Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’. Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya ‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Source:Jamii forums
No comments:
Post a Comment