Pages

Monday, June 10, 2013

TUZO ZA KILI 2013: NDIVYO SIVYO HIVI NI BAADHI YA VITU VILIVYOSHANGAZA WATU. SOMA HAPA


Na Waandishi Wetu
ZILE Tuzo za Muziki za Kili 2013 zilizolenga kuwapongeza wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012, zimeteka hisia za wengi kwa kuwa vitu vingi vilikwenda ndivyo sivyo tofauti na zilivyotarajiwa, Ijumaa Wikienda lina fulu stori.

Kala Jeremiah akiwashukuru mashabiki.
Kabla ya kukudondoshea listi ya wasanii waliong’ara kwenye tuzo hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar usiku wa kuamkia jana, kuna matukio kibao yaliyojiri kama ulivyo ulimwengu wa mastaa.

VITUKO ZULIA JEKUNDU
Baadhi ya wasanii waliojitokeza kwenye zulia jekundu ‘red carpet’ walionekana kuwa washamba kwa kushindwa kuweka pozi kwa ajili ya picha.
Wapo baadhi ambao walijikuta wakijikwaa kutokana na mavazi hasa viatu ambavyo viliwafanya washindwe kutembea.

Ommy Dimpoz akiwa na tuzo yake.
KILA MTU NA WAKE
Ishu nyingine iliyozua gumzo ni kitendo cha baadhi ya wasanii kutinga na wapenzi wao kwa mara ya kwanza.
Baadhi yao ni Ali Kiba, Barnaba, Amini na wengine kibao waliokuwa ‘klozi’ na watoto wazuri.

OMMY AMWITA WEMA SHEMEJI, AZUA MASWALI
Katika hali ya kushangaza, swahiba wa Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz aliibua mzozo baada ya kushukuru kukabidhiwa tuzo na Wema Sepetu kisha akamwita shemeji, akazua swali kwamba mnyange huyo ni shemeji yake kwa nani?
Prezidaa wa Mashujaa Band, Chalz Baba akiwa na moja ya tuzo za kundi lake.
KALA JEREMIAH ASHUKURU HADI AKABOA
Jambo lingine lililozua maswali ni pale Kala Jeremiah aliposhinda tuzo ya tatu na kushukuru hadi akaboa watu na kusababisha kuzimiwa kipaza sauti.

AMINI NA LINAH MH!
Wasanii wawili kutoka THT ambao waliwahi kuwa wapenzi na kumwagana, waliwaacha watu midomo wazi kwa mara nyingine baada ya kugandana kama ruba hasa baada ya kutwaa tuzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kushoto) akimkabidhi tuzo, prodyuza Amoroso.
CHAZ BABA, WEMA LAIVU
Muda mfupi baada ya Chaz Baba kutwaa tuzo tatu, alinaswa laivu akiteta jambo kwa kina na Wema Sepetu, jambo lililosababisha kuhisiwa kuwa huenda kuna chochote kinachoweza kujirudia kwani walishakuwa wapenzi zamani.

ACHAPIA JINA LA NAY WA MITEGO
Kituko kingine ni pale mwakilishi wa Nay wa Mitego kwenye kupokea tuzo alipochapia jina la Mitego na kusema Mitogo.

Amin akiwa na tuzo yake. Pembeni yake ni Linah.
JACK PATRICK AMWAGA MINOTI
Mrembo huyo asiyeishiwa vituko, Jack Patrick aligeuka pedeshee baada ya kuwamwagia minoti wasanii waliokuwa wanapafomu.

KWA NINI NDIVYO SIVYO?
Kwa mujibu wa wahudhuriaji wa tukio hilo, wengi walioshinda tuzo nyingi hawakutarajiwa hivyo kuacha watu midomo wazi.
Kwa mfano, kitendo cha tuzo nyingi kuchukuliwa na wasanii wa THT, mwanzoni kilishangaza wengi lakini kadiri muda ulivyosonga mambo yakabadilika.

Rappa Ferguson akionyesha kwa mbwembwe tuzo yake kwa mashabiki.
TUZO TATU ZA CHAZ BABA, KALA
Kwa upande wa Kala, alianzia katika Ukumbi wa Dar Live hivi karibuni alipotwaa tuzo ya Mwana-Hip Hop Bora wa Mwaka hivyo tuzo tatu za Kili alizotwaa ulikuwa ni mwendelezo tu, tofauti na wengi walivyotarajia kufuatia aina ya wasanii aliokuwa akishindanishwa nao kama Fid Q.
Kwa upande wake, Chaz Baba wa Mashujaa alisababisha mshtuko baada ya kutwaa tatu na rapa wa bendi hiyo, Fagason moja.
Mshtuko zaidi ulikuwa kwenye bendi yao ya Mashujaa iliyonyakua tuzo mbili na kuwashangaza wengi kwani haikutegemewa kutokana na bendi iliyokuwa ikishindanishwa nazo, kama African Stars ‘Twanga Pepeta’ na nyinginezo.
Sehemu ya umati uliohudhuria hafla hiyo.
Mwingine aliyeshtua watu ni Ommy Dimpoz ambaye hata hivyo wengi walitarajia afanye ‘wandaz’ na kweli ikatokea hivyo.
Tofauti na mwaka jana ambapo Diamond ndiye aliyetwaa tuzo nyingi, mwaka huu aliambulia mbili tu pamoja na kwamba alikuwa msanii pekee aliyefanya vizuri kupita maelezo kwa mwaka huo.

NGWEA AENZIWA
Wasanii kadhaa waliokuwa wakipanda jukwaani, walimuenzi msanii Albert Mangwea aliyefariki  dunia hivi karibuni na wengi kumuombea pumziko la amani huko aliko.
Linah akitoa burudani.
TUZO ZENYEWE
Kikundi Bora cha Taarab, Jahazi Modern Taarab kiliibuka kidedea, Mtunzi Bora wa Mashairi Taarab alikuwa ni Thabit Abdul, Wimbo Bora wa Taarab ikaenda kwa Khadija Kopa na wimbo wake wa Mjini Chuo Kikuu huku Mtayarishaji Bora wa Mwaka, Taarab akiwa ni Enrico na studio yake ya Soundcrafters.
Msanii Bora wa Kike, Taarab alikuwa ni Isha Mashauzi na bendi yake ya Mashauzi Classic na Msanii Bora wa Kiume, Taarab ni Mzee Yusuf.
Wimbo Wenye Vionjo vya Asili ulioibuka kidedea ulitoka kwa Mrisho Mpoto, Chocheeni Kuni, Mtunzi Bora wa Mashairi, Bongo Fleva akawa Ben Pol, Mtayarishaji Bora wa Mwaka, Muziki wa Kizazi Kipya ni Man Water, Msanii Bora wa Kiume, Bongo Fleva ni Diamond Platnumz na Msanii Bora wa Kike, Bongo Fleva ni Recho wa THT.
Saida Karoli na kundi lake wakipagawisha stejini.
Wimbo Bora wa Bongo Pop ulitoka kwa Ommy Dimpoz akimshirikisha Vanessa Mdee na wimbo wake wa Me and You, Msanii Bora Anayechipukia alikuwa ni Ally Nipishe, Kikundi Bora cha Muziki wa Kizazi Kipya ni Jambo Squad na Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka ni Mensen Selekta.
Wimbo Bora wa Bendi ulikwenda kwa  Mashujaa (Risasi Kidole), Mtunzi Bora wa Mashairi, Bendi alikuwa Charles Baba ‘Chaz Baba’, na Mtayarishaji Bora wa Mwaka, Bendi alikuwa ni prodyuza Amorrosso aliyekabidhiwa tuzo na Eric Shigongo, Mkurugenzi wa Global Publishers.
Katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike, Bendi aliyeibuka mshindi ni Luiza Mbutu, Msanii bora wa kiume, Bendi akawa Chaz Baba na Rapa Bora wa Bendi alikuwa ni Fagason.
Katika ‘kategori’ ya Bendi Bora ya Mwaka, Mashujaa walilamba dume huku Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba ukiwa ni Ni Wewe wa Amini.
MC Zembwela akiwavunja mbavu mashabiki.

Kwa upande wa Wimbo Bora wa Reggae, Warriors From The East waliibuka kidedea kupitia wimbo wao wa Kilimanjaro huku Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall ushindi ukienda kwa Predator na wimbo wake wa Double.
Kwa upande wa kuchana, Msanii Bora wa Hip-Hop, tuzo ilikwenda kwa Kala Jeremiah, Mtunzi Bora wa Mashairi, Hip-Hop, pia Kala Jeremiah aliibuka kidedea, Wimbo Bora wa Hip-Hop ulikuwa Nasema Nao wa Nay wa Mitego huku Wimbo Bora wa R&B ukiwa ni Kuwa na Subira wa Rama Dee akiwashirikisha Mapacha.
Wimbo Bora wa Kushirikiana, tuzo ilikwenda kwa Ommy Dimpoz akiwa na Vanessa Mdee kupitia wimbo wake wa Me and You, Wimbo Bora wa Mwaka ulikuwa ni Dear God wa Kala Jeremiah huku Video Bora ya Wimbo wa Mwaka ikiwa ni ya Baadae ya Ommy Dimpoz.
Tuzo ya Hall of Fame kwa upande wa Bendi ilikwenda kwa The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ huku Hall of Fame kwa upande wa msanii ikienda kwa Salum Abdallah Yazidu.
Katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike, tuzo ilikwenda kwa Lady Jaydee.
SOURCE : GPL

No comments:

Post a Comment