Pages

Wednesday, March 20, 2013

BIA YA KILIMANJARO IMESAINI MKATABA NA BARAZA LA SANAA KUENDELEA KUDHAMINI TUZO ZA MUZIKI TANZANIA KWA MUDA WA MIAKA MITANO

inafurahi kuwatangazia wapenzi wote wa burudani kuwa KILIMANJARO imesaini mkataba na Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA) kuendelea kudhamini Tuzo za Muziki Tanzania kwa miaka mitano zaidi hadi mwaka 2018. Hafla fupi ya kusaini mkataba huu imefanyika leo katika ofisi za TBL na kuhudhuriwa na viongozi wa BASATA pamoja na COSOTA. Kilimanjaro Music Awards mwaka huu itafanyika Juni 8 katika ukumbi wa Mlimani City. Majina ya wanamuziki watakaogombea tuzo yatatangazwa karibuni kabla ya upigaji kura kuanza

No comments:

Post a Comment