Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young wa Philippines baada ya kutwaa taji hilo.
Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi wa pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana.
Warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo.
Mlimbwende huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa Marekani, ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji la mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, na akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi kutokea".
Maelfu ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia mitaani tangu mwezi uliopita wakipinga kufanyika kwa mashindano hayo nchini Indonesia, nchi ambayo ina Waislam wengi zaidi duniani, wakiyaita mashindano hayo kuwa ni “maonyesho ya ngono”.
Upinzani huo uliwalazimisha waandaji kulihamisha tukio hilo kutoka Jakarta kwenda Nusa Dua, kusini mwa Bali.
Katika kulifahamu hilo mapema, balozi za Marekani, Uingereza na Australia zilitoa vibali vya kwenda kwenye shindano hilo kwa kuwaonya wenye kusafiri kwamba tukio hilo la mashindano ya urembo lilikuwa limepangwa kuvurugwa. Hata hivyo, polisi wa Indonesia walisema hapakuwepo na vurugu zozote siku ya Jumamosi.
Marine Lorphelin, mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ufaransa, alishika nafasi ya pili na Carranzar Naa Okailey Shooter (23) kutoka Ghana alikuwa wa tatu.
No comments:
Post a Comment