Msanii wa tasnia ya filamu Tanzania Jakob Steven JB ambae kwa sasa imelezwa kuwa kiwango chake cha kuigiza kimeshuka sana kiasi cha kupoteza mvuto kwa mashabiki huku kukiwa na taarifa kuwa huenda kampuni ya usambazaji filamu ya Steps ikampiga chini kwani kazi zake haziuzi kabisa huku zikiwa zimekosa ubunifu. Hata hivyo wadadisi wa mambo wanasema kuwa sababu ya kushuka kisanaa kwa Jb ni kutokana na kuridhika na kulewa ustaa wa kibongo bongo bila kutambua kama Watanzania wengi walimtegemea yeye baada ya kifo cha Kanumba lakini hadi sasa anazidi kurudi nyuma baada ya kupanda ili kuifikisha sanaa ya bongo kimataifa.
Vicent Kigosi Ray ambae nae kwa sasa anapumulia mashine kutokana na kazi zake kushindwa kufikia malengo ya kimataifa na hajawahi kufanya kazi yoyote iliybamba Afrika Mashariki zaidi ya kazi alizowahi kufanya na rafiki yake Marehemu Steven Kanumba na kufanikiwa kuzikonga nyoyo za Wakongo pamoja mashabiki wa Afrika Mashariki na Kati
Sababu nyingine ambayo imemfanya Ray kushuka kwa kiwango chake kiasi cha kuzidiwa hata na msanii chipukizi Manaiki Sanga ambae hana hata miaka mitatu kwenye sanaa, ilidaiwa kulinga kwa msanii huyo na kujiona amemaliza kazi kwa kujurikana Tanzania, baadhi ya waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vya habari waliofika kwenye uzinduzi wa Club Maisha Basement hivi karibuni walikera na tukio la msanii huyu kugoma kupigwa picha na waandishi ili hari siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajiri ya watu maarufu kwa Tanzania, huku msanii mwenzake Jb akikubari kupigwa picha.
Filamu ya Going Bongo ya msanii Ernest Napoleon ambae ni mtanzania aishie nchini Marekani ambayo hivi karibuni ilizinduliwa Zanzibar kwenye tamasha la maonesho ya Filamu ya nchi za Majahazi ZIFF na kushinda tuzo maalum ya filamu bora Afrika Mahariki na kati. Filamu hii imeonekana kuchangia kuwamaliza Jb na Ray kwani imekuwa filamu ya kwanza kuigiza kwenye nchi za Marekani na Tanzania na kushirikisha wasanii wengi huku gharama yake usipime.
Ernest Napoleon
Ernest Napoleon katika tuzo huko Zanzibar
Ernest Napoleon akiwa kwenye uzinduzi wa filamu yake nchini Marekani ambapo filamu hiyo ya Going Bongo hadi sasa imekwisha zinduliwa zaidi ya nchi 7 Duniani.
Libert Msuya mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania ambae ni rafiki wa karibu na Ernest Napoleon ambae nae ni msanii wa Bongo Movie mwenye malengo ya kuifikisha sanaa ya Tanzania kimataifa na sio kutaka kujulikana hapa hapa nchini kama wafanyavyo mastaa wengine.
Hii ndiyo demo ya filamu ya msanii Manaiki Sanga bofya hapa kuiona
Msanii
Manaiki Sanga the Don ambae nae ameleta mapinduzi makubwa kwenye sanaa
ya Tanzania kwa kufanya movie ya kimataifa ambayo haijawahi kufanywa na
msanii yeyote tangu tasnia ya filamu ianze nchini.Manaiki ambae ndiye
staa wa filamu ya Wake Up ambayo amewahenyesha wasanii mastaa zaidi ya
3o wa bongo movie huku filamu hii ikiwa ni ya pili kwake ambapo miaka 3
iliyopita alitoka na filamu ya Ngema ambayo nayo ilibadilisha soko la
filamu Afrika Mashariki na kati na kuwa filamu iliyonunuliwa na watu
zaidi ya laki 9 na elfu tisni. Hata hivyo kwenye hii filamu ya Wake Up
ambayo inatarajia kutoka mwisho wa mwezi huu na kwa maelezo zaidi
unaweza kumfollow Manaiki Sanga kwenye Instagram
Na Hii ni Demo ya Filamu yake ya Going Bongo ebu icheki
No comments:
Post a Comment