hk CONTACTS

hk CONTACTS

Monday, March 4, 2013

MAPACHA WATATU WAFUNIKA UZINDUZI WA ALBAM YA YARAB NAFSI


Chezea mapacha watatu weweee

Mgeni rasmi CAPTEN JOHN KOMBA

Jana ilikuwa bonge la uzinduzi, it was classic baba ake..... MASHABIKI wa muziki wa dansi nchini, mwishoni mwa wiki walishuhudia uzinduzi wa albamu ya pili ya bendi ya Mapacha Watatu.
Uzinduzi huo uliyofanyika katika Ukumbi wa Business Park, ulishuhudiwa na mashabiki lukuki.
Bendi hiyo, ambayo mwanzoni ilianzishwa kama kikundi kwa ajili ya wasanii kujiongezea kipato, huku wakiendelea kufanya kazi kwenye bendi zao na mwaka 2011, wasanii hao waliamua kuacha vibarua vyao na kuunda bendi yao rasmi.
Wasanii waliondoka kwenye bendi zao walikuwa ni Jose Mponezya ‘Jose Mara’ kutoka FM Academia, kutoka Twanga Pepeta ni Khalidi Chuma ‘Chokoraa’ na Kalala Junior, ambaye baadaye aliamua kurejea Twanga.
Albamu ya kwanza ya bendi hiyo, iliyoitwa Jasho la Mtu, ilizinduliwa mwaka 2010.

MAPACHA WATATU

ALBAM IKIZINDULIWA NA CAPTEN JOHN KOMBA

No comments:

Post a Comment