hk CONTACTS

hk CONTACTS

Tuesday, March 11, 2014

SASA KIMENUKAA WAJERUMANI WAZUSHA BALAA HOFU KUBWA YALIKUMBA JIJI LA DAR NA VITONGOJI VYAKE, NA HIVI NDIVYO UFUNGAJI WA VIFAA UNAVYOENDELEA KWENYE STUDIO ZA KITUO KIPYA CHA RADIO!


 Hapa Wataalam toka Serikali ya Ujerumani ambao ndiyo mafundi wakiwa na mafundi wa 93.7  Fm wakiendelea na ufungaji wa mitambo hiyo ambayo ni ya kwanza Tanzania na haipatikani kwenye studio yoyote kwenye redio nchini.

  Mjerumani akiseti Vifaa ndani ya Redio ya 93.7 Fm iliyopo Kawe Beach Jijini Dar es Salaam
 Vifaa ndani ya Redio ya 93.7 Fm iliyopo Kawe Beach Jijini Dar es Salaam



  93.7 Fm iliyopo Kawe Beach jinsi itakavyoonekana.

Na Livingstone Mkoi
Maandalizi ya ufungaji vifaa vipya vya studio ya kisasaa ya
Radio ambayo bado haiwekwa wazi lakini itakuwa inapatikana kwa
kwenye masafa ya 93.7 Fm yanaendelea kwa kasi kubwa huku watalaamu toka nchi ya Ujerumani wakihusishwa.

Paparazi wetu alifanikiwa kufika kwenye studio hizo na
kujionea vifaa vya mitambo ya studio hiyo ambayo kwa mujibu wa Wjerumani hao Tanzania itakuwa ya kwanza kutumiwa na radio hiyo mpya ya burudani nchini.
 Hata hivyo habari zaidi zilisema Wajerumani hao ambao sasa wana wiki ya pili wakifanya kazi hiyo usiku naa mchana na tayari wako kwenye hatua za mwisho na muda wowote Jiji la Dar na mikoa ya jirani kitanuka vibaya kutokana na kuwaa hewani kwa redio hiyo inayotarajia kusikika mikoa zaidi ya saba kwa maraa ya kwanza.
Aidha mmoja wa wadau wa redio hiyo ambae aliomba hifadhi ya jina lake alisema " Kiukweli kwamba hali si swali kwa sasa jiji limeanza kuzizima kwani Serikali kupitia mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imeshatoa baraka zake kwa kituo hicho kurusha matangazo yake na vyombo vyote vya habari vimeshapewa taarifa juu ya ujio wa redio hiyo ya vijana na watu wote" Alisema dada huyo ambae ni Miss Tanzania
 Studio hizo zitakazokuwa kwenye mwambao wa fukwe ya Kawe Beach huku mitambo yake ya kurushia matangazo ikiwa kwenye viunga vya milima ya Kisalawe na katikati ya Bahari.
" HABARI ZAIDI JUU YA UJIO WA REDIO HIYO FATILIA GAZETI LA MASKANI BONGO KILA JUMATANO LITAKUWA LINAKUPA MCHONGO NZIMA"

No comments:

Post a Comment