Pages

Thursday, November 7, 2013

JACKLINE WOLPER ARUDI KATIKA DINI YAKE YA AWALI NA KWENDA KANISANI BAADA YA KUMWAGANA NA DALLAS.

                            

Jackline Wolper Actress maarufu Swahiliwood Jackline Wolper ameamua kurudi katika dini yake ya kikiristo baada ya mwaka jana kubadili dini na kuwa muislamu kufuatia kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mfanyabiashara Abdallah Mtoro(Dallas) na kuahidiana kuoana lakini kabla ndoa haijatokea penzi la wawili hao liliota mbawa. Wolper baada ya kubadili dini na kuwa muislamu mwaka jana alikuwa anaitwa jina la Ilham lakini Jumapili iliyopita actress huyo mwenye mvuto alienda katika kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama na kusali na waumini wenzake huku akiimba nyimbo za dini hiyo kwa hisia kali na baada ya hapo kuteta mawili matatu na waumini wenzake. Alipoulizwa na Globalpublishers sababu za yeye kurudia katika dini yake ya awali Wolper alisema "Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite Jacqueline kama zamani"

No comments:

Post a Comment