hk CONTACTS

hk CONTACTS

Sunday, May 5, 2013

PICHA MBALI MBALI ZA KANISA LILILOLIPUKA ARUSHA



 Hii ni njia ya kuelekea olasiti kanisani ambapo mlipuko mkubwa umetokea leo asubuhi wakati wa misa ya ufunguzi wa kigango ambapo mgeni rasmi alikuwa ni balozi wa papa nnchini tanzania
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
 Waumini  pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki  wasiamini nini kilichotokea  kutokana na mlipuko mkubwa  uliotokea asubuhi ya leo.


 Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia  leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka.
Polisi waki imarisha doria eneo la tukio   baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi ...Mpaka tunaondoka eneo la tukio Viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa arusha walikuwemo eneo hilo.


The communitytz inawapa pole wote waliofikwa na janga hilo na tunawaombea Mungu  awaponye upesi huku tukiwa watulivu kwenye kipindi hiki kigumu wala tusifikiri kulipa visasi kwa sababu kisasi si juu yetu.

No comments:

Post a Comment