Pages

Wednesday, August 14, 2013

MASTAA WATANO (5) WANAOCHUKIWA SANA KIPINDI HIKI


1)MWANA-FA
Sababu za kuchukiwa:-


a)MSALITI/KIBARAKA
   Baada ya vuguvugu la kutaka wasanii kujikomboa kutoka katika mfumo wa kinyonyaji waliamua kwa pamoja (na yeye akiwemo) kuunda chombo cha kuwatetea kilichoitwa TUMA lakini mwisho wa siku aliwageuka na kwa kushirikiana na wale ambao wasanii wanawataja kuwa ni miongoni mwa mfumo wa kinyonyaji wakatengeneza chombo kingine 
kilichoitwa TFU kwa ajili ya kupambana na harakati zozote zitakazofanywa na TUMA.  

b)KUACHUKUA UBALOZI WA FISTULA
     Kitendo cha MwanaFA kuchukua ubalozi wa FISTULA kimetafsiriwa kama ni kutumiwa na watu wanaopambana na JIDE kwa sababu kabla ndiye alikuwa balozi wa ugonjwa huwa na alijitolea kwa hali zote,kitendo hicho kilifanya wadau mbalimbali kumshambulia kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya mtandao.

c)KUANDAA SHOW SIKU MOJA NA JIDE
      Kitendo cha kuandaa show siku moja na siku ambayo JIDE anafanya uzinduzi wa albamu yake NOTHING BUT THE TRUTH kinatafsiriwa kama ni kutaka kumuharibia JIDE kimechangia sana chuki dhidi yake kutoka kwa mashabiki wake.

2)CHID BENZ

UGOMVI
a)Kitendo cha kumpiga rafiki yake wa karibu sana MANGWEA na kuendelea kushambuliana kwenye mitandao ya kijamii
b)Kitendo cha kuvamia show ya akina KALA PINA hali iliyopelekea kutokea kwa vurugu zilizopelekea yeye kupigwa na kiongozi wa kikosi cha mizinga Kalama Masoud 'KALA PINA'.
kumfanyia fujo msanii wa tiptop conection tundaman newmaisha club, Pia kiliwakasirisha watu mashabiki wake wengi na kumjengea chuki dhidi yake.

3)MATONYA/ TID

     Hawa wameingia hapa kwa kosa moja tu linalofanana nalo ni kuitosa show ya Lady jaydee ili hali wakiwa tayari wamechukua malipo ya awali kwa ajili ya show hiyo na mashabiki wakaamua kuwajengea chuki kwa kutafsiri kitendo hicho kuwa si cha kiungwana kumfanyia dada huyo.

4)MRISHO NGASA

    Kauli aliyoitoa baada ya kuondoka klabu ya SIMBA 'Nimeisaidia Simba kushika nafasi ya tatu' ni kauli aliyotafsiriwa na mashabiki wa SIMBA kama kejeli kwao.Wanadai kuwa alikuwa anahujumu timu ndo maana timu imekosa nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa

5)NEY WA MITEGO

    Sababu kuu wanadai kuwa hawezi kufanya wimbo bila kudis wasanii wenzie hilo ndio limetajwa kuwa ni tatizo lake kubwa kwamba akirekebisha hapo anaweza akasamehewa.

NB-haya ni maoni kutoka kwa wadau mbalimbali na vyanzo mbalimbali kutoka katika mitandao ya kijamii 'DONT TAKE IT TOO PERSONAL'
Ni mawazo yao si yangu msijenge chuki ni mtazamo tu hata afande sele na solothang walishawahi kuimba.....nimemalizaaaaaa.

No comments:

Post a Comment