hk CONTACTS

hk CONTACTS

Friday, May 24, 2013

WASANII WA KUNDI LA ZE KOMEDY KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UDHARIRISHAJI!


 Msanii Kiwewe akiwa na mabinti hao ambapo picha hizo zimelalamikiwa sana na wananchi hasa wale wanaopata habari kupitia mitandao ya kijamii.Kwa madai kuwa wasanii hao wamewadharirisha sana mabinti hao na kusema kuwa hiyo siyo sanaa huo ni udharirishaji.

 Wasanii Kiwewe, Kushoto,Masawe katikati na Master Face kushoto

 Msanii Master Face ambae kwenye picha hizo alikuwa kinara wa udharirishaji wa mabinti hao kama anavyoonekana kwenye picha.
Na Livingstone Mkoi
Zile picha za kundi la Ze Komedy la linalorusha kipindi chake kupitia televisheni ya East Africa TV zinazowaonesha wasanii hao wakiwa na mabint ufukweni zimechukua sura mpya baada ya wanasheria  kuahidi kuzisaidia familia za wazaza wa mabint hao. 

Wakitoa maoni yao kwenye mtandao huu wananchi hao ambao wengi wao ni wasomaji wa blog hii na mingine walisema" Nimeziona picha hizo kupitia mtandao wenu kweli imeniuma kama mzazi kwani huo ni unyanyasaji ambao haukubariki hata kidogo naziomba familia za mabint hao kuchukuwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kushtaki ili iwe fundisho kwa wasanii wengine wanaopenda kudhalilisha watu wengine kwa masrahi yao binafsi" Alisema Fortunatus Kasomfi ambae ni mtanzania anaeishi nchini Afrika Kusini 

Aidha nae Hawamu Juma ambae ni mkazi wa Arusha maeneo ya Unga Limited ambae ni Mwanasheria maarufu Mkoani humo alioneshwa kusikitishwa sana na tukio na kuwashauri wazazi wa wasichana hao kumtafuta kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka wasanii hao" Napenda kuwashauri wazazi wa wabint hao kama wanahitaji msaada wa kisheria wanitafute kupitia  simu namba 0713-146416 nitawapa mawazo ya kitaalam ya kisheria ili wasanii hao wafikishwe mahakamani" Alisema Mwanasheria huyo
Wananchi wengi  walitoa maoni yao lakini hata hivyo inadaiwa kulikuwa na ushawishwaji mkubwa kwa mabinti hao wakati wa kupigana picha hizo kwa madai kuwa watasaidiwa kuwa mastaa kama watapiga picha hizo na mastaa hao. 

Na tayari kuna taarifa kuwa baba mzazi wa mmoja wa wasichana hao ambae anaishi Tabata ameanza kuchukuwa hatua za awali kwani siku ya tukio msanii wa kundi la Komedy Manaiki Sanga alifika nyumbani kwa bint huyo na kumchukuwa kwa madai anaenda nae Location. 

Hata katika hali ya kushangaza kiongozi wa kundi hilo Mtanga alishindwa kuchukuwa hatua yoyote dhidi ya wasanii wake walihusika na tukio hilo na kuchukulia ni tukio hilo lilikuwa la kawaida bila kufahamu madhara yake kwa jamii inayohitaji kujifunza mengi mema na ya kuelimisha kupitia wao.

No comments:

Post a Comment