hk CONTACTS

hk CONTACTS

Tuesday, June 18, 2013

MECHI YA TAIFA STARS DHIDI YA IVORY COAST YAINGIZA 500 MILIONI



Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ya Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Taifa Stars na Ivory Coast 'The Elephants' iliyochezwa juzi Juni 16  katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.

Fedha hizo  ni mara mbili ya zile zilizopatika katika mchezo ulipita dhidi Morocco ambao ulingiza sh. 226,546,000.

Tiketi kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo zilizouzwa kwa sh 5,000, sh 7,000, sh 10,000, sh 15,000, sh 20,000 na sh 30,000.

Kwamjubu wa Ofisabari wa Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF', Boniface Wambura alisema kuwa mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
 
Katika hatua nyingine Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imevunja kambi yake jana  baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa juzi kwenye  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote waliokuwa kwenye timu taifa ya sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.

Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Taifa Stars itaianza safari yake ya michuano ya CHAN kwa kupambana na  Uganda  (The Cranes) jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu kabla ya kurudiana  wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala


No comments:

Post a Comment