MSANII Wema
Sepetu amemlipia faini ya shilingi milioni 13 msanii mwenzake, Kajala Masanja,
na kumfanya awe huru. Mapema leo, hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mcheza
filamu za Kitanzania anayefahamika kwa jina la 'Kajala Masanja' na mumewe mbele
ya Hakimu 'Sundi Fimbo' kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es
salaam.
Katika hukumu
hiyo 'Kajala' amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi
milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni
200.
Kajala alikuwa
anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe 'Faraji Agustino' kukumbwa na
makosa ya kutakatisha fedha haramu.
Hata hivyo
baada ya hukumu hiyo kutolea mahakamani hapa, mwanadada maarufu hapa Bongo
anayefahamika kwa jina la Wema Sepetu' aliweza kujitolea yeye mwenyewe kiasi cha
Tsh. milioni 13 kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya kumlipia msanii mwenzake wa
filamu 'Kajala' asiweze kutumikia adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5
jela.
Hii ni mara ya
pili kwa msanii 'Wema Sepetu' kujitolea kiasi kikubwa cha fedha kusaidia msanii
mwenzake.!
Kwa sasa
Kajala yupo nyumbani kwao maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na
ndugu na jamaa.
ZEDDYLICIOUS
BLOG INAKUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AKUZIDISHIE WEMA SEPETU KATIKA KILA
UTALOLIFANYA, NI WACHACHE SANA WENYE MOYO KAMA WAKO!!
No comments:
Post a Comment