SIKU 1 NA MASAA KADHAA ZIMEBAKI ILI KUFIKIA ILE SHOW ILIYOKUWA INASUBIRIWA KWA
HAMU NA MAELFU YA WAKAZI WA MJI WA DODOMA NA VITONGOJI VYAKE, NI LIVE DJ DRUMMER
NDANI YA CLUB MAISHA JUMAMOSI HII YA TEREHE 2/11/2013 NI BALAA KUBWA WABUNGE WA
VYAMA VYOTE WAUNGANA KUPISHA SHOW HIYO!!!
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiuaga Mwili wa
Marehemu Balozi Isaac Sepetu, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,
Mnazi mmoja Mjini Unguja
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI......
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimpa pole Mjane wa
Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam Sepetu,alipofika katika ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja, kuuaga mwili wa
Marehemu.
Ibada ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Sepetu ikiendelea
kwenye Kanisa la Minara Miwili Zanzibar
Baadhi ya watoto wa marehemu Balozi Sepetu
wakisikiliza neno la mungu
Wema Sepetu(Aliyesimama Kushoto)
akiwa kanisani kwenye maombezi ya baba yake mzazi
Baadhi ya Wananchi
mbali mbali wakiwa katika sehemu maalum nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
la zamani, Mnazi mmoja Mjini Unguja,wakisubiri kuuaga mwili wa Marehemu Balozi
Isaac Sepetu, ambapo utazikwa Kijiji kwao Mbuzini Wilaya
Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar, Cosmas Amani
Shayo, alipowasili katika eneo la
Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu, yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi
Unguja jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akiwa na viongozi wengine akiwemo Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Mohamed
Gharib Bilali,katika Mazishi ya
Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja
jana
Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham
Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika
kaburi lake yalipofanyika mazishi
kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja jana.
Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili
Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa
marehemu Balozi Issac Abraham
Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya
ya Magharibi Unguja jana.
---------------------
Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed
Shein, jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya mwanasiasa na
mwanadiplomasia mkongwe Marehemu
Balozi Issack Abraham Sepetu
(71),aliyezikwa katika Kijiji cha Mbuzini,Mkoa wa Kusini Unguja jana
Alasiri.
Viongozi wengine waliohudhuria
mazishi hayo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk
Mohamed Gharib Bilal pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mapema mwili wa Balozi Sepetu
uliagwa na waombolezaji wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali
Iddi na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa shughuli ambayo
ilifanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo eneo la
Kikwajuni katika Manispaa ya Zanzibar kabla ya misa maalumu iliyofanyika katika
Kanisa la Mtakatifu Joseph katika Mtaa wa Shangani.
Watoto wa marehemu, Amani,Mkusa,
Wema na wengineo walikuwapo katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na Balozi
mstaafu, Ali Abeid Karume, ambaye alisema marehemu ameacha pengo kubwa katika
jamii kwani alikuwa kiongozi makini na mzalendo aliyelipenda taifa
lake.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar,Vuai Ali Vuai,alimwelezea marehemu kama mwasisi wa mazungumzo ya
kutafuta mwafaka wa kisiasa Zanzibar wakati juhudi hizo zilipoanza mara ya
kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi visiwani mwaka 1995
kupitia kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Chifu Emeka
Anyaoku.
HAYA NDIYO MAAJABU YA XTREME DEEJAYZ NDANI CLUB
MAISHA DODOMA JUMAMOSI HII USINGOJE KUFIMULIA FIKA UONE LIVE DJ DRUMMER KWA MARA
YA KWANZA MKOANI HUMO!!!
No comments:
Post a Comment