hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, June 17, 2013

YALIOJILI KWENYE TUKIO ZIMA LA BONGOMOVIE AWARDS LILIVYOENDA KUTOKA BLUE PEARL.



OLYMPUS DIGITAL CAMERAJana kwenye hotel ya Blue Pearl kulifanyika tuzo za kwanza ambazo zilitolewa na Steps kwa wasanii wanaofanya nao kazi. Tukio hilo ambalo lilikuwa na limited seats kwa watu walioalikwa tu ikijumisha wasanii,waandishi wa habari,viongozi wa serikali pamoja na wadau wa bongomovie. Tunakupa hiyo coverage incase kama uli-miss hili tukio, walivaa nini mastaa wa movie,red carpet ilikuaje na wapi next time pazingatiwe mpango mzima wa awards uende poa.

RED CARPET:
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Red carpet ilikuwa busy na media tofauti with different taste ya nguo mbalimbali japokuwa card za mualiko zilikuwa zinasema dress code iwe ki-africa(kikwetukwetu).Sasa basi kila mtu akatupia kachumbari yake, waliotupia fresh ni poa..waliochemsha next time tafuteni ma-designer wawasaidie nguo za kuvaa. Hawa ni baadhi ya watu waliovaa vizuri wakapendeza ambao walipita mbele ya camera ya bongomovietz.com


PATCHO MWAMBA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA Mmoja kati ya watu wachache ambao walifuata dress code ya usiku wa Bongomovie Awards, Patcho alitupia  nguo ya kitenge ambayo imeandikwa “DEBOUT CONGOLAIS” INDEPENDENCE 3O JUNNE. Ikimaanisha kwamba kumbukumbu ya miaka 30 ya Uhuru wa Congo. Zaidi ya hapo mkononi alikuwa na fimbo flani hivi,chini alivaa simple sandlez akamalizia na kiko mdomoni.


ZAMARADI MKETEMA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Mc wa usiku wa Bongomovie awards, alipendeza mwanzo mwisho kuanzia chini hadi juu. Hakuna cha kuongeza wala kuzungumzia, purple color ndiyo moja ya rangi zinzo-kick sana kwenye dunia ya fashion. So with that dress ambayo ilikuwa na sehemu kubwa with rangi ya purple, no doubt it was perfect.


RAY
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Suti always inakuwa classic, lakini ikiongezewa kitu cha ziada inakua poa sana. Koti la suti la Ray lilikuwa na touch za animal print plus neck tie aliyotupia ilitisha sana. Yap, that was nice Mr director.


IRENE PAUL
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Best new actress, yeye ni mweupe na nguo yake nyeusi alitokelezea


SHAMSA FORD
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Unaweza kumcheki hapo alivyotokelezea na dress lake jekundu.


JB
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Watoto wa New York wanaiita “All black Everything”, Bonge la bwana he was about to it. Kasori shati lakini still rangi nyeusi kuanzia suti yake,tai hadi kiatu vilimtoa vizuri sana.

WASHINDI WA USIKU HUO
Kwanza kabisa zilianza awards za heshima;

1. STEVEN KANUMBA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Tuzo ilipokelewa na mama yake amaye aliambatana na baadhi ya watu wa Kanumba the great filim.

2. JUMA KILOWOKO – SAJUKIOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERA


Tuzo ilipokelewa na mke wake Wastara Juma


3. HUSSEIN MKIETI – SHARO MILLIONEAOLYMPUS DIGITAL CAMERA
Tuzo hii ilipokelewa na mtu wake wa karibu katika kazi Mzee Majuto

No comments:

Post a Comment