hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, August 10, 2015

TEAM DIAMOND WAFANYA UMAFIA WA KUTISHA NCHINI UINGEREZA, WATANZANIA WAPIGWA NA BUTWAA, WAKENYA WATOA KAURI NZITO..!


FILAMU YA WAKE UP YA MSANII MANAIKI SANGA AMBAY MWISHO WA MWEZI HUU ITAKUWA MTAANI KWA MAELEZO ZAIDI MCHEKI KWENYE Manaiki Sanga instagram utapata mengi zaidi kuhusu movie hiyo

 DEMO YA FILAMU YA GOING BONGO EBU BOFYA HAPA KUONA MAAJABU YA MSANII HUYU WA KITANZANIA ALIYEFANYIWA UMAFIA WA KUTISHA NA MSANII DIAMOND

 Ernest Napoleon staa wa filamu ya Going Bongo
Na Ripota wa maskanibongotz Uingereza
Katika hali isiyokuwa ya kawaida siri nzito imevuja kuhusu shoo anazozifanya nje ya nchi msanii Diamond hasa nchini Uingereza na kubainika kuwa kumbe mwanamuziki huyo hufanya maonesho yake sehemu yenye hadhi ya chini na inayokaliwa na watu masikini kupita kiasi.
Habari za uhakika toka kwa Raia mmoja toka nchini Kenya aliyejitambulisha kwa jina la Otieno ambae pia mshirika kwa moja ya kampuni za mapromota wanawaandalia shoo wasanii wa Afrika Mashariki na Kati ambae anaishi nchini Uingereza alisema" Unajua tatizo la wanamuziki wa Tanzania ni kuficha ukweli wa mambo mara nyingi huwa nasikia wakitamba kuwa wao ni wa kimataifa na shoo zao za kimataifa awa wapi hiyo sio kweli mafano mzuri ni onesho la Diamond alilolifa tarehe 16 may, 2015.
Otieno aliendelea kusema katika onesho hilo Diamond alilifanya katika eneo la East London eneo ambalo hukaliwa na watu masikini na wenye hadhi ya chini na hata kiingilio chao huwa ni kidogo sana " Kwa wanaojiua Uingereza watakuwa wanailijua eneo hili kiukweli ni eneo ambalo wasanii wengi wanaoitwa wenye hadhi ya chini ndiyo hutupwa huk, lakini kumekuwa na uposhwaji na sijui ni promo au nini utakuta msanii anapopata nafasi ya kupelekwa huko basi katika nchi yake hutangaza kuwa anakwenda kufanya shoo Uingereza bila kutaja eneo analokwenda kufanya onesho lake yeye anachong'ang'ania ni Uingereza ili watu watishike na kumuona wa matawi ya juu" Alisema Promota huyo
Promota huyo aliongeza kusema Diamond hajulikani hata kidogo nchini Uingereza ndiyo maana hata hutupwa huko polini na ili kuona kama hajulikana wanaokuja kuhudhuria onesho lake ni watanzania wachache tu ambao hawazidi hata elfu 20 na huwezi kukuta mastaa wakubwa wanashiriki onesho lake kutokana na kutomtambua na kushindwa kufahamu anachokiimba mwanamuziki huyo.
Habari zaidi zilielezwa kuwa wasanii wenye ubavu wa kufanya onesho katika ya mji wa Uingereza ni kama Davido,  Jose Chamilioni, P-Square na wengineo na sababu kubwa ya wasanii hao kufanya maonesho hayo katikati ya mji ni kutokana na Wanigeria wengi kuishi katikati ya mji ambapo ilikadilikiwa wanigeria zaidi ya laki mbili wanaishi katikati ya mji hali, lakini pia kutokana na kazi zao kujulikana kimataifa kuliko za Diamond.
Hata hivyo mkenya huyo alisikitishwa na tukio la Diamond la kumfanyia umafia msanii mwenzake aishie nchini Marekani aliyefika kwenye onesho lake kwa ajili ya kuonesha trailer ya filamu yake iitwayo Going Bongo.
Otieno alisema kuwa  Ernest Napoleon ambae ni msanii wa Kitanzania na ndiye staa wa filamu ya Going Bongo  aliongea na promota wa Bongo Deejays walio-organize concert hiyo kuonyesha trailer ya Going Bongo kabla ya Diamond kupanda jukwaani. Ernest Napoleon alilipia projector pamoja na hela ya kuonyesha trailer yake.
 Mkenya aliongeza kusema Trailer hiyo ilijaribiwa kabla ya shughuli hiyo kuanza, na kutokuwa na hitilafu yeyote kwa upande wa
picha au sauti. Lakini baada ya Ernest Napoleon kupanda jukwaani na kumtangaza Diamond  pamoja
na movie yake ya Going Bongo, deejay wa Diamond aliingia ghafla kwenye mitambo na kuondoa sauti ya
trailer.
Wakati huo huo Diamond alipelekewa Mic backstage na kuanza kuimba wakati trailer hiyo ikionyeshwa.
Ernest Napoleon alishuka kwenye stage kufuatilia kwa nini trailer inaonyeshwa bila sauti, Diamond aliingia stejini na kuanza kutumbuiza huku trailer hiyo ikimuulika kifuani mwake hali ilionesha Diamond aliamua kumfanyia umafia msanii huyo.
Kilichofuatia ni mvutano kati ya Ernest Napoleon na team ya Diamond kuhusu hitilafu ambazo hazikuonekana kabla ya trailer hiyo kuonyeshwa. Promota wa event hiyo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kwa shingo upande walirejesha pesa waliyopewa ingawa hawakulipia projector ambayo ililetwa special kwa ajili ya kuonyesha Going Bongo.
Wiki kadhaa baada ya onyesha la Diamond ambalo lilifanyika eneo la East London ambapo wasanii wengi wa Bongo hufanya matamasha yao kutokana na bei nafuu ya eneo hilo ambalo linakaliwa na watu wenye kipato cha chini mjini, London, Going Bongo ilizinduliwa West London katika eneo ambalo movie au show za muziki kutoka Afrika hazifanyiki kwa sana.
Uzinduzi wa Going Bongo ulihudhuriwa na mastaa wa Uingereza wakiwemo wa jumba la Big Brother Uingereza, Akia Katobe wa Mad Men, Sean Cronin wa Mission Impossible, Grace Andrews wa Towie, Ella Jade wa Apprentice na wengineo wengi. Uzinduzi huo uliandikwa na media nyingi kubwa za Uingereza zikiwemo Daily Mail
 Kitendo hicho kilionekana kumkera mkenya huo na kupelekea kumdharau mwanamuziki huyo kwa roho ya kiswahili aliyomfanyia mtanzania mwenzake.
Gazeti hili lilipomtafuta sataa wa filamu ya Going Bongo Ernest Napoleon ili kuthitibisha taarifa alikiri ni kweli kulikuwa kumetokea tukio hilo dhidi yake kutoka kwa Mwanamuziki huyo lakini alishasamehe muda mrefu na ndiyo maana ni tukio la toka mwezi wa tano lakini yeye hakuwahi kusema lakini kiukweli tukio hilo liliwashtua hata raia wa Tanzania waishio nchini Uingereza.
Upande wa Diamond alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani ili aweze kuzungumzia tukio hilo simu yake haikupokelewa licha ya kugigwa zaidi ya mara sita hadi gazeti hili linaenda mitamboni.
Source: Maskanibongotz

No comments:

Post a Comment