hk CONTACTS

hk CONTACTS

Wednesday, March 19, 2014

SHEKH SHARIF KHAMIS, USTAADH KESSY WATANGAZA VITA NA WACHAWI WOTE TANZANIA, WAAMBIWA HERI WAJISALIMISHE MAPEMA OFISNI KWENYE MSIKITI WA KICHANGANI MAGOMENI JIJI DAR!


 Ustaadh Kessy na Shekh Sharif Khamis wakipeana miko no baada ya kikao chao na waandishi wa habari hivi karibuni kwa ajili ya utambulisho wa ofisi yao mpya ya Manaklin Natural Heling Clinic iliyopo kwenye msiki wa Kichangani Magomeni Mapipa.
 Ustaadh Kessy akizungumza na wanahabari kuitambulisha ofisi ya  Manaklin Natural Heling Clinic iliyopo kwenye msiki wa Kichangani Magomeni Mapipa. Na ndipo wananchi wanapaswa kufika hapo kwa ajili ya mahitaji yote yanayohusiana na Shekh Sharif Khamis

 Shekh Sharif Khamis akiwazizitizia watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari juu ya kufika kwa wingi ofisini kwake kwa ajili ya kuwasadia wenye shida na wanaoteseka na magonjwa mbalimbali .

Na Sakina Shabani
Yule kijana mwenye kalama ya ajabu nchini Tanzania na Dunia nzima maarufu kama Shekh Sharif Khamis akishirikiana na msemaji wake Ustaadh Kessy maarufu kama Mtoto wa Mchungaji wanatarajia kutikisa nchi kwa mihadhara mbalimbali kuanzia mtaa hadi mtaa kwa ajili ya kusafisha mambo mabaya pamoja na kuwakomboa wananchi wanaoonewa na wachawi.

Akiongeana Gazeti hili msemaji wa Shekh Sharifu Khamis alisema " Tuna programu kubwa ya kufanya mikutano nchi nzima lakini tutaanzia Jijini Dar na tayari hivi karibuni tulifanya mkutano mmoja huko Tandika ambao hakika ulikuwa na mafanikio makubwa" Alisema Ustaadh huyo
Aliendelea kusema kuwa kufuatia taarifa hiyo kamati ya Mihadhara hiyo ambayo iko chini ya Shekh Sharif wananchi wanaojiona wao ni washirikina au wanafanya mambo yasiyompendeza mungu ni heri wakajisalimisha kabisa kwenye ofisi zao za Manaklin Natural Heling Clinic zilizopo kwenye msikiti wa Kchangaji Jiji Dar kabla ya balaa kuwakuta huko majumbani kwao.
Hata hivyo Ustaadhi huyo ameendelea kutoa uwito kwa Watanzania wote bila kujali imani zao kufika ofisini kwa kijana huyo kwa ajili ya kupata dua za aina tofauti kwa mahitaji watakayoyahitaji na waliotayari wawasiliane nao kwa namba 0717-688792  hii ni ya Shekh Sharif Mwenyewe, au wapige namba hii .0713-247829 ni ya kwake msemaji.

No comments:

Post a Comment