RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIPEANA MKONO NA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA |
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIWAJIBIKA KWENYE MOJA YA MAJUKUMU YAKE HIVI KARIBUNI
MKUTANO WA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA KATA YA NAKASANGWE TEGETA JIJINI DAR
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA NAKASANGWE KWENYE MKUTANO ALIOUANDAA YEYE MWENYEWE KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIWA AMEKAA CHINI PAMOJA NA NA WAKAZI HAO AMBAO KWA KIPINDI KIREFU WALIKUWA WANAISHI KWA HOFU NA MASHAKA KWA KUHOFIA KUPIGWA MABOMU NA POLISI KWA KILE KILICHOELEZWA KUWA WALIKUWA WAMEVAMIA ENEO HILO LA MWEKEZAJI JAMBO LILILOPIGWA NA WAKAZI HAO
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA AKIWALINGANISHA WAKAZI HAO JINSI UWIANO ULIVYO KWA KATI YA MTU ALIYEKUWA NACHO NA ASIYEKUWA NACHO AKIPIGIA MFANO KUWA HUYO JAMAA MFUPI NDIYE MAKAZI WA ENEO HILO NA HUYO BAUNSA NDIYE FISADI ANAETAKA KUDHURUMU ENEO HILO.
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MH PAUL MAKONDA
Na Livingstone Mkoi
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wakazi wa Kata ya Wazo na
Nakasangwe wamemuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumuongezea cheo Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni kwa kile kilichoelezwa amewasaidia kuwarejeshea
amani waliyoitafuta kwa zaidi ya miaka mitano.
Wakaiongea
mwandishi wa E-fm Radio bwana Livingstone Mkoi kwenye mkutano wa hivi
karibuni ulioandaliwana Mkuu huyo wa Wilaya ambae ni kipenzi cha watu
walisema" Ndugu Mwandishi kwa sasa tunajiona ni watanzania halisi kwani
hali ilikuwa mbaya kuhusu huu mgogoro wa ardhi ambao uliwasababishia
umasikini mkubwa baada ya kubomolewa makazi yao na mali nyingi
kuharibiwa" Alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Dula
Mgogoro
huo wa ardhi uliwaathiri wakazi wa eneo hilo ambao wengi wa wafuasi wa
chama cha Mapinduzi CCM na kupelekea suala hilo kufika kwenye mamlaka za
kisheria na walishashinda na walitakiwa kulipwa fidia lakini katika
hali nyingine upande wa wa pili ambao wanadai ni wawekezaji walikata
rufaa na kutaka kesi iendelee ambapo hadi sasa bado kesi hiyo
inaendelea.
Mkuu
wa Wilaya aliandamana na Mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni, Afisa
Ardhi wa Manspaa na maofisa wengine toka Wilaya akiwepo RPC Wambura na
kwa kauri yake Mkuu wa Wilaya hiyo baada ya kupata maelezeo ya toka kwa
wananchi ambao walimweleza wazi kuwa kufika hapo kwa mgogoro huo
kulikuwa kumesababishwa na mkuu wa Wilaya aliyepita kabla yake ambae
walimtuhumu kuwa alikuwa akishirikiana na mafisaidi kuwakangamiza
wananchi pamoja na kutoa amri kwa jeshi la Polisi kuwabomolea nyumba zao
na kuwalipua kwa mabomu ya machozi.
Hivyo
kutokana na Mkuu huyo wa Wilaya kuonesha moyo wa dhati wa kuwapigania
wananchi hao wanyonge na kufuta kauri ambayo awali ilikuwa inatumiwa na
viongozi wa Manspaa kuwa watu hao ni wakaimbizi kutokana na ukweli
kwamba watu wote wanaoishi eneo hilo ni watanzania halisi, wanchi hao
walifarjika na kumuomba Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kumuongezea cheo Mh
Makonda na kumpa ukuu wa Mkoa kwa vile kwa kipindi kifupi alichooingia
madarakani tayari amefanya mambo makubwa hasa kuhusu migogoro ya ardhi
sehemu mbalimbali ya Wilaya hii hivyo wanaamini endapo akiwa mkuu wa
Mkoa nadhani atahakikisha Mkoa mzima unakuwa na amani pamoja na vijana
wengi kupata ajira.
No comments:
Post a Comment