Baada ya
maneno ya chinichini kumtafuna staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa
amepungua mwili, ameibuka na kuweka bayana kuwa hakuna kingine kilichosababisha
zaidi ya mazoezi.
Hivi
karibuni kuliibuka maneno kuwa staa huyo amekonda kupita kiasi ambapo vyombo
mbalimbali vya habari viliripoti juu kupungua kwake huko.
Baadhi
ya watu wake wa karibu, walianza kuzungumzia sababu ‘chungu mbovu’ huku kila
mmoja akisema sababu anazozijua mwenyewe.
Punde
baada kurejea Rwanda walipokwenda kuhudhuria tuzo za filamu nchini humo, Ray
aliamua kuweka picha zake kwenye mtandao wake zinazomuonesha akifanya mazoezi na
kufafanua kuwa amemaliza ubishi kwa wadau wa filamu waliokuwa wakijadili juu
kupungua kwake.
No comments:
Post a Comment