KIGOGO ALIYEJINYONGA KWA KAMBA HADI KUFA YADAIWA NI HASIRA BAADA YA KUGUNDUA MKEWE ANATEMBEA NA RAFIKI YAKE!
Askari akipanda juu ya mti kwaajili ya kuushusha mwili wa marehemu.
BABU SEYA HUENDA AKAACHIWA HURU NA KURUDI URAIANI, KESI YAKE KUANZA KUSIKILIZWA TAREHE 30 MWEZI HUU!
MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kufanya kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe. Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la
Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na
Salum Massati. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo
iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza
huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis
Nguza.
Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii
Nguza ‘Papii Kocha’, Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya
kubaka na kulawiti.
Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga
hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa
wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.
Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10
ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya
kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika
maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment