hk CONTACTS

hk CONTACTS

Wednesday, May 15, 2013

MCHEZA FILAMU ZA NGONO SEHEMU YA 4.




Gibson akaonekana kuanza kujisahau kabisa, mara kwa mara alikuwa akifanya mapenzi na Katie hotelini. Alimsaliti sana Prisca lakini katika hayo yote ambayo alikuwa akiyafanya, yalikuwa yakimpatia fedha nyingi kwa kumridhisha Katie kwa namna ambayo alikuwa akiitaka.
Kuanzia hapo hakukuwa na siri tena, mapenzi yao yakajulikana kwa kila mfanyakazi wa kampuni ile ya Utalii katika mbuga ya wanyama ya Mikumi. Mara kwa mara walikuwa wakitoka na kwenda katika sehemu nyingine mbalimbali, kimuonekano wa nje, Gibson alikuwa amekwishaanza kubadilika.
Siku ambayo waigizaji walitakiwa kurudi nchini Marekani ikafika lakini Katie hakutaka kurudi, bado alikuwa akihitaji muda zaidi wa kutanua na Gibson ambaye alionekana kuwa kama mpenzi wake wa dhati.
Akili ya Gibson ilikuwa ikifanya kazi sana na mara kwa mara alikuwa makini sana na kila kilichokuwa kinaendelea katika maisha yake. Kwanza hakutaka kuonyesha mabadiliko yoyote yale kwa mpenzi wake, Prisca, kila siku alikuwa akimjali huku kila alipokuwa akirudi nyumbani kwake alikuwa akikaa nae karibu sana.
Ilikuwa ni vigumu sana kwa Prisca kugundua kama Gibson alikuwa ameanza kutoka nje ya uhusiano wao katika kipindi hicho. Mapenzi yalikuwa yameongezeka hasa na hii ilitokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho alikuwa akikipata kila siku.
“Bado miezi miwili mpenzi nikajifungue” Prisca alimwambia Gibson ambaye akaonyesha tabasamu pana.
Gibson akaanza kulishaika tumbo la Prisca, tabasamu likaongezeka usoni mwake, maneno ambayo aliambiwa na Prisca yalionekana kumfurahisha kupita kawaida. Bado alikuwa akitamani kupata mtoto katika maisha yake, kila siku alitamani kuitwa baba.
“Nitafurahi nikimuona mtoto wangu. Ninapenda kuiona damu yangu” Gibson alimwambia Prisca.
Huo haukuwa mwisho wake wa kuendelea kuwa pamoja na Katie, mahusiano yao yalikuwa yakiendelea kama kawaida huku wakiendelea kusafiri sehemu mbaimbali na kufanya kila kitu kama wapenzi.
Bado Prisca hakuonekana kuwa na wasiwasi, moyo wake ulikuwa ukiendelea kumuamini Gibson kupita kawaida. Hata alipokuwa akihoji kuhusu fedha nyingi ambazo alikuwa akizipata, majibu ambayo alikuwa akipewa yalionekana kumridhisha kwa asilimia mia moja.
“Kuna safari tunatakiwa kwenda kesho” Gibson alimwambia Prisca.
“Safari ya wapi tena?”
“Mbuga ya Ngorongoro. Kuna wazungu wamepanga kwenye ile hoteli yetu wanataka tuwapeleke huko” Gibson alimwambia Prisca.
“Na mtarudi lini?”
“Bado sijajua. Nafikiri bosi akituambie siku ya kurudi, nitakutaarifu simuni” Gibson alimwambia Prisca.
Prisca hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, bado moyo wake ulikuwa ukimuamini Gibson kupita kawaida, kwa moyo mmoja akakubaliana nae. Gibson akaonekana kuwa na furaha, hadi kipindi hicho hakuamini kama kweli Prisca alikuwa akikubaliana nae na wakati alikuwa akimsaliti.
Kiukweli, hakukuwa na safari ya Ngorongoro kama alivyomwambia Prisca bali alikuwa akitaka kupata siku tatu mfululizo kuwa pamoja na Katie. Mapenzi ya Katie yakaonekana kumlevya kupita kawaida, fedha ambazo alikuwa akipewa mara kwa mara na mwanamke huyo wa kizungu zikanekana kumteka kupita kawaida.
Safari hii, Kati akalipa kiasi cha dola elfu moja mia tano kwa ajili ya Gibson na kumkabidhi bosi wa kampuni ile. Wote kwa pamoja wakaanza kuelekea Arusha ambako huko wakala sana raha na kisha kuelekea visiwani Zanzibar. Katika kila kona ambazo walikuwa wakienda, walikuwa wakipeana mapenzi ya dhati huku Gibson akijitahidi kufanya ngono na Katie, ile ngono ya uhakika ambayo ilikuwa ikimchanganya sana Katie.
Walikaa Zanzibar kwa siku mbili na ndipo wakarudi tena Morogoro.Gibson hakutaka kumwambia Katie kama alikuwa na msichana ambaye alikuwa akiishi nae kwa wakati huo, alichokisema yeye ni kwamba alikuwa akiishi peke yake na wala hakuwa na uhusiano na msichana yeyote yule.
“Kwa hiyo utanioa?” Katie alimuuliza.
“Muda wowote ukitaka” Gibson alimwambia Katie ambaye akaonyesha tabasamu pana la furaha.
Katie hakutaka kuendelea kukaa sana Tanzania, alichokifanya kwa wakati huo ni kumuachia kiasi cha dola elfu kumi Gibson na kisha kuelekea nchini Marekani huku akiahidi kuwasiliana nae kila siku.
Maisha ya Gibson yakaanza kubadilika, kila mtu mtaani alionekana kushangaa lakini wala hakuonekana kujali. Shida ambazo walikuwa wamezipitia zikaonekana kubaki kuwa kama historia ambazo zingekumbukwa tu vichwani mwao.
Bado Prisca hakuonekana kufahamu sehemu ambazo fedha zile zilipokuwa zinatoka kwani kila alipokuwa akiuliza, majibu ambayo alikuwa akipewa hayakuwa yakieleweka sana. Gibson hakutaka kubadilika, bado mapenzi yake kwa Prisca yalikuwa yakiendelea vile vile, alikuwa akimpenda kupita kawaida huku akimfanya kuwa na furaha kila siku.
Mawasiliano kati yake na Katie yalikuwa yakiendelea mara kwa mara kwa siri, alikuwa akipigiwa simu na kuongea nae, alikuwa akitumiwa zawadi mbalimbali pamoja na fedha nyingine nyingi.
Gibson hakutaka kumsahau rafiki yake, Richard ambaye alikuwa amempa ushauri mkubwa wa kutembea na Katie, mtu huyo ndiye ambaye alionekana mtu ambaye alikuwa na ushauri mkubwa katika maisha yake.
“Sasa si unaona bahati hiyo. Ulikuwa unaogopa nini sasa?” Richard alimuuliza Gibson.
“Unajua nilikuwa nimefunikwa na ujinga. Asante sana Rich”
“Usijali. Wewe ni rafiki yangu, hautakiwi kuwa na wasiwasi” Richard alimwambia Gibson.
“Asante sana. Ila kuna safari nataka unisindikize” Gibson alimwambia Richard.
“Safari ya wapi tena?”
“Kuelekea Dar es Salaam”
“Kufanya nini?”
“Kununua gari. Nataka niwe na gari kwanza kabla ya kujenga nyumba” Gibson alimwambia Richard.
“Dah! Yaani umeshafika huko. Kweli ulikuwa na bahati”
Siku mbili zilizofuata, wakasafiri kuelekea jijini Dar es Salaam ambako wakarudi na gari aina ya Opa. Kuanzia hapo maisha ya Gibson yakabadilika kabisa. Kwanza akaacha kazi na kuanzisha biashara zake kubwa. Maisha yake yakahamia jijini Dar es Salaam. Katika kipindi hiki hakutaka kuishi na Prisca kama mpenzi wake bali akaanza kuishi nae kama mke wake baada ya kufunga ndoa huku wakiishi pamoja na mtoto wao wa kiume, Genuine.
“Mwaka umepita bila kukuona mpenzi” Gibson alikuwa akichati na Katie katika mtandao wa Bearshare
“Nafahamu mpenzi. Mambo yamekuwa mengi sana. Ila ningependa uje huku ukae nami japo mwezi mmoja tu” Katie alimwambia Gibson.
“Mimi kuja huko?”
“Ndio. Kwani kitu gani kinashindikana?”
“Tatizo viza. Ubalozi wenu unasumbua sana”
“Usijali. Nitakutumia kadi ya mualiko. Kila kitu nitashughulikia mimi mwenyewe” Katie alimwambia Gibson.
“Sawa”
Kuanzia hapo, Gibson akaanza kujiandaa na safari ya kwenda Marekani kuonana na mpenzi wake, Katie. Maandalizi yake yakaanza kuwa ya chini chini ila mwisho wa siku akaamua kumwambia Prisca juu ya safari hiyo.
“Kwa hiyo unakwenda kufanya nini huko?”
“Kuna watu fulani nakwenda kuonana nao kwani nataka kufungua kituo cha watoto yatima. Mimi kama mimi siwezi, ninahitaji sana msaada kutoka kwa watu wengine. Ninakwenda huko kuonana nao, kama mambo yatakwenda vizuri, nafikiri watanisaidia kiasi fulani cha fedha na ndipo nitaanza kufungua kituo hicho” Gibson alidanganya.
“Kwa maana hiyo hao watakuwa kama wafadhili?”
“Yap. Hiyo ndio maana yangu mke wangu” Gibson alimwambia Prisca.
Siku zikaendelea kukatika huku mawasiliano ya siri kati yake na Katie yakiendelea kama kawaida. Waliwasiliana kwa meseji huku wakati mwingine wakiwasiliana kwa maongezi kwa kutumia mitandao mbalimbali.
Kila mmoja akaonekana kuwa katika mapenzi ya dhati lakini kwa Gibson akaonekana kuishi kwa tahadhali ili mke wake kipenzi asiweze kufahamu kitu chochote ambacho kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.
“Nitakufanyia saplaizi kubwa sana mpenzi” Katie alimwambia Gibson.
“Niambie mpenzi. Ipi hiyo?”
“Mbona una haraka? Wewe njoo tu uje uione” Katie alimwambia Gibson.
Kuanzia hapo akili ya Gibson haikuweza kutulia, kila wakati alikuwa akiifikiria saplaizi ambayo alikuwa ameambiwa na Katie. Alishindwa kufahamu ni kitu gani ambacho alikuwa ameandaliwa. Alitamani aondoke haraka na kwenda nchini Marekani, akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikiendelea kufikiria fedha tu.
Alikuwa na fedha nyingi sana lakini bado alikuwa akihitaji zaidi na zaidi. Ndoto za kuwa tajiri mkubwa ndizo ambazo zilikuwa zikitawala kichwani mwake kwa wakati huo. Alihakikisha anakuwa na Prisca mpaka pale atakapoona amechukua fedha nyingi sana kutoka kwa msichana huyo ambaye kwake alionekana kutoka katika moja ya familia za kitajiri nchini Marekani.
“Mmmh! Huyu msichana ameniandalia nini? Mbona ameushtua sana moyo wangu? Haiwezekani, ngoja niende” Gibson alijisemea.
Siku ya kupanda ndege ikawadia na kama kawaida alifika uwanjani katika muda husika na kupanda ndege ya shirika la American Airways. Kwa wakati huo akili yake ilikuwa ikifikiria saplaizi ambayo alikuwa ameandaliwa na mpenzi wake, Katie. 
Moyoni hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ingemletea matatizo makubwa, hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ilimpelekea hata Prisca kufahamu kile ambacho alikuwa amekifuata nchini Marekani, hakujua kama saplaizi hiyo ndio ambayo ilimpelekea kujuta kutembea na Katie huku saplaizi hiyo ndio ikimuwekea kifungo cha kuonana na Prisca kwa kipindi kirefu kijacho.

Je nini kitaendelea nchini Marekani?
Je ni saplaizi gani ambayo Katie ameandaa kwa ajili ya Gibson?
Je Prisca ataweza kugundua kinachoendelea kwa mpenzi wake?
Itaendelea kesho saa nne

No comments:

Post a Comment