hk CONTACTS

hk CONTACTS

Thursday, April 18, 2013

FM ACADEMIA WAACHIA MBILI KWA MPIGO KWENYE UJIO WAO MPYA

 Kimya kingi kina mshindo mkubwa sana, moja kati ya zile band kongwe tanzania ni FM ACADEMIA yenye zaidi ya miaka kumi na tano ( 15) kwenye game bila yakutetereka, Ukimya wao wanauvunja soon wiki mbili zijazo kwa kuachia nyimbo mbili mpya kwa pamoja. Akiongea na HYPER HK manager wa band ya fm academia MR KELVIN amesema '' tangu mwaka 2010 hatujatoa nyimbo mpya muda wote huo tulikuwa jikoni tunapika mambo na sasa vitu vimeshahiva ,Tunaachia nyimbo mbili kwa pamoja ya kwanaza inaitwa CHUKI YA NINI utunzi wake RAIS WA BAND NYOSHI ELISADAT na ya piuli inaitwa FATAKI utunzi wake KING BLAISE. Manager wa band ya FM ACADEMIA KELVIN amejitamba sana na kusema ni nyimbo kali sana ambazo zitasumbua sana band zote hapa nchini na nje ya tanzania,

 Pia alisema uzinduzi wa nyimbo hizo mbili mpya utafanyika katika KIJIJI CHA MAKUMBUSHO KIJITONYAMA na LISTENING PARTY yake itafanyika NEW MAISHA CLUB ambapo kila siku ya jumatano huwa wanapiga hapo,Nachowaomba wapenzi wa FM ACADEMIA mjitokeze kwa nguvu zote kuja kuona band yenu ya ukweli.

Alimaliza kwakusema anawapenda sana mashabiki wa fm academia kwani niwavumilivu na watakula mbivu hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment