Maisha
hayakuwa ya shida tena, umasikini ambao alikuwa ameupitia pamoja na Gibson
ukaonekana kutokujirudia tena katika maisha yao. Kwa wakati huo kila kitu
kilionekana kubadilika kabisa. Walikuwa na fedha za kutosha, walijenga nyumba ya
kifahari huku wakiwa na magari mawili ya kifahari.
Hawakuishia
hapo, pia walikuwa na miladi mbalimbali ambayo ilikuwa ikiwaingizia kiasi
kikubwa cha fedha. Mapenzi yao yaliendelea kama kawaida, hakukuonekana kama
kulikuwa na mtu ambaye alimchoka mwenzake, walionekana kuzidi kupendana kadri
siku zilivyozidi kwenda mbele.
Prisca
hakujua fedha zile zilitoka wapi, kila alipokuwa akiuliza, alipewa majibu ambayo
wala hayakuonekana kuridhisha japokuwa baada ya muda fulani akaonekana
kuyaamini. Hakujua kama fedha zile ambazo zilikuwa zikitumika kuwatengenezea
maisha yao zilikuwa zikitoka kwa msichana ambaye alikuwa muigizaji mashuhuri wa
filamu za ngono na ndiye ambaye kwa wakati huo alikuwa akimuibia penzi lake
kutoka kwa mume wake, Gibson.
Maisha
yakaendelea kusonga mbele, furaha yao ikaongezeka zaidi na zaidi, mtoto wao
mpendwa, Genuine alikuwa akiwafanya kuwa karibu sana. Kutokana na fedha ambazo
walikuwa nazo katika kipindi hicho, wakaanza kujulikana jambo ambalo likaanza
kuwaweka katika listi ya watu mia moja ambao walikuwa na fedha nyingi ndani ya
jiji la Dar es Salaam.
Maisha
yaliendelea kwenda mbele mpaka pale ambapo Gibson akaelekea nchini Marekani huku
akisingizia kwamba alikuwa akienda kukutana na wafadhiri wa kituo cha watoto
yatima ambacho alikuwa akitarajia kukifungua jijini Dar es Salaam.
Prisca
akaonekana kuridhika, katika maisha yake alikuwa akiwajali sana watoto yatima,
aliwapenda kupita kawaida kwani alijua fika kwamba walikuwa wakiishi katika
mazingira magumu na ya tabu kupita kawaida.
Akampa
baraka zote mume wake kwamba aende na arudi salama ndani ya nchi ya Tanzania ili
waendelee na maisha yao kama kawaida. Moyoni hakujua, hakujua kwamba mume wake
alikuwa akienda kukutana na saplaizi ambayo ilionekana kubadilisha kila kitu
katika maisha yao.
Wiki
ya kwanza ikakatika, japokuwa alikuwa ameahidiana na mumewe kwamba
wangewasiliana lakini haikuwa hivyo, Gibson akaonekana kuwa kimya sana. Hakukuwa
na mawasiliano ambayo yalikuwa yakiendelea, kila alipokuwa akitafutwa, hakuwa
akipatikana.
Baada
wiki mbili kupita hapo ndipo alipokutana na taarifa ambayo ilikuwa imemchanganya
kupita kiasi. Mwanamke ambaye wala hakuwa akifahamiana nae akamfuata nyumbani
pale na kisha kumuonyesha picha ambazo zilikuwa zikimuonyesha Gibson akiwa ndani
ya suti huku pembeni yake kukiwa na msichana ambaye alivalia shela.
Kwa
jinsi picha ile ilivyokuwa ikionekana, wala hakukuwa na kitu cha kujiuliza kama
pale kulikuwa na tukio gani ambalo lilikuwa likiendelea, lilionekana kuwa ni
tukio la harusi kati ya watu hao wawili.
Prisca
akajihisi akikosa nguvu, miguu ikaanza kumlegea na kujikuta akikaa kochini.
Hakuweza kuiamini picha ile, akahitaji picha nyingine zaidi na zaidi,
akaonyeshewa zaidi ya picha ishirini jambo ambalo lilimfanya kuumia
zaidi.
“Mungu
wangu! Gibson” Prisca aliita huku akiziweka zile picha mezani.
Tayari
akaonekana kuchanganyikiwa, hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa amekiona
kwa wakati ule. Machozi yakaanza kumtoka, hapo ndipo alipogundua sababu ambayo
ilimpelekea Gibson kutokuwasiliana nae kwa kipindi kirefu tangu aelekee nchini
Marekani.
“Umezitoa
wapi hizi picha?” Prisca aliuliza huku akionekana kama mtu
aliyechanganyikiwa.
“Kwenye
mtandao. Hivi kwanza unamjua huyo mwanamke?” Mwanamke yule aliyejitambulisha kwa
jina moja tu la Fatuma aliuliza.
“Hapana”
“Pole
sana shoga yangu. Mwanamke huyu ni mcheza fiamu za picha za ngono nchini
Marekani” Fatuma alimwambia Prisca maneno ambayo yakaonekana kumshtua
zaidi.
Prisca
akaonekana kuchanganyikiwa zaidi, akashindwa kuvumilia kukaa mahali pale,
alichokifanya kwa wakati huo ni kuondoka kuelekea chumbani huku akiwa na baadhi
ya zile picha. Akajifungia na kuanza kulia, alilia kwa uchungu, hakuamini kama
kweli Gibson angeweza kufanya kitu kama kile, kufunga ndoa na mwanamke wa
kizungu.
Kilio
chake hakikuweza kumsaidia chochote kile, aliendelea kulia zaidi na zaidi lakini
ukweli bado ukabaki kuwa pale pale kwamba Gibson alikuwa amefunga ndoa na
mwanamke wa kizungu ambaye alikuwa mcheza filamu za ngono, Katie.
Siku
hiyo ndio ilikuwa siku ambayo ilijaa maumivu kuliko siku zote katika maisha
yake. Akatoka chumbani na moja kwa moja kuelekea katika sehemu ya kuegesha
magari na kuchukua gari moja aina ya Verosa, akamuweka Genuine kwenye kiti
kingine na kisha kuwasha gari na kuondoka mahali hapo.
Akili
yake kwa wakati huo ilikuwa ikimwambia afanye kitu kimoja tu, aondoke na
kuelekea nyumbani kwa wazazi wake ambako huko angewaambia kila kitu ambacho
kilikuwa kimetokea na kuwaoyesha zile picha na kuwa kama ushahidi
kwake.
Alipofika,
akamchukua Genuine na kuanza kuingia ndani ya nyumba yao. Alipogonganisha macho
yake na wazazi wake, akaanza kulia, kila kitu kikaanza kujirudia ndani ya kichwa
chake.
“Kuna
nini tena?” Mzee Steven alimuuliza binti yake.
Prisca
hakutoa jibu la swali lile, akabaki akilia zaidi na zaidi. Katika kipindi hicho
alijiona kutokuwa na nguvu za kuongea hata mara moja, alikuwa akijiskia kulia
zaidi na zaidi tena kwa uchungu mkubwa.
“Prisca.
Kuna nini kimetokea?” Mama yake, Bi Magreth aliuliza.
Prisca
hakutoa jibu lolote lile, alichokifanya kwa wakati huo ni kuwaonyeshea wazazi
wake picha zile ambazo alikuwa ameletewa na Fatuma. Wazazi wake wakazichukua na
kuanza kuangalia picha moja baada ya nyingine.
“Mmmh!”
Mzee Steven alisikika akiguna.
“Hii
inawezekana kweli” Bi Magreth aliuliza huku akiziangalia vizuri picha
zile.
Hakukuwa
na mtu ambaye alikuwa akiamini kile ambacho alikuwa akikiona katika picha zile,
waliziona kuwa kama picha za kutengenezwa ambazo mtu yeyote mwenye ujuzi wa
kuzitengeneza angeweza kuzitengeneza.
Chini
ya zile picha kulikuwa na jina la mtandao ambao picha zile zilikuwa
zimechukuliwa jambo ambalo likamfanya mzee Steven kuchukua laptop yake,
akaiunganisha na internet na kisha kuanza kuufungua mtandao ule.
Picha
ambazo alikuwa akiziona katika mtandao ule zilikuwa ni picha zile zile ambazo
walikuwa nazo mikononi na huku nyingine zikionekana kuwa mbaya zaidi ambazo
zilidhihirisha kwamba watu wale walionekana kuwa mume na mke ambao walikuwa
wameingia katika ndoa.
“Hivi
inawezekana kwa Gibson kufanya vitu kama hivi?” Mzee Steven aliuliza huku
akionekana kushangaa.
“Inawezekana
na ndio maana amefanya hayo” Bi Magreth alijibu.
Kitu
walichokifanya mahali hapo ni kuondoka na kuelekea nyumbani kwa mzee Lyimo
ambaye alikuwa baba wa Gibson. Kwa kutumia usafiri wa gari lao, walitumia muda
wa dakika thelathini wakawa wamekwishafika, wakateremka na kuanza kuelekea
katika nyumba hiyo.
Muda
wote huo Prisca alikuwa akiendelea kulia, bado mawazo yake yalikuwa kwa mume
wake ambaye aliamua kufanya jambo lililomshtua kupita kawaida. Hamu ya kuwa
ndani ya ndoa ikanekana kuanza kumtoka moyoni, hakutamani kurudi nyumbani
kabisa.
“Mmmh!
Inawezekana kweli kwa Gibson kufanya haya?” Mzee Lyimo aliuliza huku akionekana
kushtuka kupita kawaida.
Tayari
picha zile zikaonekana kumshtua kupita kawaida, hakuamini kama mtoto wake,
Gibson alikuwa ameamua kuoa nchini Marekani na wakati alikuwa na mke pamoja na
mtoto mdogo ambaye alikuwa na miezi kumi tu.
“Mmmh!”
Mama yake Gibson, Bi Yustina aliguna.
Kila
mmoja akaonekana kutokuelewa sababu ambazo zilimfanya Gibson kuamua kufanya
uamuzi ule ambao ulionekana kumuumiza kila mtu aliyeziangalia picha zile. Prisca
bado alikuwa akiendelea kulia kupita kawaida, moyo wake ukaanza kupatwa na
majeraha ya mapenzi, mtu ambaye alikuwa akimuamini ndiye ambaye alikuwa amekuja
kumuumiza.
“Inaniuma
sana” Prisca aliwaambia huku akiendelea kulia.
“Pole
sana Prisca”
“Sijaumia
kwa yeye kuoa mwanamke mwingine tu bali nimeumia pia kwa aina ya mwanamke
aliyemuoa” Prisca aisema.
“Eeeeh!
Kwani unamjua?”
“Hapana”
“Sasa
ni mwanamke wa aina gani?”
“Mcheza
filamu za utupu”
“Unasemaje?”
Wazazi wote wanne walisema kwa pamoja.
“Ndio.
Ni mcheza filamu mzuri wa utupu duniani” Prisca aliwaambia.
Maneno
hayo ndio ambayo yalionekana kuwachanganya zaidi na zaidi, wakaona kwamba kijana
wao tayari alikuwa amepotea njia kwa uamuzi ule ambao alikuwa ameufanya. Taarifa
kwamba msichana ambaye alikuwa amemuoa alikuwa mcheza filamu za ngono ilionekana
kuwaumiza na kuwakasirisha kupita kawaida.
Walichokijua
ni kwamba kule alipokuwa akifanya kazi Gibson, mbugani ndipo ambapo kulikuwa na
uwezekano wa kukutana na mwanamke yule, walichokitaka kwa wakati huo ni
kuwasiliana na mtu yeyote kutoka katika kampuni ile aliyokuwa akifanyia kazi kwa
ajili ya kutaka kuufahamu ukweli.
“Nina
namba ya rafiki wake wa karibu, Richard” Prisca alisema.
Hapo
ndipo mawasiliano na Richard yalipoanza. Kitu ambacho alitakiwa kukifanya
Richard ni kutoka Morogoro na kuja jijini Dar es Salaaam kwa kutumia usafiri wa
ndege na gharama zote zilikuwa juu ya Prisca.
Ndani
ya masaa kadhaa, Richard alikuwa katika nyumba hiyo ya mzee Lyimo. Kitu cha
kwanza walichokifanya ni kumkabidhi Richard picha zile na kuanza kuziangalia.
Richard akaonekana kushtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona kwa wakati
ule.
“Umeshtuka
nini?” Mzee Lyimo alimuuliza.
“Kuona
picha hizi” Richard alijibu.
“Yaani
unajifanya kama haujui chochote kile”
“Yeah!
Sikujua kama angefanya kitu hiki” Richard aliwaambia.
“Kwa
hiyo ulikuwa ukijua kwamba ana mwanamke?”
“Hapana.
Ila nilijua kwamba anakwenda nchini Marekani kwa sababu aliniaga” Richard
alisema.
“Alipokuaga
alikwambia nini?”
“Kwamba
anakwenda kukutana na wadhamini wa kituo cha watoto yatima ambacho anataka
kuanzisha” Richard alidanganya.
“Kwa
hiyo haujui chochote kuhusu mwanamke huyo?”
“Sijui”
Richard alijibu.
“Hapana.
Kuna kitu unafahamu tu. Naomba utuambie ili tujue pa kuanzia. Unajua
limekwishakuwa suala kubwa sana hili” Mzee Lyimo alimwambia Richard.
Richard
hakutaka kutoa siri ya kitu ambacho kilikuwa kinaendelea. Alikuwa akikataa
kuzungumza kitu chochote mpaka pale alipobanwa sana na ndipo akaanza kuelezea
kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika kipindi cha nyuma.
Prisca
akaonekana kushtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwa
Richard, hakujua kama Richard nae alikuwa akifahamu kila kitu japokuwa alikuwa
mtu wake wa karibu kuliko marafiki wote wa Gibson.
“Kwa
hiyo ukanisaliti? Ukawa unafahamu kila kitu ila haukutaka kuniambia?” Prisca
alimuuliza Richard kwa sauti ya ukali.
“Nilihofia.
Nilichokuwa nikitaka kukiona ni kuona kwamba Gibson anafanikiwa na kutoka kwenye
maisha aliyokuwa anaishi. Niliamini kama angefanikiwa, hata mimi rafiki yake wa
karibu ningefanikiwa pia. Na hiyo ndivyo ilivyokuwa” Richard
alimwambia.
“Unamaanisha
hata hizi fedha zote alizokuwa akizipata Richard zilitoka kwa mwanamke huyu?”
Mzee Lyimo aliuliza.
“Ndio.
Hebu jifikirieni hapo, kama ningeamua kumwambia Prisca juu ya hili, unafikiri
hizi fedha wangezipata? Unafikiri Prisca angekuwa muelewa. Niliiangalia hali
yao, ilikuwa hali mbaya, Prisca alikuwa mjauzito ambaye alikuwa akihitaji kiasi
kikubwa cha fedha kwa ajili ya matunzo. Kitendo cha msichana Katie kuja katika
maisha ya Gibson niliona kuwa kama muujiza ambao wala haukutakiwa kuachwa
kutokea. Na kweli, baada ya kumkubali Katie kisiri, mafanikio yakaja. Najua kwa
kufanya hivyo nimekuumiza sana Prisca ila jua nilifanya hivyo kwa sababu
sikutaka uishi maisha ya tabu mara utakapojifungua. Mshahara wa Gibson haukuwa
ukitosheleza” Richard alimwambia Prisca.
Wote
wakaanza kumuelewa Richard, maneno ambayo alikuwa ameyaongea yakapenya masikioni
mwao na kutulia katika akili yao. Ni kweli alionekana kuwa msaada mkubwa sana
kwa Prisca kwani kama angeamua kusema ukweli, Prisca angekuwa kwenye hali mbaya
katika kipindi kile cha ujauzito.
“Kwa
hiyo haukufahamu kama huyu binti alikuwa mcheza filamu za ngono?” Mzee Steven
aliuliza.
“Sikufahamu
kabisa na ninadhani kwa sababu mimi si mpenzi wa filamu hizo” Richard
alijibu.
“Shukrani
sana. Umeamua kuwa mkweli. Sasa tuambie kwamba hakukwambia kama alikuwa anaenda
kufunga ndoa na msichana huyu?” Mzee Lyimo aliuliza.
“Hakuniambia
kabisa. Kitu ambacho aliniambia ni kwamba alikuwa ameandaliwa saplaizi na
mwanamke huyo, nadhani harusi ndio ilikuwa ni saplaizi yenyewe. Nina uhakika
kwamba Gibson ameoa huku akiwa hataki kuoa. Naamini hilo” Richard
aliwaambia
“Unawasiliana
nae?”
“Hapana.
Nimejaribu kumuandikia barua pepe zaidi ya tatu, naona kimya” Richad
alijibu.
“Dah!
Sasa ataweza kurudi nchini Tanzania?”
“Ataweza.
Gibson anachokiangalia kwa mwanamke yule ni fedha tu, hakuna kingine cha zaidi.
Mitego yake yote ameiweka katika fedha tu kwani anajua kwamba mwanamke yule ana
fedha nyingi” Richard aliwaambia.
Waliendelea
kumuuliza maswali mengi na Richard alikuwa akijibu kwa ufasaha sana bila kusema
kwamba yeye ndiye alikuwa amemshinikiza Gibson kutembea na Katie.
Maisha
yakaendelea zaidi na zaidi, kila siku Prisca alikuwa mwanamke mwenye huzuni,
japokuwa alikuwa na fedha za kutosha lakini fedha hazikuwa na thamani kwake,
thamani kubwa ilikuwa ni Gibson ambaye alikuwa na mapenzi yake ya dhati moyoni
mwake.
Je
nini kitaendelea?
Je
wazazi wa pande zote mbili wataamua nini?
Je
maisha ya Gibson yatakuwaje nchini Marekani?
Je
ndoa yao itadumu?
Hapa
ndipo hadithi inapoanza rasmi.
Itaendelea
saa nne usiku.
igizo hili limedhaminiwa na DICK SOUND MNYAMA,ZANEL BONGO LADIES WEAR,MAC AUTO ACCESSSORIES na FACE BOOK TAKE AWAY Ywauzaji wa chips TAM TAM kinondoni.
contact kwa udhamini 0786435543.
contact kwa udhamini 0786435543.
No comments:
Post a Comment