TUMEINYAKA kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, |
Habari
zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo
huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya
Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha akalazwa, akachomwa sindano na
kutundikiwa dripu.
Akizungumzia hali hiyo, Penny aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli
alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa
vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.
Hata hivyo, habari tulizozipata
wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini
na anaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment