Siku
ya leo haikuonekana kuwa nzuri kwa Gibson, alikuwa amefika nyumbani hapo huku
akionekana kutokuwa na furaha kabisa, alikuwa katika hali ambayo ilikuwa
ikimuonyeshea kuwa na unyonge wa hali ya juu. Prisca akaonekana kuishangaa hali
ile, hakuwahi kumuona Gibson akirudi katika hali ya unyonge kama siku
hiyo.
Prisca akawa na kiu ya kufahamu sababu
iliyomfanya Gibson kuwa katika hali hiyo lakini wala Gibson hakuwa radhi kusema
zaidi ya kusingizia kwamba hakuwa akijisikia vizuri kiafya, hakutaka kumwambia
Prisca kwamba msichana Katie ambaye alikutana nae ofisini ndiye ambaye alikuwa
amemsababishia hali ile.
Kichwa cha Gibson kikatawaliwa na jina la Katie,
msichana yule, kwake alionekana kuwa msichana mrembo lakini hakuona kama alikuwa
na urembo ambao ungemfanya kumsaliti mpenzi wake, Prisca. Bado alikuwa akimpenda
Prisca, bado alikuwa akiona kuwa na uhitaji wa kuendelea kuwa mwaminifu kwa
Prisca.
“Kichwa kinauma. Na ninadhani hata mafua
yameanza kuuma pia” Gibson alidanganya.
“Pole mpenzi wangu. Ila naona ungekunywa
dawa”
“Nimekwishakunywa ofisini. Nilikuwa sijisikii
vizuri kwa kipindi kirefu sana” Gibson alimwambia Prisca.
Tayari Katie akaonekana kuanza kuharibu kila
kitu moyoni mwake, alijitahidi sana kutokumfikiria lakini jambo hilo likaonekana
kuwa gumu moyoni mwake. Kipindi cha nyuma hasa alipokuwa shuleni kabla hajampata
Prisca alikuwa akitamani sana kuwa na msichana wa kizungu huku lengo lake kubwa
likiwa kama tiketi ya urahisi ya kumfanya kuingia katika nchi za Ulaya au
Marekani.
Kile kitu ambacho alikuwa akikifikiria, leo
kilikuwa kimefika ila kilikuwa kimefika katika wakati mbaya sana. Hakujua ni
kitu gani ambacho alitakiwa kufanya, Katie kwake nae alionyesha kuwa na mapenzi
ya kweli huku akiwa hajui kabisa kwamba msichana yule alikuwa muigizaji bora wa
filamu za ngono duniani.
“Siwezi kumsaliti Prisca” Gibson
alijisemea.
Kesho asubuhi ilipofika, asubuhi na mapema kama
kawaida yake akaanza kwenda ofisini. Bado akili yake ilikuwa ikimfikiria Katie
ambaye alimuona kuwa na asilimia kubwa ya kuharibu mapenzi yake na Prisca.
Gibson hakutaka kuficha, alichokifanya ni kumuita rafiki yake, Richard na kuanza
kumpa taarifa.
“Da! Una zali ile kinoma” Richard alimwambia
Gibson.
“Nina zali?”
“Sasa unataka niliite nini hilo? Demu wa kizungu
mtu wangu, yaani hapo uhakika wa kupata viza nje nje bila usumbufu” Richard
alimwambia Gibson.
“Kwa hiyo unataka nifanyeje?”
“Swali la kitoto hilo wewe. Mchukue tu. Lala
nae. Yeye si ndio anavyotaka. Kula mshiko wewe” Richard alimwambia
Gibson.
“Ushauri wako unaonekana
kutokuniingia”
“Tatizo lako moja. Yaani unataka mpaka Mungu
akutokee usiku akwambie kwamba hiyo ni nafasi yako ya kwenda Marekani na kuutoka
umasikini. Acha hizo Gibson. Wakati mwingine baraka za Mungu zinakuja kimafumbo.
Kama ukiiacha hii, haiji mara mbili” Richard alimwambia
Gibson.
“Lakini si unajua ninaishi na mpenzi wangu,
Prisca ambaye ni mjauzito?”
“Ndio. Ila ukiwa na huyu mzungu, Prisca atajua?
Sikiliza Gibson, ngoja nikueleze kitu kimoja. Wasichana wa Kibongo si wa
kuwawekea dhamana. Unaweza ukagoma kumchukua huyo mzungu kwa ajili yake, halafu
huyo huyo Prisca baadae anakuja kutembea na mshikaji mwingine. Hii ndio nafasi.
Wazungu wanasema ‘Nafasi ya dhahabu haiji mara mbili’. Yaani hata misemo ya
wahenga umeisahau. Kama hautaki, basi acha ila baadae usije ukajuta tu” Richard
alimwambia Gibson.
Maongezi yao yalikuwa yakiendelea zaidi na
zaidi, muda wote Richard alikuwa akimwambia Gibson kuanza uhusiano na Katie.
Ingawa maneno yale yalikuwa hayamuingii kabisa akilini, lakini kadri Richard
alivyokuwa akimwambia na ndivyo ambavyo yakaanza kumingia
akilini.
“Mmmh! Lakini inawezekana bwana kwamba Mungu
ameamua kunipa baraka kimafumbo. Ngoja nami niitumie nafasi hii” Gibson alisema
katika kipindi ambacho alikuwa akiitwa kwenda kuwachukua wazungu wale kuwaingiza
ndani ya mbuga huku Katie akiachiwa nafasi ya mbele kabisa kukaa na dereva,
Gibson.
****
Muda mwingi Gibson alikuwa akiyaangalia mapaja
ya Katie ambaye alikuwa amekaa pembeni yake ndani ya gari lile. Kwa wakati huo,
akili yake haikuwa mahali hapo tena, ilikuwa ikifikiria ngono tu. Tayari
akajiona akianza kuvutwa katika himaya ya msichana yule ambaye alikuwa mcheza
filamu za ngono mkubwa ambaye alikuwa akijulikana sana na watazamaji wa filamu
zile.
Katie alijifanya kutulia huku akimuangalia
Gibson kwa macho ya wizi, tayari akajiona kufanikiwa juu ya lile lengo lake
ambalo alikuwa amejiwekea la kumteka kimapenzi Gibson. Katie akashindwa
kujizuia, akaanza kumgusa gusa Gibson begani mwake, yaani wakati wote alikuwa
akimgusagusa tu.
Walipofika mbugani, wote wakaanza kupitishwa
huku na kule huku wakiangalia wanyama mbalimbali. Kwa wakati huo kichwa cha
Gibson kilikuwa kikifikiria fedha, tayari akaonekana kugundua kuwa kama
angekubali kuwa na Katie, kwa kiasi fulani angekuwa akipata fedha kutoka kwa
msichana huyo.
Japokuwa Katie alikuwa akipenda wanyama na wazo
la kwenda mbugani lilikuwa lake lakini kwa wakati huo hakuwa na habari na
wanyama, kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuwa pamoja na
Gibson tu.
“Will you be ready? (Utakuwa tayari?)” Katie
aliuliza.
“For what? (Kwa lipi?)”
“I need you tonight in my bedroom (Ninakuhitaji
usiku wa leo chumbani kwangu)” Katie alimwambia Gibson.
Mawazo ya Gibson yakahama kwa wakati huo,
akaanza kumkumbuka Prisca wake ambaye alikuwa amemuacha nyumbani akiwa mjauzito.
Maneno yale ambayo aliyaongea Katie yalikuwa na maana kwamba kama alikuwa tayari
kumsaliti Prisca usiku wa siku ile. Kichwa chake hakikuweza kutulia, alimpenda
sana Prisca na alimpa ahadi nyingi huku miongoni mwa ahadi hiyo ikiwa ni ya
kutokumsaliti katika maisha yake yote.
“Haiwezekani” Gibson alijisemea
moyoni.
Huku akiwa amelifikiria jibu hilo, mara
kumbukumbu ya rafiki yake Richard ikaanza kujirudia kichwani mwake. Maneno mengi
ya Richard ambayo yalikuwa yakimtaka kutokuacha kumkubali Katie yalikuwa
yakijirudia kichwani mwake.
Maneno yale bado yalikuwa yakijirudia kwamba ile
ilikuwa ni bahati ambayo Gibson alikuwa ameipata na kamwe asikubali kuipoteza
kwani kama angeipoteza kamwe isingeweza kurudi tena mikononi
mwake.
Tayari hapo akatengeneza jibu la kitu gani
ambacho alitakiwa kukifanya na ambacho kilionekana kuwa uamuzi sahihi kutoka
moyoni mwake. Hakukuwa na kingine alichokifikiria zaidi ya kukubali kile ambacho
kilikuwa kikitakiwa kufanyika na Katie.
“Kwani Prisca atajua? Hawezi jua bwana. Kwanza
kufanya mapenzi na mwanamke wa kizungu bahati kwa sisi wenye ngozi nyeusi
tuishio Afrika” Gibson alijisemea.
Akayarudisha macho yake usoni mwa Katie na kisha
kuachia tabasamu pana ambalo lilionyesha kukubaliana na kile kitu ambacho
alikuwa amezungumza Katie. Matembezi ndani ya mbuga ile yaliendelea zaidi na
zaidi mpaka ilipofika saa kumi na mbili, muda ambao walitakiwa kurudi
hotelini.
Kitu cha kwanza alichokifanya Gibson mara baada
ya kufika hotelini ni kuanza kumtafuta Richard na kisha kumwambia uamuzi ambao
alikuwa ameupanga na ambao aliuona kufaa kwa kipindi hicho.
“Kama umekubali hapo sawa. Wanawake kama hao
ambao wanakuja kuja wewe chukua tu” Richard alimwambia Gibson.
“Ila kitu hii nataka kibaki siri kati yangu na
wewe”
“Usijali. Yule mjauzito hatojua” Richard
alimwambia Gibson.
“Baadae ndio naenda chumbani
kwake”
“Safi sana. Ila kuna kitu nataka
ukifanye”
“Kitu gani?”
“Mkamue hasa ukifika nae kitandani. Yaani mkamue
hadi aite mama” Richard alimwambia Gibson.
“Du!”
“Usishangae wala kushtuka. Kama ukimkamua haswa,
hata akifika Ulaya atakukumbuka na atakuwa akitamani kukutana nawe kimapenzi
zaidi. Ila ukipiga rasharasha, hatorudi tena” Richard alimwambia Gibson ambaye
akaonekana kuyakariri maneno yote.
Ilipofika saa tatu usiku, akashtuliwa simu na
kwamba alikuwa akihitajika chumba namba ishirini na mbili. Kitendo cha kuitwa
tu, tayari hamu ya kufanya mapenzi ikamshika, akaanza kupiga hatua za haraka
haraka kuelekea katika mlango wa kuingilia chumba kile, alipoufikia, akapiga
hodi na kuingia ndani.
Katie alikuwa amejilaza kitandani huku akiwa na
nguo ya ndani tu. Mapigo ya moyo ya Gibson yakaanza kudunda, alipokikodolea
vizuri kifua, kilikuwa kile ambacho alikuwa akikipenda sana na si kama cha
Prisca ambacho kilikuwa kikiendelea kujaa tayari kwa
kunyonyesha.
Akaanza kusogeza pale kitandani. Akapokelewa kwa
mikono miwili na kuanza kuvuliwa nguo. Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa
Gibson kumsaliti Prisca. Kadri alivyokuwa akiucheza mchezo ule na ndivyo ambavyo
kichwa chake kilivyozidi kumkumbuka Prisca.
Walichukua masaa matano, wakawa
wamekwishamaliza, wakaenda bafuni kuoga na kisha Gibson kuondoka chumbani mule
huku mfukoni mwake akiwa amewekewa kiasi cha zaidi ya dola za Kimarekani elfu
mbili mfukoni mwake bila kujijua.
Ilikuwa ni saa tisa usiku katika kipindi ambacho
Gibson alikuwa akirudi nyumbani kwake kwa kutumia bajaji ambayo ilimpeleka
salama. Alipofika nyumbani, akagonga hodi, mfanyakazi wa ndani, Hilda akaja na
kuufungua mlango.
Prisca bado hakuwa amelala, muda wote huo
alikuwa macho akimsubiria mpenzi wake. Usingizi kwake wala haukupatikana kabisa,
mawazo kibao yalikuwa yamemsonga kichwani mwake. Moyo wake haukujisikia amani
kabisa, alikuwa akimkumbuka mpenzi wake kupita kawaida.
Katika kipindi ambacho Gibson aliingia chumbani
mule, akakaribishwa na kumbatio la nguvu na mabusu mengi mashavuni mwake. Kwa
jinsi alivyoonekana kuwa na furaha, Prisca akashindwa kuvumilia, akajikuta
akitokwa na machozi.
“Nimerudi mpenzi. Usilie, niko salama” Gibson
alimwambia Prisca huku moyo wake ukijihukumu kwa kile ambacho alikuwa amekifanya
hotelini.
“Nakupenda mpenzi. Nilikuwa na wasiwasi mpenzi”
Prisca alimwambia Gibson.
“Usijali. Niko salama. Nimekumisi pia” Gibson
alimwambia Prisca huku nae akianza kumbusu.
“Mbona ulizima simu mpenzi?”
“Iliisha chaji. Niliiacha ofisini nikiichaji
huku mimi nikiwa nimewapeleka wazungu mbugani. Ila wazungu wa leo walikuwa
wanazingua sana. Yaani mpaka wakatuchelewesha” Gibson alimwambia
Prisca.
“Pole na kazi mpenzi. Vumilia, hayo ndio
maisha”
“Usijali. Nitafanya kila liwezekanalo kwa ajili
yako” Gibson alimwambia Prisca na kisha kumbusu.
Prisca akatoka nje ya chumba kile na kwenda
kumuandalia mpenzi wake chakula. Muda wote ambao Gibson alikuwa akimwangalia
Prisca, alikuwa akiendelea kujuta moyoni mwake. Alijuta kufanya mapenzi na
Katie, alikosa amani kwa sababu alikuwa amemsaliti mpenzi
wake.
“Sifanyi nae tena. Sitokubali kumsaliti mpenzi
wangu kwa mara ya pili” Gibson alijisemea huku akionekana
kujuta.
Akavua suruali yake. Huku akitaka kuitundika
katika mbao ya kutundikia nguo, akajikuta akigusa kitu kama karatasi mfukoni
mwake jambo lililomfanya kuuingiza mkono mfukoni mwake. Kiganja chake kikagusa
karatasi kadhaa, alipozitoa zilikuwa dola.
Akazihesabu haraka haraka, zilikuwa ni dola elfu
mbili ambazo zilikuwa zaidi ya milioni tatu. Uso wake ukaonyesha tabasamu,
akaonekana kufurahi kupita kawaida. Akatamani kuruka ruka kwa furaka, akajikuta
akijilaza kitandani.
“Haya ndio maisha bwana. Kwa staili hii, wala
siwezi kumuacha, kesho nampa dozi zaidi” Gibson alisema huku
akitabasamu.
Je nini kitaendelea?
Je nini kitatokea Gibson atakapoendelea zaidi
kutembea na Katie?
Je Prisca atajua?
Na je Katie atajua kama Gibson ana mchumba
mjauzito?
Itaendelea kesho saa nne usiku
IMEDHAMINIWA NA DICK SOUND,NA FACEBOOK TAKE AWAY wauzaji wa chips tamudar es salaam.
No comments:
Post a Comment