Pages

Friday, December 18, 2015

KIMENUKA: MIPANGO MIJI, MAAFISA ARDHI KINONDONI NA MAFISADI WA ARDHI KATA YA WAZO SASA ROHO ZAO ZIPO MIKONONI MWA WAZIRI LUKUVI ZOEZI LA DC MAKONDA LAIBUA MADUDU MAKUBWA...!


                   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi ambe kwa sasa ameshikilia roho za maafisa Ardhi, Mipango Miji na mafisadi Ardhi kata ya Wazo kwenye mtaa wa Nyakasangwe na Nakalekwa ambao wameshasababisha roho za watu wengi kupotea kwa uzembe huku wakidaiwa kutumia nguvu ya pesa kuwashika watu wa Mipango Miji na Ardhi Manispaa Kinondoni.
 Wakazi wa Nyakasangwe kata ya Wazo hivi ndivyo walivyompokea DC MAKONDA kwa mabango ya kuwakataa Maafisa Ardhi na Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DASA. kwa kukosa imani nao kwa madai ya kuwa wameshirikiana na mafisadi kuwaangamiza

  DC MAKONDA kama anavyoonekana amezungukwa na mabango ya kuwakataa watu wa mipango miji na Ardhi kwa kutuhumiwa kwa ufisadi.

 Na Mwandishi Wetu- Wazo
 Tangu kuteuliwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi, hali ya mafisadi wa ardhi nchini kote imekuwa mbaya kwani huenda muda wowote ni kikawaka kwa kuporwa ardhi hizo ambzo ni mashamba makubwa ambayo yalikuwa hayalipi kodi Serikalini hadi wananchi walipoyavamia na kujenga makazi.
Moja ya eneo linalotajwa sana kuwa kuna ufisadi mkubwa ni Wazo kwenye mitaa ya Nakasangwe na Nakalekwa ambapo tayari kulikuwa na jitihada za DC Makonda kutaka kumaliza mgogoro huo lakini nguvu yake ilikuwa ni ndogo kutokana na nguvu kubwa waliyokuwa nayo mafisadi hao ambao wanamtandao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar.
Hata hivyo kwenye zoezi linaloendelea sasa la kuhakiki viwanja hivyo kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa mafisadi hao ambao awari walizungumza uwongo kwa kusema wanaukubwa flani wa eneo lakini kwenye vipimo wanakuta tofauti hali ambayo inadaiwa huenda ikawaletea matatizo mafisadi hao kutokana kuidanganya Serikali na Mahakama.
Kutiokana na hali hiyo watu wengi nchini wana imani na Mh Lukuvu kushugurikia ufisadi huu na wale wote waliohusika na mgogoro huo kama ni maafisa ardhi na watu mipango miji basi wachukulie hatua.
Credit: Maskanibongotz 

No comments:

Post a Comment