hk CONTACTS

hk CONTACTS

Tuesday, October 8, 2013

PENNY WA DIAMOND AJIPANGA KWA MAISHA YA “UJANE”, UKIMUONA KWA SASA ANATIA HURUMA ATAMANI KUMPIGIA MAGOTI WEMA SEPETU IKI WARUDIE USHOSTI WAO KUMKOMESHA DIAMOND, ASEMA ALIMPA KILA KITU MPENZI WAKE LAKINI WAPI!








Na Mwandishi Wetu
Ama kweli wahenga waliosema mtoto akililia wembe usimkataze mwanchie tu acheze nao utakapomkata ndipo atatia adabu!
Usemi huu ndio unaonekana kumkuta mtangazaji nyota wa kituo bora cha tv cha DTV Pennieh Mwingilwa “33” ambae kwa sasa hivi hana amani ya maisha tena kufuatia mchumbaake Diamond kuripotiwa amerudiana na Wema na siku za hivi karibuni walionekana nchini China wakila bata batani.
Habari za uhakika toka kwa beki tatu wa Penny ambae aliomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa “ Kwa kweli Pennieh anaihaitaji msaada wa kufarijiwa kwa sasa ishu ya Diamond kuonwa China akiwa na Wema Sepetu imemuweka vibaya kiasi cha kushindwa kula na juzi kapoteza fahamu baada ya pressure kupanda kwa kiwango cha juu” Alisema dada huyo
Aidha habari zaidi ziliendelea kusema kuwa mtangazaji huyo kwa sasa anajipanga na maisha ya “ujane”  kwani anamini mwisho wa mchezo umefika kati yake na Diamond “ Pennieh ameanza kujipanga katika maisha mapya ya ujane sasa hivi ameanza kushindwa kazini kwake  maneno Komakoma na staafu wenzake japo kurejea kwenye hali yake ya kawaida” Ilielezwa
Hata hivyo mtangazji amekuwa akiumia zaidi akifikiria namna ya kurejesha mahusiano yake na Wema tena pamoja na kampuni yake ya zamani ambayo ni Kajala, Lulu, Jenifa Pemba, ambao hao wote walikuwa wamemtenga kwa kosa la kupora mume wa mtu Diamond ambae alikuwa na Wema Sepetu.
"Nimempa kila alichohitaji mwanaume huyu hata vingine ambayvyohajawahi kupewa lakini wapi na kuifanyia wema familia yake lakini wapi aah kha jamani ngojeni nipumue tu"
Katika hatua nyingine familia ya Diamond imepigwa na butwa kwa taarifa hizo za Diamond na Pennieh kurudiana kwani ni dhahili kuwa familia hiyo ilikuwa inafurahishwa na mkwe wao Pennieh ambae anafiwa sana kwa mambo ya kupika mahanju mati ambapo tofauti na Wema Sepetu ambae yeye hajui chochote.

No comments:

Post a Comment