hk CONTACTS

hk CONTACTS

Tuesday, May 28, 2013

MSANII WA MAIGIZO DUDE AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

Kulwa Kikumba, msanii wa maigizo aliye maarufu kwa jina la Dude, amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mama yake mzazi asubuhi ya leo jijini Dar es salaam. Katika ujumbe wake ambao ameutuma kwa wadau wake, msanii huyo ameandika

"Ndugu zangu wapendwa, nimefiwa na mamaangu mzazi niliyempenda kuliko mtu yeyote kwenye dunia hii, leo saa 12 asubuhi. Inna Lillah waa inna illah rajiun" 
(Pichani ni msanii huyo akiwa kwenye gari akimpeleka mama yake hospitalini kwa matibabu, kumbe mama huyu tayari alishakuwa ameiaga dunia"

Mimi binafsi, wadau wangu na wadau wa Jukwaa Huru Media Inc kwa ujumla, tunampa pole Dude kwa pigo hili. Mungu ampe nguvu ya kuweza kusimama imara katika wakati huu mgumu kwake na familia yake kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment