hk CONTACTS

hk CONTACTS

Thursday, January 23, 2014

KIGOGO WA BONGO FLAVA MATATANI KWA KUWADHURUMU WASANII HELA YA MH. LOWASA ALIYOITOA KWENYE TAMASHA LA BODABODA DAY..!











Na Mwandishi wetu
WAKATI kelele za wasanii wa fani zote nchini zikiendelea kusikika kuhusu wizi na dhuluma bila mkombozi thabiti kuonekana, wasanii waliopanda jukwaani kuimba siku ya tamasha la waendesha pikipiki jijini Dar es Salaam ambalo lilihitimishwa kwa hotuba ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, walipunjwa malipo waliyopewa.
Chanzo cha uhakika kilicho karibu na walioratibu, kusimamia na kushiriki maandalizi ya tamasha hilo, kinasema kigogo mmoja anayelalamikiwa sana na wana Bongo Fleva kuwa amekuwa akiwadhulumu na kukandamiza haki zao, alipewa tenda ya kuwatafuta, kuzungumza na hatimaye kuwalipa wasanii watakaoimba siku hiyo ya tukio lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam m.
Inadaiwa kuwa wakati wa majadiliano ya tenda hiyo, kigogo huyo alitoa bei kubwa kwa waratibu wa tamasha hilo, akidai wasanii wa siku hizi wameshtuka na wanataka fedha nyingi, jambo ambalo lilikubaliwa na watayarishaji hao, waliokuwa chini ya mtoto wa Mheshimiwa Lowassa aitwaye Fredy.
Inadaiwa kigogo huyo alitaja fedha ambazo kila msanii alistahili kupewa na zikatolewa (Fedha ya chini kabisa inasemekana ilikuwa shilingi milioni 1), kulingana na hadhi, ubora na kukubalika kwa wasanii hao kwa sasa.
“Baada ya tamasha kukamilika, msanii mmoja alilalamika kuhusu kiwango kidogo cha fedha alizopata, mmoja wa waamndaaji alipodadisi kiasi alichopewa, akamwambia laki mbili. Akamwambia ameibiwa, akamshauri aende kwa Fredy kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa akisimamia malipo ya wasanii, alipokwenda na kumweleza, Fredy alishangaa sana, akamuonyesha jinsi ambayo kila msanii alipaswa kulipwa,” kilisema chanzo hicho.
Inadaiwa baada ya msanii huyo kuonyeshwa malipo yaliyotolewa alishangaa sana na alipodai kupewa kilichobaki, aliambiwa aende kwa kigogo huyo, lakini kutokana na hofu iliyojengwa dhidi ya mtu huyo, msanii huyo alinywea na kumezea.
“Wasanii wanamuogopa sana jamaa (linatajwa jina la kigogo huyo), wengi walikwenda kulalamika, lakini wakaambiwa waende wakamweleze kisha wapeleke majibu kwa Fredy, lakini hakuna aliyekwenda,” kilisema chanzo hicho.
Xdeejayz  lilimvutia waya mlalamikiwa, ambaye anatajwa kuwa karibu na wadau wote wanaojihusisha na muziki Tanzania, kiasi cha kuonekana kama Mungu mtu miongoni mwa wanamuziki na wasanii.
Simu yake ya kiganjani iliita kwa muda wote bila kupokelewa hata baada ya kupigiwa zaidi ya mara moja. Kana kwamba haitoshi, gazeti hili lilituma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) likiomba kujibiwa kwa maswali hayo, lakini bado kigogo aliendelea kuuchuna. Hata hivyo, juhudi za kuwatafuta wadau zaidi wa sakata hili zinaendelea.
"GAZETI LA MASKANI BONGO LIKO MTAANI KILA JUMATANO DAKA KOPI YAKO"

No comments:

Post a Comment