Wasanii
wa kundi la Bongo Movie wakiongozwa na Maadam Wema Sepetu ambapo
wasanii hao wamefanyiwa umafia wa kutisha kiasi huku tsh milioni 52
zikitumika kuwaangamiza kabisa.
Wasanii Jack Wolper na Jb wakipeana mkono muda mfupi baada ya kumalizkia kuingia Demo ya Filamu ya Wake huku Jb akimpongeza msanii huyo kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya Wake Up ya msanii Manaiki Sanga ambapo filamu hiyo hadi sasa imevunja rekodi ya Afrika Mashariki na Kati kwa kupata oda zaidi ya milioni 30. Kampuni ya Stesp imekili kuwa kwa kiasi hicho ni kingi ambacho hakija wahi kufikiwa na msanii yeyote tangu histori ya filamu kuanza.
Msanii Manaiki Sanga The Don akiwa na aliyekuwa baunsa wa Diamond Mwarabu ambae kwa sasa amemuhodhi kwa ajiri ya kumlinda yeye.
Na Dorcus Shabani
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushta msanii Manaiki Sanga amewafanyia umafia wa kutisha wasanii Wema Sepetu na Jb kwa kuwashusha kiwanga kwenye mauzo ya filamu za kitanzania kufuatia filamu yake ya Wake Up hadi sasa kupata oda zaidi ya milini 30 nchi nzima huku bado nchi za kenya na uganda zikiwa bado hawajapelekewa.
Habari za uhakika toka kampuni ya Steps toka kwa mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo alisema" Mimi hapana taja jina langu kwani sio msemaji bwana lakini ukweli kwamba filamu ya Wake Up imevunja rekodi ya filamu zote zilizowahi kusambazwa na kampuni yetu kwa kuuzwa nakala nyingi zaidi ambapo hadi sasa tayari tumepokea oda ya zaidi ya nakala milioni 30 nchi nzima" Alisema Muhindi huyo ambae ilidiwa ni mdogo wake na bosi kubwa kubwa wa kampuni hiyo.
Hata hivyo muhidni huyo anasema kuwa Jumatatu ya tarehe 31. 08. 2015 ndiyo itakuwa mtaani lakini tayari watu toka Mikoani maajenti wapo Dar tayari kuchukua kopi zao huku nchi za kenya uganga, Kongo na Burundi zikipelekewa kopi zaidi ya laki nane.
Aidha filamu hiyo ambayo kesho Jumamosi wiki hii itaoneshwa live pale Jangwani kwenye screen kubwa zitakazokuwepo pembezoni mwa uwanja huo kwa lengo la maelfu ya watanzania kuona kabla ya Jumatatu kupata kopi halisi ya filamu iliyogharimu zaidi ya tsh milioni 52 huku ikiwashirikisha zaidi ya wasanii 30 mastaa wa bongo movie.
Aidha staa wa filamu hiyo Manaiki Sanga ameuambia mtandao huu wa maskanibongotz kuwa kuna zawadi ya tisheti zenye picha za filamu hiyo ya Wake Up na zitagawiwa bure pale Jangwani kesho lakini kama mtu anahitaji na angependa kupelekewa mahara alipo basi apige simu 0652-446446 hii na tisheti ni bureee kabisa.
Hata hivyo baada ya matokeo hayo msanii huyo amevunja rekodi ya wasanii wote waliowahi kutoa filamu zao ambazo ziliwahi kudiriki kufikia rekodi hiyo kwa mbali akiwemo Wema Sepetu na Jakob Steven Jb.
T shirt za bure piga simu hiyo juu kuipata hata kama mko familia wewe sema tu zitakuja hata hamsani
No comments:
Post a Comment