hk CONTACTS

hk CONTACTS

Thursday, January 23, 2014

Hii ni kauli ya Nay wa mitego baada ya mshindi wa BSS 2013 kuonyesha mali alizonunua


.
.
Jana jioni kupitia millardayo.com mshindi wa shindano la vipaji la BSS 2013 Emmanuel Msuya aliziachia picha za nyumba aliyonunua, gari pamoja na studio… vyote akiwa kavifanya kutokana na zile milioni 50 za ushindi wa BSS.
Yafuatayo ni maoni ya Nay wa Mitego ambae aliwahi kudiss kwenye wimbo wake kwamba washindi wa BSS pesa za ushindi wanapewa, mbona hakionekani chochote?
Ya moyoni kutoka kwa Ney ni haya >>> ‘kitu ambacho watu walikua hawajui ni kwamba hivyo vitu alivyokua akivifanya mimi ni mtu wa kwanza kunieleza, aliposhinda tu ile November 30 2013 alinipigia simu siku ya pili akajitambulisha kwa kusema ‘brother mimi ni Emmanuel Msuya mshindi wa BSS, nakukubalia sana’
Screen Shot 2014-01-22 at 5.15.57 PMKwenye sentensi ya pili Nay anasema Msuya alimwambia ‘kesho mi napewa mpunga wangu’ kweli alipopewa akaniambia bro nimepewa hela yangu na nimeshaingiza bank, alipokwenda Musoma akaniambia ana mpango wa kufungua studio na nikawa nampa ushauri kwenye mambo mbalimbali’
‘Nimefurahi kusikia hivyo na ni moja kati ya vitu ambavyo huwa naviimba, hii ni nzuri zaidi… hiki ndicho kinachotakiwa kufanywa’ -Nay
.
.

No comments:

Post a Comment