Gibson akaonekana kuanza kujisahau kabisa, mara kwa
mara alikuwa akifanya mapenzi na Katie hotelini. Alimsaliti sana Prisca lakini
katika hayo yote ambayo alikuwa akiyafanya, yalikuwa yakimpatia fedha nyingi kwa
kumridhisha Katie kwa namna ambayo alikuwa akiitaka.
Kuanzia hapo hakukuwa na siri tena, mapenzi yao
yakajulikana kwa kila mfanyakazi wa kampuni ile ya Utalii katika mbuga ya
wanyama ya Mikumi. Mara kwa mara walikuwa wakitoka na kwenda katika sehemu
nyingine mbalimbali, kimuonekano wa nje, Gibson alikuwa amekwishaanza
kubadilika.
Siku ambayo waigizaji walitakiwa kurudi nchini Marekani
ikafika lakini Katie hakutaka kurudi, bado alikuwa akihitaji muda zaidi wa
kutanua na Gibson ambaye alionekana kuwa kama mpenzi wake wa
dhati.
Akili ya Gibson ilikuwa ikifanya kazi sana na mara kwa
mara alikuwa makini sana na kila kilichokuwa kinaendelea katika maisha yake.
Kwanza hakutaka kuonyesha mabadiliko yoyote yale kwa mpenzi wake, Prisca, kila
siku alikuwa akimjali huku kila alipokuwa akirudi nyumbani kwake alikuwa akikaa
nae karibu sana.
Ilikuwa ni vigumu sana kwa Prisca kugundua kama Gibson
alikuwa ameanza kutoka nje ya uhusiano wao katika kipindi hicho. Mapenzi
yalikuwa yameongezeka hasa na hii ilitokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho
alikuwa akikipata kila siku.
“Bado miezi miwili mpenzi nikajifungue” Prisca
alimwambia Gibson ambaye akaonyesha tabasamu pana.
Gibson akaanza kulishaika tumbo la Prisca, tabasamu
likaongezeka usoni mwake, maneno ambayo aliambiwa na Prisca yalionekana
kumfurahisha kupita kawaida. Bado alikuwa akitamani kupata mtoto katika maisha
yake, kila siku alitamani kuitwa baba.
“Nitafurahi nikimuona mtoto wangu. Ninapenda kuiona
damu yangu” Gibson alimwambia Prisca.
Huo haukuwa mwisho wake wa kuendelea kuwa pamoja na
Katie, mahusiano yao yalikuwa yakiendelea kama kawaida huku wakiendelea kusafiri
sehemu mbaimbali na kufanya kila kitu kama wapenzi.
Bado Prisca hakuonekana kuwa na wasiwasi, moyo wake
ulikuwa ukiendelea kumuamini Gibson kupita kawaida. Hata alipokuwa akihoji
kuhusu fedha nyingi ambazo alikuwa akizipata, majibu ambayo alikuwa akipewa
yalionekana kumridhisha kwa asilimia mia moja.
“Kuna safari tunatakiwa kwenda kesho” Gibson alimwambia
Prisca.
“Safari ya wapi tena?”
“Mbuga ya Ngorongoro. Kuna wazungu wamepanga kwenye ile
hoteli yetu wanataka tuwapeleke huko” Gibson alimwambia
Prisca.
“Na mtarudi lini?”
“Bado sijajua. Nafikiri bosi akituambie siku ya kurudi,
nitakutaarifu simuni” Gibson alimwambia Prisca.
Prisca hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, bado
moyo wake ulikuwa ukimuamini Gibson kupita kawaida, kwa moyo mmoja akakubaliana
nae. Gibson akaonekana kuwa na furaha, hadi kipindi hicho hakuamini kama kweli
Prisca alikuwa akikubaliana nae na wakati alikuwa
akimsaliti.
Kiukweli, hakukuwa na safari ya Ngorongoro kama
alivyomwambia Prisca bali alikuwa akitaka kupata siku tatu mfululizo kuwa pamoja
na Katie. Mapenzi ya Katie yakaonekana kumlevya kupita kawaida, fedha ambazo
alikuwa akipewa mara kwa mara na mwanamke huyo wa kizungu zikanekana kumteka
kupita kawaida.
Safari hii, Kati akalipa kiasi cha dola elfu moja mia
tano kwa ajili ya Gibson na kumkabidhi bosi wa kampuni ile. Wote kwa pamoja
wakaanza kuelekea Arusha ambako huko wakala sana raha na kisha kuelekea visiwani
Zanzibar. Katika kila kona ambazo walikuwa wakienda, walikuwa wakipeana mapenzi
ya dhati huku Gibson akijitahidi kufanya ngono na Katie, ile ngono ya uhakika
ambayo ilikuwa ikimchanganya sana Katie.
Walikaa Zanzibar kwa siku mbili na ndipo wakarudi tena
Morogoro.Gibson hakutaka kumwambia Katie kama alikuwa na msichana ambaye alikuwa
akiishi nae kwa wakati huo, alichokisema yeye ni kwamba alikuwa akiishi peke
yake na wala hakuwa na uhusiano na msichana yeyote yule.
“Kwa hiyo utanioa?” Katie
alimuuliza.
“Muda wowote ukitaka” Gibson alimwambia Katie ambaye
akaonyesha tabasamu pana la furaha.
Katie hakutaka kuendelea kukaa sana Tanzania,
alichokifanya kwa wakati huo ni kumuachia kiasi cha dola elfu kumi Gibson na
kisha kuelekea nchini Marekani huku akiahidi kuwasiliana nae kila
siku.
Maisha ya Gibson yakaanza kubadilika, kila mtu mtaani
alionekana kushangaa lakini wala hakuonekana kujali. Shida ambazo walikuwa
wamezipitia zikaonekana kubaki kuwa kama historia ambazo zingekumbukwa tu
vichwani mwao.
Bado Prisca hakuonekana kufahamu sehemu ambazo fedha
zile zilipokuwa zinatoka kwani kila alipokuwa akiuliza, majibu ambayo alikuwa
akipewa hayakuwa yakieleweka sana. Gibson hakutaka kubadilika, bado mapenzi yake
kwa Prisca yalikuwa yakiendelea vile vile, alikuwa akimpenda kupita kawaida huku
akimfanya kuwa na furaha kila siku.
Mawasiliano kati yake na Katie yalikuwa yakiendelea
mara kwa mara kwa siri, alikuwa akipigiwa simu na kuongea nae, alikuwa akitumiwa
zawadi mbalimbali pamoja na fedha nyingine nyingi.
Gibson hakutaka kumsahau rafiki yake, Richard ambaye
alikuwa amempa ushauri mkubwa wa kutembea na Katie, mtu huyo ndiye ambaye
alionekana mtu ambaye alikuwa na ushauri mkubwa katika maisha
yake.
“Sasa si unaona bahati hiyo. Ulikuwa unaogopa nini
sasa?” Richard alimuuliza Gibson.
“Unajua nilikuwa nimefunikwa na ujinga. Asante sana
Rich”
“Usijali. Wewe ni rafiki yangu, hautakiwi kuwa na
wasiwasi” Richard alimwambia Gibson.
“Asante sana. Ila kuna safari nataka unisindikize”
Gibson alimwambia Richard.
“Safari ya wapi tena?”
“Kuelekea Dar es Salaam”
“Kufanya nini?”
“Kununua gari. Nataka niwe na gari kwanza kabla ya
kujenga nyumba” Gibson alimwambia Richard.
“Dah! Yaani umeshafika huko. Kweli ulikuwa na
bahati”
Siku mbili zilizofuata, wakasafiri kuelekea jijini Dar
es Salaam ambako wakarudi na gari aina ya Opa. Kuanzia hapo maisha ya Gibson
yakabadilika kabisa. Kwanza akaacha kazi na kuanzisha biashara zake kubwa.
Maisha yake yakahamia jijini Dar es Salaam. Katika kipindi hiki hakutaka kuishi
na Prisca kama mpenzi wake bali akaanza kuishi nae kama mke wake baada ya
kufunga ndoa huku wakiishi pamoja na mtoto wao wa kiume,
Genuine.
“Mwaka umepita bila kukuona mpenzi” Gibson alikuwa
akichati na Katie katika mtandao wa Bearshare
“Nafahamu mpenzi. Mambo yamekuwa mengi sana. Ila
ningependa uje huku ukae nami japo mwezi mmoja tu” Katie alimwambia
Gibson.
“Mimi kuja huko?”
“Ndio. Kwani kitu gani
kinashindikana?”
“Tatizo viza. Ubalozi wenu unasumbua
sana”
“Usijali. Nitakutumia kadi ya mualiko. Kila kitu
nitashughulikia mimi mwenyewe” Katie alimwambia Gibson.
“Sawa”
Kuanzia hapo, Gibson akaanza kujiandaa na safari ya
kwenda Marekani kuonana na mpenzi wake, Katie. Maandalizi yake yakaanza kuwa ya
chini chini ila mwisho wa siku akaamua kumwambia Prisca juu ya safari
hiyo.
“Kwa hiyo unakwenda kufanya nini
huko?”
“Kuna watu fulani nakwenda kuonana nao kwani nataka
kufungua kituo cha watoto yatima. Mimi kama mimi siwezi, ninahitaji sana msaada
kutoka kwa watu wengine. Ninakwenda huko kuonana nao, kama mambo yatakwenda
vizuri, nafikiri watanisaidia kiasi fulani cha fedha na ndipo nitaanza kufungua
kituo hicho” Gibson alidanganya.
“Kwa maana hiyo hao watakuwa kama
wafadhili?”
“Yap. Hiyo ndio maana yangu mke wangu” Gibson
alimwambia Prisca.
Siku zikaendelea kukatika huku mawasiliano ya siri kati
yake na Katie yakiendelea kama kawaida. Waliwasiliana kwa meseji huku wakati
mwingine wakiwasiliana kwa maongezi kwa kutumia mitandao
mbalimbali.
Kila mmoja akaonekana kuwa katika mapenzi ya dhati
lakini kwa Gibson akaonekana kuishi kwa tahadhali ili mke wake kipenzi asiweze
kufahamu kitu chochote ambacho kilikuwa kinaendelea kwa wakati
huo.
“Nitakufanyia saplaizi kubwa sana mpenzi” Katie
alimwambia Gibson.
“Niambie mpenzi. Ipi hiyo?”
“Mbona una haraka? Wewe njoo tu uje uione” Katie
alimwambia Gibson.
Kuanzia hapo akili ya Gibson haikuweza kutulia, kila
wakati alikuwa akiifikiria saplaizi ambayo alikuwa ameambiwa na Katie.
Alishindwa kufahamu ni kitu gani ambacho alikuwa ameandaliwa. Alitamani aondoke
haraka na kwenda nchini Marekani, akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikiendelea
kufikiria fedha tu.
Alikuwa na fedha nyingi sana lakini bado alikuwa
akihitaji zaidi na zaidi. Ndoto za kuwa tajiri mkubwa ndizo ambazo zilikuwa
zikitawala kichwani mwake kwa wakati huo. Alihakikisha anakuwa na Prisca mpaka
pale atakapoona amechukua fedha nyingi sana kutoka kwa msichana huyo ambaye
kwake alionekana kutoka katika moja ya familia za kitajiri nchini
Marekani.
“Mmmh! Huyu msichana ameniandalia nini? Mbona ameushtua
sana moyo wangu? Haiwezekani, ngoja niende” Gibson
alijisemea.
Siku ya kupanda ndege ikawadia na kama kawaida alifika
uwanjani katika muda husika na kupanda ndege ya shirika la American Airways. Kwa
wakati huo akili yake ilikuwa ikifikiria saplaizi ambayo alikuwa ameandaliwa na
mpenzi wake, Katie.
Moyoni hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo
ingemletea matatizo makubwa, hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ilimpelekea
hata Prisca kufahamu kile ambacho alikuwa amekifuata nchini Marekani, hakujua
kama saplaizi hiyo ndio ambayo ilimpelekea kujuta kutembea na Katie huku
saplaizi hiyo ndio ikimuwekea kifungo cha kuonana na Prisca kwa kipindi kirefu
kijacho.
Je nini kitaendelea nchini
Marekani?
Je ni saplaizi gani ambayo Katie ameandaa kwa ajili ya
Gibson?
Je Prisca ataweza kugundua kinachoendelea kwa mpenzi
wake?
Itaendelea kesho saa nne
No comments:
Post a Comment