Pages

Tuesday, April 16, 2013

CANDY CALFONIA ALIA NA PENZI LA MASHAKA

 Moja kati ya wasichana waliopata nafasi ya kung'aa nyota zao katika tamasha kubwa tanzania la NI WAKATI WAKO TOUR linalomilikiwa na television ya dtv ni SNURA,SCOPION GALS,JASSY QUEEN na mwanadada Huyu WAKUITWA CANDY CALFONIA,Hivi karibuni ameamua kueleza hisia zake kupitia wimbo wake mpya kabisa wa PENZI LA MASHAKA......Akiongea na HYPERMAN HK, CANDY CALFONIA amesema wimbo wake mpya huo wa penzi la mashaka ameufanya katika studio za NK PRODUCTION chini ya  PRODUCER mahiri CHRISTONE.......Alifunguka zaidi kuhusu wimbo wake wa PENZI LA MASHAKA alisema'' wimbo huu unahusu mapenzi ya utapeli,visa,na vituko katika swala zima la mapenzi.ni ishu inayowatokea watu wengi kwa kuwaamini wapenzi wao asilimia mia 100 na kutojali maneno ya watu, kwa kawaida imeshazoeleka maneno ya watu ni sumu.

 Lakini yeye anasema sometimes maneno ya watu yanasaidia na yanajenga,sababu yote aliokuwa anaambia na watu na kuyakataa ndio yale mpenzi wake ndio alikuwa anafanya na kujuta kwanini hakuwasikiliza walimwenzgu.

Kiukweli ni wimbo mzuri sana na ukitoka lazima utawashika sana watu wa lika tofauti. aliendelea kujigamba mwanadada CANDY CALFONIA. pia alisema wimbo huo anategemea  kuuachia tarehe za mwisho wa mwenzi huu wa nne, video itafata baada ya audio kutoka na mfumo huu wa digital kuwa tatizo ,inabidi kwanza aanze kuachia audio. anachooomba ni suport kwa wadau na mashabiki wa muziki wa bongo fleva tanzania,yuko tayari kukosolewa na kuonywa kama atakosea na sio kusimangwa,alisema'' CANDY CALFONIA  pia ametoa namba yake ya simu kwa watakao taka kumpa maoni na ushauri ambayo ni 0659132373.Namba hii ni kwa ajili ya maswala ya muziki tu na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment