BAADA YA KICHAPO NA KALAPINA HII NDIO KAULI YA CHIDI BENZ
"mimi jana
nilienda maisha mida flani kama ya saa tisa hivi sawa, nikamuona yule Nikki
mbishi, halafu nikaona aaah sijawahi kumpa sapoti hafu mbali ya hiyo, namsikiaga
kuna mtu anatutukanaga, anamtukanaga Nikki Mbishi yule mtoto ananitukanaga na
mimi unanielewa, kwahiyo nikasema anyway for the support, na yule ni kama mdogo
wangu, mi natokea pale kwenye stage, i know kwa kawaida mi nikitokea sehem
lazima watu washangilie sana na watu wameshangilia sana ile club maisha, so nia
yangu ilikua mimi pale ni kuchukua ile mic, ki ukweli hata nilikua sijui ni show
ya nani, nachojua nikwamba nilimuona Nikki nikazunguka halafu kutoka VIP kwa nia
moja yaani kabisa kwamba namfata yule Nikki pale nikitokea stage najua watu
watapiga yowe nampa sapoti pale nachana nini bana sapoti kwa Nikki Mbishi nini
halafu mimi najikata, nikachukua mic kwa Gilla ni kwamba watu wameshangilia
nikapiga verse kidogo pale watu wakashangilia, nikataka kusema bwana shout out
kwa nikki mbishi nimependa show yake anavyofanya..........
kumbe ile show ni ya kina Pina na wala hakuna
ubaya mimi kupanda stage na kutaka pale kutoa shout out eidha kwa Nikki au kwa
yeye Kala Pina au msanii yoyote yule ambae namzuka nao kwa hiyo pina na wenzie
wametokea kwa nyuma mmoja akanisukuma pina ye akanipiga ngumi, nilikua namsikia
mtu kama anasema asiehusika na hii show ashuke, sikujua kama ni kala pina,
ningejua kama ni yeye ningejua ni ize yeye ni msanii wa hiphop na mi ni msanii
wa hiphop.
TAZAMA VIDEO CHID
AKIPIGWA:
kumpiga mtu ni hali ya wewe na yeye mpigane
puuuh puuuh puuuh mtu mbili halafu ukanipiga, ndio uwaambie watu umempiga Chidi
Benz, sio nyie mmetokea kwa nyuma, mgongoni kwangu huku mmekuja mkanisukuma
mmoja kanipiga ngumi, mpo ishirini sijui wangapi show yenu kumbe maisha club,
mnasema mmenipiga???? we unaonge mtu umempiga
hakuna mtu ambae hajui,
hakuna msanii ambae hajui, zamanai nilikua nagombana na kina pina kwasababu
walikuwa wanawaonea wasanii, walishawaonea wakina mangwea, o ten, mimi nipo na
kina FA namkimbiza pina na kundi lake mimi, yeye na anajua, so mi hapa hajawa
hata mara moja kunichengua, wao wameshawahi kufanya ugomvi na mimi msasani club,
mimi peke yangu wao kibao na wakanishindwa umenielewa sijui, kwa hiyo pina sio
kwamba mimi ananiweza yule ni jitu tu na manyama yake
kibao"
No comments:
Post a Comment