwa tofauti sana.
Kwake, mwanaume huyo alikuwa na mvuto mkubwa,
kifua kipana kilionekana kumchanganya kupita kawaida. Ingawa waigizaji wengine
walikuwa bize kuwasikiliza vijana ambao walikuwa wakiwaelekeza mambo mengi
lakini kwa Katie muda wote macho yake yalikuwa yakimwangalia
Gibson.
Katie akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni
kuanza kupiga hatua kumfuata Gibson, alipomfikia, akaamua kumsogelea karibu
zaidi. Gibson hakuonekana kuwa na wasiwasi, kwake, wazungu walionekana kuwa watu
wa kawaida sana kiasi ambacho ilimjia vigumu sana kumtambua msichana wa kizungu
kama alikuwa ameangukia katika mapenzi.
“Hi” Katie alimsalimia Gibson huku tabasamu pana
likiutawala uso wake.
“Hi” Gibson aliitikia.
Katie akaanza kujiumauma. Wakati mwingine
alikuwa akijishikashika kiuno, mara akiikutanisha mikono yake na kujishika huku
akijipindapinda, kwa wakati huo alikuwa akijitahidi kuleta mapozi mengi ya
kizungu ili Gibson aweze kuelewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati
huo.
“Can I ask you something? (Naweza kukuuliza
kitu?)” Katie alimuuliza.
“Yeah” Gibson alimwambia
Katie.
Huo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yao. Katika
kila hatua ambayo ilikuwa ikiendelea kati yao, Gibson alikuwa akichukulia
kawaida tu japokuwa muda mwingi Katie alikuwa akionyesha dalili zote kwamba
alikuwa akimhitaji Gibson kwa kipindi hicho.
Dakika ziiendelea kwenda mbele, Gibson akaja
kugundua kwamba Katie alikuwa kwenye hisia kali hasa mara baada ya kufanya tukio
ambalo lilionekana kumshtua, kushika maeneo ya zipu yake.
Gibson alibaki akitetemeka, hakuamini kile
ambacho Katie alikuwa amekifanya. Kwa mara ya kwanza alifikiri labda ilikuwa ni
bahati mbaya lakini baada ya kuyapeleka macho yake usoni mwa Katie, msichana
yule alikuwa akitabasamu tu.
“Mmh!” Gibson aliguna.
Kuanzia muda huo Katie hakutaka kuficha kitu
chochote kile, akaanza kujionyesha dhahiri kwamba alikuwa ametekwa na mapenzi ya
mwanaume huyo. Japokuwa Gibson alijitahidi sana kuzuga ili wazungu wengine
wasiweze kuelewa kilichokuwa kinaendelea lakini hali ikaonekana kushindikana
kabisa, kila mtu akafahamu.
Kwa sababu maisha yao yalikuwa ni ya kawaida,
Katie hakutaka kujificha, akaamua kuwaambia wenzake kwamba kwa kipindi hicho
moyo wake ulikuwa umetekwa kwa asilimia mia moja na Gibson. Gibson hakuongea
kitu, muda wote alikuwa akijisikia aibu.
Muda wa kurudi hotelini ulipofika, wakaanza
kurudi huku Katie akiwa kiti cha mbele kabisa. Katika kipindi hicho alikuwa
akihakikisha kwamba anafanya kila liwezekanalo mpaka mwanaume huyo, Gibson
anakuwa wake bila kujua kwamba Gibson alikuwa na mchumba aliyeitwa Prisca,
ambaye alikuwa akimpenda kuliko mwanamke yeyote huku tumboni mwake akiwa na
kiumbe alichosaidiana kutengeneza na Gibson, ujauzito.
****
Kijana Gibson alikuwa akijulikana sana katika
mtaa wa Mwembechai sehemu ambayo alikuwa akiishi ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Maisha yake yalikuwa ni maisha ya kawaida sana, utafutaji wake ambao alikuwa
akiufanya kila siku ndio ambao ulikuwa ukimuweka hapa mjini kila
siku.
Gibson alimaliza Elimu ya kidato cha sita katika
shule ya Sekondari Mbezi High iliyokuwa maeneo ya Mbezi ile ya kuelekea Kibaha.
Katika maisha yake ya shuleni ndani ya shule hiyo, Gibson akafanikiwa kupata
marafiki wengi ambao walikuwa wakivutiwa nae kutokana na ucheshi mkubwa ambao
alikuwa nao.
Wasichana nao hawakuwa nyuma, walikuwa
wakimpenda sana Gibson kiasi ambacho kila msichana akatamani kuwa nae. Gibson
hakutaka kujirahisisha kabisa, kwa kipindi hicho maisha yake yalikuwa
yakifikiria elimu tu.
Hakujua ni wapi alipokosea mpaka msimamo wake wa
kutokutaka kuwa na msichana kupotea, akajikuta akiangukia katika mapenzi ya
msichana Prisca. Uhusiano wao wa kimapenzi ukaanzia hapo. Mara kwa mara
walionekana kuwa pamoja, wanafunzi wakaufahamu uhusiano huo japokuwa wao wenyewe
walijaribu kuuficha ukweli.
Miezi ikaendelea kukatika mpaka pale ambapo
wakamaliza elimu ya kidato cha sita na kukaa nyumbani kwa ajili ya kusubiria
matokeo. Kwao, kumaliza kule kulionekana kuwa na unafuu, wakaanza kujiachia vya
kutosha, walikuwa wakifanya mapenzi mara kwa mara hasa katika kila kipindi
ambacho msichana Prisca alipokuwa akienda kumtembelea Gibson.
Miezi ikakatika na matokeo kutoka, hakukuwa na
mtu ambaye alikuwa amefanya vizuri, wote walikuwa wamefeli mitihani yao. Wote
wakaonekana kuumia, hawakuamini kile ambacho kilikuwa kimetokea lakini ikawabidi
kukubaliana na ukweli kwamba walikuwa wamefeli mitihani yao.
Maisha ya mitaani yakaanza. Kwa kuwa kila siku
alikuwa akishinda sana nyumbani, akaanza kuonekana kuwa mzigo kwa wazazi wake.
Mzee Lyimo ambaye alikuwa baba yake, akaamua kumpa kiasi cha shilingi milioni
moja na nusu kwa ajili ya kwenda kuanzisha biashara.
Gibson akazitumia fedha zile vilivyo, akaanzisha
biashara ndogo ndogo ambazo zikaanza kukua kila siku na kuanza kumuingizia fedha
japokuwa hazikuwa nyingi sana. Bado uhusiano wake na Prisca ulikuwa ukiendelea
kama kawaida.
Kila siku walikuwa wakitumia kinga. Mioyoni mwao
hawakuwa na wasiwasi na magonjwa ya zinaa au UKIMWI bali walikuwa na wasiwasi na
mimba tu. Ndani ya chumba cha Gibson, mipira ya kufanyia mapenzi ilikuwa mingi
na alikuwa akiitumia katika siku ambazo Prisca alikuwa akija nyumbani
hapo.
“Mmmh! Hili baridi” Gibson alimwambia Prisca
huku manyunyu yakimwagika nje.
“Limefanya nini tena?” Prisca
aliuliza.
“Linanipa hali fulani ya kuhitaji joto” Gibson
alimwambia Prisca.
“Ngoja nikupe sweta” Prisca alimwambia Gibson
huku akiachia tabasamu.
“Hapana. Hebu njoo karibu yangu” Gibson
alimwambia Prisca ambaye akamsogelea pale kitandani na kisha
kumkumbatia.
Hali ile ndio ambayo ikaonekana kuwa na unafuu
kwa Gibson, kwa mbali akaanza kuhisi joto kutoka katika mwili wa Prisca. Gibson
hakuona hali ile kutosha, akaamua kuipitisha mikono yake katika kiuno cha
Prisca. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Gibson alivyozidi
kuipeleka mikono yake zaidi na zaidi katika mwili wa Prisca, baada ya dakika
chache, Prisca alikuwa mtupu.
Hilo ndilo lilikuwa lengo la Gibson,
kilichofuata mahali hapo ni kuanza kumchezea Prisca. Aliendelea na mchezo ule
mpaka pale alipoona ameridhika. Akaupeleka mkono wake katika boksi la mipira,
hakukuwa na mpira hata mmoja.
“Da! Kumbe yote iliisha!” Gibson alijisemea
moyoni.
Hakuwa na jinsi. Kwa hali ambayo alikuwa nayo
mahali pale ilikuwa ni vigumu kuinuka na kuelekea duka la madawa kununua mipira,
alichokifanya ni kufanya mapenzi na Prisca bila kutumia mpira
wowote.
Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya
mapenzi na Prisca bila kutumia mpira, hiyo ndio ilikuwa siku ambayo
ikamsababishia Prisca kuanza kutapika na kujisikia kichefu chefu, siku hiyo ndio
ambayo ilimfanya Gibson kujiandaa kuitwa baba.
Prisca akawa na ujauzito. Marafiki zake Gibson
walikuwa wakimshauri mara kwa mara kwamba amwambie Prisca aende akautoe ujauzito
ule lakini Gibson hakuonekana kukubali. Moyo wake ulikuwa ukimpenda sana mtoto
wake ambaye alikuwa tumboni mwa mpenzi wake, Prisca.
Kutokana na kuwa bize na ujauzito wa Prisca,
biashara zake zikaanza kuyumba. Faida aliyokuwa kipata alikuwa akiitumia
kumtunza Prisca ambaye alionekana kuwa kwenye wakati mgumu. Kwa kuwa kipindi
hicho alikuwa amepanga, hakutaka wazazi wake wafahamu kitu chochote
kile.
Tayari Gibson alikwishaona kwamba mambo yalikuwa
magumu. Kiasi cha fedha ambacho alikuwa amebaki nacho, akaamua kujifunza
udereva. Alisoma kwa muda wa mwezi mmoja, alipoona amekuwa tayari, akaamua
kwenda kusoma NIT ili aweze kuendesha magari ya viongozi mbalimbali wa
Serikalini.
Gibson akawa dereva mzuri, masomo yake akawa
amemaliza kwa kufanya vizuri mpaka pale ambapo alipewa cheti tayari kwa kuanza
kazi pale ambapo angeipata. Kwa wakati huo, kiasi ambacho alikuwa amebaki nacho
kilikuwa kidogo sana, akaamua kukibana hivyo hivyo mpaka pale
kilipokwisha.
Kazi zikaonekana kuwa ngumu kupatikana.
Aliangaika kwa muda wa miezi mitatu na ndipo alipoona kwenye gazeti kwamba
kampuni ya Utalii ya Filbert Royal Tourism iliyokuwa Morogoro katika mbuga ya
Mikumi ilikuwa ikitafuta madereva.
Gibson hakutaka kupuzia, japokuwa alikuwa
amejaribu kuomba kazi sehemu nyingi na kukosa, hapo napo akaamua kujaribu. Baada
ya wiki moja, akaitwa kwa ajili ya kufanyiwa usaili na alipoonekana kustahili,
akaanza kazi.
Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake. Mshahara wake
wa kwanza, akamsafirisha Prisca na kuishi nae mkoani Morogoro huku wazazi wa
binti huyo wakiwa wameridhia kwa kila kitu. Ukaribu ambao alikuwa nao kwa mpenzi
wake ulikuwa mkubwa, kila alipokuwa akitoka ofisini, moja kwa moja alikuwa
akielekea nyumbani na kukaa na mpenzi wake, Prisca.
Maisha yaliendelea kila siku. Tumbo la Prisca
kwa kipindi hiki lilikuwa kubwa. Alichokifanya Gibson ni kumuajiri mfanyakazi wa
ndani kwa ajili ya kumwangalia mpenzi wake na kumfanyia kazi
nyingine.
Simu ndio kilikuwa chombo ambacho alikuwa
akipenda sana kukitumia kuwasiliana na Prisca kila alipokuwa mbali nae.
Hakujisikia raha kama yalipita masaa mawili bila kuwasiliana na Prisca. Prisca,
kwake alikuwa kila kitu, alimpenda kuliko msichana yeyote katika dunia
hii.
Wasichana wa Morogoro wakaonekana kuvutiwa sana
na Gibson ambapo mara kwa mara walikuwa wakimtaka kimapenzi. Gibson hakuonekana
kukubaliana nao, hakuwa tayari kumsaliti Prisca kwa msichana yeyote yule,
mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa Prisca yalikuwa ni makubwa
sana.
“Ninakupenda sana mpenzi wangu” Gibson
ailimwambia Prisca.
“Ninakupenda pia”
“Ulikumbuka kwenda hospitali leo?” Gibson
alimuuliza.
“Ndio”
“Dokta amesemaje baada ya
kukupima?”
“Otea”
“Wa kike” Gibson alimwambia
Prisca.
“Hapana”
“Kwa hiyo ni wa kiume?”
“Ndio” Prisca alijibu na kutoa tabasamu
kali.
“Asante Mungu. Nilikuwa na kiu ya kupata mtoto
wa kwanza awe wa kiume. Mungu amejibu maombi yangu” Gibson alimwambia
Prisca.
“Kwa nini haukuomba wa kike?”
“Ninataka kwanza niwe na mlinzi wa nyumba yangu.
Wa pili akiwa wa kike, nitafurahi zaidi. Hata kama baadae watakua, huyu wa kike
inabidi awe na heshima kwa kaka yake” Gibson alimwambia
Prisca.
“Kwani akiwa wa kwanza wa kike hatokuwa na
heshima?”
“Hilo jibu niachie moyoni mwangu. Si unajua
nyumbani kwetu wa kwanza ni wa kike! Niachie tu jibu langu kwani naamini
mwenyewe umeshaona sana ulipokuwa ukija nyumbani” Gibson alimwambia
Prisca.
Kwa wakati huo walikuwa wakipiga stori ambazo
kwa mtu mwingine zingeonekana kuwa za kijinga lakini kwao zilikuwa ni stori
nzuri ambazo zilimvutia kila mmoja. Waliendelea kuongea usiku kucha mpaka katika
kipindi ambacho wote wakapitiwa na usingizi.
Je nini kitaendelea?
Je Katie ataweza kumpata
Gibson?
Je Prisca ataweza kujifungua salama hapo
baadae?
Kuna mengi yatatokea katika hadithi hii,
yatakuhuzunisha sana, yatakufurahisha sana ila mwisho wa yote, hadithi hii
itakuburudisha sana.
Itaendelea KESHO SAA 1 USIKU.
inamuendelezo na marudio kama MARACLARA.
No comments:
Post a Comment