hk CONTACTS

hk CONTACTS

Saturday, March 16, 2013

HIKI NDIO KILICHOMFANYA MUIGIZAJI RAY KIGOSI KUKONGOLOKA, ATOA VITHIBITIISHO KIBWENA'

 


Baada ya maneno ya chinichini kumtafuna staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa amepungua mwili, ameibuka na kuweka bayana kuwa hakuna kingine kilichosababisha zaidi ya mazoezi.

Hivi karibuni kuliibuka maneno kuwa staa huyo amekonda kupita kiasi ambapo vyombo mbalimbali vya habari viliripoti juu kupungua kwake huko.

Baadhi ya watu wake wa karibu, walianza kuzungumzia sababu ‘chungu mbovu’ huku kila mmoja akisema sababu anazozijua mwenyewe.

Punde baada kurejea Rwanda walipokwenda kuhudhuria tuzo za filamu nchini humo, Ray aliamua kuweka picha zake kwenye mtandao wake zinazomuonesha akifanya mazoezi na kufafanua kuwa amemaliza ubishi kwa wadau wa filamu waliokuwa wakijadili juu kupungua kwake.

“Nikiwa mazoezini… nadhani maswali yatakuwa yamekwisha baaada ya kuwawekea picha hizi…” aliandika Ray mtandaoni.

No comments:

Post a Comment