Washiriki wa Kili Music Awards wametangazwa March 25 ambapo ndani ya washiriki hao kuna baadhi yao wakiwa hawapo na sababu kubwa ikiwa ni nyimbo zao kukosa maadili ya kitanzania ikiwa kama miongoni mwa vigezo vilivyoorodheshwa na Baraza la sanaa la taifa.
Nyimbo 3 zimeingia kwenye adhabu hiyo ya kutoshiriki kwenye tuzo za KTMA 2013,ukimtoa Madee na Jux msanii Snura nae yupo kwenye kundi hili na kaingia kwa wimbo wake wa Nimevurugwa ambapo ilitoka taarifa ya kufungiwa kwa video hiyo.
Snura ameongea na kuelezea hisia zake baada ya kusikia hiyo taarifa na kuona yupo kwenye list ya wasanii ambao wimbo wake wa Nimevurugwa umetolewa kwenye mashindano hayo ameanza kwa kusema ’Sio nimevugwa peke yake hadi Majanga nao haukuingia’
‘Labda niuzungumzie wimbo wa Nimevurugwa kama ambavyo wamesema hauna maadili unajua hapa kuna kitu kimoja ambacho watu wanatakiwa kukifahamu,si kwamba wimbo hauna maadili hata kidogo,wimbo wa Nimevurugwa ni wimbo mkubwa kwanza unaofundisha na ndani yake nimeimba mambo yanayoihusu jamii’
‘Nadhani waliousikia wameelewa ule wimbo nimeimba nini ila video niliyofanya labda kutokana na kukatika sana kwa hiyo video ndiyo waliyosema haina maadili na ndiyo maana video ikafungiwa lakini sio wimbo wa Nimevurugwa hauna maadili bali video,kwenye tuzo kuna category nyingi sana na ndiyo maana kuna category ya wimbo bora video bora’
‘Hapa kuna vitu viwili tofauti inawezekana wimbo ukawa mzuri ukapata tuzo na inawezekana video ikawa sio nzuri ikakosa tuzo,kwenye wimbo wa Nimevurugwa ilikua inastahili wimbo kama wimbo lakini video imeonekana haina maadili sawa upande wa video isingeingia lakini upande wa audio ungeingia’
‘Nimekua na kijiswali kinachonitatiza kichwani mwangu inawezekana haya mambo sijayaelewa vizuri labda nimeingia kwenye category ya msanii bora chipukizi wa mwaka 2013 ni kipi ambacho nilikifanya kizuri kilichopelekea mimi kuingia hapo’
‘Nauliza hivyo kwa sababu sikuingia kwenye utumbuizaji bora wala hakuna nyimbo yangu yoyote iliyoingia kuwania tuzo si majanga wala nimevurugwa sasa hapo kidogo pananitatiza sijui ubora wangu umetokea wapi hadi kuingizwa kwenye chipukizi’
more athttp://harakatizabongo.blogspot.com/2014/03/snura-atoa-lake-la-moyoni-kuhusu-ktma.html#sthash.7WEZnfr8.dpuf
No comments:
Post a Comment