hk CONTACTS

hk CONTACTS

Friday, November 15, 2013

IMEBAKI SIKU MOJA TU TUKIO LA AJABU KULIKUMBA JIJI LA MBEYA, WANANCHI WASHIKWA NA HOFU, XTREME DEEJAYZ WAZUSHA BALAA SHUGHURI ZOTE ZA SIMAMA!



 Timu ya mpira ya Mbeya City itakuwa moja ya watu watakaokuwa kivutia kwenye uchezaji wakati zitakapokuwa zinaporomoshwa na DVJ MAJIZO 4 CHIZO" DAD" huku kushoto kwake atapatikana ZUNGU MNYAMA pamoja na Hyperman Hk.
Wachezaji wa timu ya mpira ya Mbeya City wakishangilia moja ya ushindi wa magoli ya timu yao, ambapo wacheaji hao watapongezana ndani ya Club Maisha jumamosi hii.
 Jiji la Mbeya
SOMA ZAIDIDD
 Hivi ndivyo shughuri za wananchi wa Mbeya zinavyoendelea, lakini siku ya Jumamosi hii tarehe 16 kazi zote zinatarajia kusimama kupisha show moja tu ya vijana wa  XTREME DEEJAYZ  kwa staili ya LIVE DJ DRUMMER itakayofanyika ndani ya Club Maisha Mbeya.

  Hawa ni maelfu ya mashabiki waliofika Club Maisha DODOMA kwenuye show ya XTREME DJ LIVE DRUMMER.


Majizo 4 Chizo "DVJ MAJEY" akifanya balaa kwenye moja ya show za XTREME LIVE DJ DRUMMER mjini Dodoma hivi karubuni.
 Sakina Shabani na Amida Mlima
Katika hali isiyotarajiwa wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake wako kwenye maandalizi makubwa ya kuipokea timu ya XTREME DEEJAYZ inayotarajia kuwasili kesho Ijumaa kwa njia ya ndege kwa ajili ya tukio moja tu la kukumbukwa litakalofanyika ndani ya Club Maisha.
Habari zaidi zilizothibitishwa na waandishi wetu toka Mbeya zinasema kuwa wananchi  hasa wapenda burudani wamekuwa roho juu tangu waliposikia matangazo ya ujio wa vijana hao machachari toka Jijini Dar wa XTREME DEEJAYZ ambapo hutumia mfumo wao wa DJ LIVE DRUMMER kuwa watatua mkoani humo kwa ajili ya kufanya onesho moja tu.

Wakiongea na XDEEJAYZ kwa njia ya simu wanachi hao walisema kuwa " Kwa kweli kwanza tuna hamu ya kumuona huyo Zungu Mnyama tunasikia mambo yake ni balaa kubwa hivyo tunawasubir kwa hamu sana ili tuje tupate burudani" Alisema dada mmoja ambae ni mwanafunzi wa chuo 

Aidha katika hatua nyingine onesho hilo linatarajia kunogeshwa na vijana wa timu ya mpira ya Mbeya Citu ambao watajipongeza kwa kufanya vizuri kwenye mechi zao kwenye ligi hivyo wananchi wote watakaofika Club Maisha humo watapata furusa ya kupiga picha na wachezaji hao. 

GAZETI LA MASKANI BONGO LITAKUJIA HIVI KARIBUNI KAA MKAO WA KULA, IFANYE SIKU YAKO KUWA YA AMANI NA FURAHA KWA KUSOMA GAZETI LA MASKANI BONGO! 

No comments:

Post a Comment