hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, October 7, 2013

TAZAMA HAPA YALIYOJIRI SERENGETI FIESTA MOSHI KILIMANJARO:



115Shilole kama kawaida

112Shilole akiwa kazini baada ya kutoa mwaliko wa kudance na shabiki 1Juma Nature na timu yake..
 Msanii mkongwe katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake kibao waliofurika vilivyo ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi
 Kundi la Weusi likiongozwa na Joe Makini wakilishambulia jukwaa  kwenye tamasha la serengeti fiesta uwanja wa Majengo mjini Moshi.

 Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,Menina akiimba kwa hisia jukwaani
Mkali mwingine wa bongofleva anaefanya vyema kwenye muziki  huo,akitambulika kwa jina la kisanii Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake  kwenye wakati wa tamasha la serengeti fiesta.

 
 Mwanadada Linah akimpagawisha shabiki wake vilivyo jukwaani  ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Majengo mjini  Moshi.

 Mkali wa shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba kwa hisia jukwaani  kwenye tamasha la serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amekuwa akifanya vyema tangu aibuliwe na Serengeti supa Nyoya kutoka jijini Mbeya,Neylee kwa sasa anakula matunda ya ufanisi wake wa kisanii katika anga ya muziki huo,pichani akiwa kwenye jukwaa la serengeti fiesta  mjini Moshi kwenye uwanja wa Majengo
 Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka nyumba ya vipaji THT,Ally Nipishe akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta .

 Mzee wa masauti kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,Christian Bella akiimba jukwaani.
 Sehemu ya umati wa watu kutoka mjini Moshi wakiwa kwenye tamasha la fiesta usiku ndani ya uwnaja wa Majnego.
 Mwanamuziki wa bongofleva kutoka THT,pichani kati Linah akicheza kwa madaha kabisa na madansa wake jukwaani


Wasanii wanaounda kundi la Jambo Skwadi wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee kabisa  kwenye tamasha la serengeti fiesta lililofanyika kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment