IMENICHUKUA saa kadhaa kuzungumza na
mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu za Bongo, Elizabeth Michael
'Lulu', hakika yeye ni Lulu kama lilivyo jina lake. (HM)
Kwa wakati huu msanii huyu ni lulu
kweli katika tasnia ya filamu za Bongo Movie. Inaaminika kuwa binti huyo
ambaye ni hivi karibuni tu alifikisha umri wa kuhesabiwa kuwa ni mtu
mzima (miaka 18), naye ameingia katika kundi la wasanii wa kike
wasiokamatika kwa kiwango.
Yeye ndiye Mwigizaji Bora wa Kike kwa
mwaka 2012/2013 kupitia tuzo zilizotolewa na Zanzibar International Film
Festival, anasema kuwa amekua kiumri na sasa yeye ni Lulu mpya mwenye
majukumu ya kuelimisha jamii.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa yuko nje kwa
dhamana kutokana na kukabiliwa na kesi ya kuhusika na mauaji bila
kukusudia ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Alichofanya Lulu sasa ni kuzindua filamu inayokwenda kwa jina la 'Foolish Age'. Filamu hiyo ilizinduliwa
Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wa mamia ya wapenzi wa fani hiyo.
Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wa mamia ya wapenzi wa fani hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Lulu
aliipongeza kampuni inayomsimamia ya Proin Promotion kwa kumpa nafasi ya
kuwafundisha wengine mambo aliyopitia akiwa mtoto ambaye hakupenda sana
kuwasikiliza wakubwa zake.
Lulu ni nani na aliingiaje katika filamu?
Anasema alianza kuigiza alipokuwa na
umri wa miaka minne, lakini hakuwa maarufu. Alipofikisha umri wa miaka
saba, alikutana na Mahsein Awadh 'Dk. Cheni' katika bonaza moja ambalo
pia Dk. Cheni aliaandaa Talent Show. Akiwa na mama yake alimweleza Dk.
Cheni kuwa anaweza kuigiza.
Katika hilo Dk. Cheni anasema:
"Nakumbuka ilikuwa pale Dar West Park, alionyesha maajabu tulipompa
nafasi, yeye ndiye aliibuka namba moja. Alimpita hata Masanja
Mkandamizaji aliyeangukia nafasi ya tatu."
Dk. Cheni anasema alimchukua hadi kwa
uongozi wa kundi la Kaole Sanaa Group ambapo Lulu alifanyiwa usaili na
kupita kwa asilimia. Jukumu kubwa la usalama wa Lulu likaachwa kwa Dk.
Cheni.
Akiwa Kaole, Lulu alichagua jina la
Nemu na alikubalika kutokana na uwezo wake kisanii pamoja na usafi jambo
ambalo hata Herieth Samson 'Kemmy' alishikwa na mshangao baada kufungua
mkoba wa Lulu.
Kemmy alishangaa kukuta vipodozi vya
wakubwa ndani ya mkoba huo wakati Lulu alikuwa badomdogo, alipoulizwa
vipodozi vile ni vya nani, Lulu alimjibu kwa kujiamini tu kuwa ni vyake.
Kemmy anaongeza akisema: "Siku zilivyozidi kwenda mbele alibadilika na
kupenda kuvaa mavazi mafupi, yaani ilifikia hatua picha zake kuchapishwa
gazetini."
Kemmy anafichua kwamba jina la Lulu,
msanii huyo alipewa na Salum Mchoma 'Chiki' mtunzi wa mchezo wa Tetemo
aliyelifuta lile la Nemu.
"Ndoto zangu zimeonekana, wakati
ninaandika mchezo wa Tetemo nikampa jina la Dhahabu lakini kwa sababu
tulikuwa na uhusiano na Mr. Chuzi akaniomba nibadilishe jina ili
tusiwachanganye watu maana naye alikuwa na Jumba la Dhahabu, ndipo
nikampa jina la Lulu," anasema Chiki.
Ushuhuda wake
Lulu mwenyewe anasema ukiacha hayo
yaliyosemwa na hao waliomkuza kisanii, lakini amepitia mengi katika
maisha yake kiasi cha kumpa maumivu makubwa mama yake.
Lakini anaamini yote hayo yalikuwa
njia ya kumfanya aje kuwa mtu wa kuifundisha jamii kupitia sanaa na
ndiyo maana ameandaa filamu inayoelezea maisha yake akiwa chini ya miaka
18.
"Sikumsikiliza mama yangu, wakubwa
zangu, nilikuwa kizani. Yale niliyoyafanya ndio niliamini kuwa ni
sahihi, yaani sikuona hatari yoyote mbele yangu," anasema.
"Hata hivyo naamini ulikuwa mpango wa Mungu kwa yote yaliyotokea. Kuna walionihukumu
, lakini kwa sasa nimekua, ninampenda Yesu na mimi ni Lulu ni mpya. Lengo langu ni kuielimisha jamii kupitia sanaa yangu," anasema.
, lakini kwa sasa nimekua, ninampenda Yesu na mimi ni Lulu ni mpya. Lengo langu ni kuielimisha jamii kupitia sanaa yangu," anasema.
Lulu ndiye mlezi wa familia yake, ndiye anayegharimia ada ya mdogo wake anayesoma katika moja ya shule za kimataifa.
Anasema malengo yake ni kuwa mwigizaji
wa kimataifa na kuitangaza Tanzania kupitia filamu. Anaamini anaweza
kufanya hilo, anaomba Mungu amsaidie.
Baada ya filamu ya 'Foolish Age', Lulu
anatarajia kutoa filamu ya 'Mapenzi Ya Mungu' kazi ambayo
amemshirikisha mama yake marehemu Kanumba, Frola Mtegoa.
Anasema filamu hiyo, nayo bado itakuwa
ikiongelea maisha na mikasa huku akisisitiza kuwa sasa hatotengeneza
wala kuigiza filamu za mapenzi.
Filamu alizoigiza siku za nyuma na
kumpa sifa ni 'Tetemo', 'Jahazi', 'Dira', 'Tufani', 'Gharika' na
'Baragumu'. Chanzo: mwanaspoti
No comments:
Post a Comment