NJEMBA moja iliyojulikana kwa jina la Haji Bakari maarufu kama Mchome
limekamatwa baada ya kudaiwa kutapeli kiasi cha shilingi 570,000 kwa
njia ya simu za mkononi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, njemba
hilo lilifanikisha utapeli huo kwa kutumia majina ya watu wanaofahamiana
na washirika kibiashara.
Kijana huyo aliomba pesa hizo kwa madai
kuwa gari lake limemharibikia maeneo ya Chalinze mkoani Pwani hivyo
alihitaji kiasi hicho ili aweze kulitengeneza. Bila hiyana, aliyeombwa
alitoa fedha hizo kwa moyo mmoja ingawa kwa awamu mbili.
Akizungumza na gazeti hili, mtu aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la Godilizen Moshi alisema baada ya kumkamata mtu huyo, alijihami na kusema kuwa aliyefanya mchezo huo ni pacha wake.
Akizungumza na gazeti hili, mtu aliyetapeliwa aliyejitambulisha kwa jina la Godilizen Moshi alisema baada ya kumkamata mtu huyo, alijihami na kusema kuwa aliyefanya mchezo huo ni pacha wake.
Akisimulia mkasa huo,
Moshi alidai: “Kijana huyu ni mzoefu na alikuwa akitumia simu nambari
0655 301646, nilimuamini baada ya kunitajia jina la mtu ambaye
nafahamiana na tunashirikiana kibiashara.”
Alisema baada ya
kukamilisha kumpatia kiasi hicho cha fedha alizoomba alimpigia simu ili
kuhakiki kama amezipata lakini ilipopokelewa, mpokeaji alisema alikuwa
mazishini mkoani Kilimanjaro, kitu ambacho kilimshtua na kuhisi
kutapeliwa.
Baada ya hapo, Moshi aliwataarifu ndugu zake na mara moja msako mkali dhidi ya tapeli huyo ukaanza.
Baada ya hapo, Moshi aliwataarifu ndugu zake na mara moja msako mkali dhidi ya tapeli huyo ukaanza.
“Nilipagawa baada ya kujibiwa kuwa niliyemtumia fedha yuko Kilimanjaro, jibu hilo lilinichanganya sana,” alisema Moshi.
Kwa mujibu wa Moshi, alitafuta watu wa kumsaidia kumkamata mtu huyo na
hatua yao ya kwanza ilikuwa ni kwenda ofisi za mtandao wa Tigo zilizopo
Mlimani City jijini Dar ili kujua sehemu halisi alipo tapeli huyo.
Baada ya kueleza tatizo lao, mfanyakazi wa kampuni hiyo aliwaeleza kuwa
mtu mwenye namba hiyo anapatikana eneo la Ubungo Kibangu, jijini Dar es
Salaam.
“Na kweli tulipoenda Kibangu tukiwa na wenyeji wa huko tulifanikiwa kumpata kirahisi sana na kumchukua, kutokana na kibano alichopewa alisema sio yeye aliyetapeli bali ni pacha wake,” alisema.
“Na kweli tulipoenda Kibangu tukiwa na wenyeji wa huko tulifanikiwa kumpata kirahisi sana na kumchukua, kutokana na kibano alichopewa alisema sio yeye aliyetapeli bali ni pacha wake,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura
alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amekamatwa.
“Tunamchunguza kabla ya kumfikisha kortini,” alisema.
No comments:
Post a Comment