MAPACHA WATATU WAFUNIKA UZINDUZI WA ALBAM YA YARAB NAFSI
Chezea mapacha watatu weweee
Mgeni rasmi CAPTEN JOHN KOMBA
Jana ilikuwa bonge la uzinduzi, it was classic baba ake.....
MASHABIKI wa muziki wa dansi nchini, mwishoni mwa wiki walishuhudia uzinduzi wa
albamu ya pili ya bendi ya Mapacha Watatu. Uzinduzi huo uliyofanyika katika
Ukumbi wa Business Park, ulishuhudiwa na mashabiki lukuki. Bendi hiyo, ambayo
mwanzoni ilianzishwa kama kikundi kwa ajili ya wasanii kujiongezea kipato, huku
wakiendelea kufanya kazi kwenye bendi zao na mwaka 2011, wasanii hao waliamua
kuacha vibarua vyao na kuunda bendi yao rasmi. Wasanii waliondoka kwenye
bendi zao walikuwa ni Jose Mponezya ‘Jose Mara’ kutoka FM Academia, kutoka
Twanga Pepeta ni Khalidi Chuma ‘Chokoraa’ na Kalala Junior, ambaye baadaye
aliamua kurejea Twanga. Albamu ya kwanza ya bendi hiyo, iliyoitwa Jasho la
Mtu, ilizinduliwa mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment