Pages

Wednesday, October 5, 2016

CHURA WA SNURA AACHIWA HURU BAADA YA KUFANYIWA MAREKEBISHO

Msanii Wa Bongo Fleva Snura Mushi (Snura) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kufunguliwa kwa video ya nyimbo yake ya Chura iliyokuwa imefungiwa kwa miezi minne leo katika ukumbi wa Maisha Basement.
Waandishi wa habari wakiwa kazini

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemruhusu msanii wa muziki, Snura Anthony Mushi 'Snura' kuachia video yake mpya ya wimbo 'Chura' baada ya msanii huyo kufanya marekebisho ya maudhui ya wimbo huo na kukubaliwa na wizara.

Aidha, katika barua ya wizara imemtaka Snura kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari.

Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.
Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar es salaam, Snura amesema anamshukuru Mh waziri Nape Moses Nnauye kwa kumkubalia ombi lake la kuiruhusu kazi hiyo kutoka.

"Mh Nape ameuruhusu wimbo wangu mpya wa Chura na video Chura kupigwa na kuonyeshwa katika vituo mbali mbali vya radio na runinga baada ya kuona video yangu mpya ya wimbo ina maadili na ujumbe ndani yake ikiwa ni kukidhi makubaliano ya awali kwamba wimbo wangu 'Chura' utakafunguliwa pale nitakapofanya video mpya ya muziki yenye maadili ya kitanzania," alisema Snura.

Aliongeza, "Video yangu mpya Chura inaeleza maana halisi ya neno Chura. Chura ninae mzungumzia ni mwanamke anaeruka ruka katika mahusiano kwa kubadilisha wanaume mbalimbali matokeo yake kupata magonjwa sugu,".

Pia katika barua hiyo ya Mh Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempa onyo kali msanii huyo kutokurudia kufanya tena video zisiyokuwa na maadili ya kitanzania.

 

No comments:

Post a Comment