Pages

Monday, May 13, 2013

MCHEZA FILAMU ZA NGONO SEHEMU YA 3.



  Siku ya leo haikuonekana kuwa nzuri kwa Gibson, alikuwa amefika nyumbani hapo huku akionekana kutokuwa na furaha kabisa, alikuwa katika hali ambayo ilikuwa ikimuonyeshea kuwa na unyonge wa hali ya juu. Prisca akaonekana kuishangaa hali ile, hakuwahi kumuona Gibson akirudi katika hali ya unyonge kama siku hiyo.
Prisca akawa na kiu ya kufahamu sababu iliyomfanya Gibson kuwa katika hali hiyo lakini wala Gibson hakuwa radhi kusema zaidi ya kusingizia kwamba hakuwa akijisikia vizuri kiafya, hakutaka kumwambia Prisca kwamba msichana Katie ambaye alikutana nae ofisini ndiye ambaye alikuwa amemsababishia hali ile.
Kichwa cha Gibson kikatawaliwa na jina la Katie, msichana yule, kwake alionekana kuwa msichana mrembo lakini hakuona kama alikuwa na urembo ambao ungemfanya kumsaliti mpenzi wake, Prisca. Bado alikuwa akimpenda Prisca, bado alikuwa akiona kuwa na uhitaji wa kuendelea kuwa mwaminifu kwa Prisca.
“Kichwa kinauma. Na ninadhani hata mafua yameanza kuuma pia” Gibson alidanganya.
“Pole mpenzi wangu. Ila naona ungekunywa dawa”
“Nimekwishakunywa ofisini. Nilikuwa sijisikii vizuri kwa kipindi kirefu sana” Gibson alimwambia Prisca.
Tayari Katie akaonekana kuanza kuharibu kila kitu moyoni mwake, alijitahidi sana kutokumfikiria lakini jambo hilo likaonekana kuwa gumu moyoni mwake. Kipindi cha nyuma hasa alipokuwa shuleni kabla hajampata Prisca alikuwa akitamani sana kuwa na msichana wa kizungu huku lengo lake kubwa likiwa kama tiketi ya urahisi ya kumfanya kuingia katika nchi za Ulaya au Marekani.
Kile kitu ambacho alikuwa akikifikiria, leo kilikuwa kimefika ila kilikuwa kimefika katika wakati mbaya sana. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kufanya, Katie kwake nae alionyesha kuwa na mapenzi ya kweli huku akiwa hajui kabisa kwamba msichana yule alikuwa muigizaji bora wa filamu za ngono duniani.
“Siwezi kumsaliti Prisca” Gibson alijisemea.
Kesho asubuhi ilipofika, asubuhi na mapema kama kawaida yake akaanza kwenda ofisini. Bado akili yake ilikuwa ikimfikiria Katie ambaye alimuona kuwa na asilimia kubwa ya kuharibu mapenzi yake na Prisca. Gibson hakutaka kuficha, alichokifanya ni kumuita rafiki yake, Richard na kuanza kumpa taarifa.
“Da! Una zali ile kinoma” Richard alimwambia Gibson.
“Nina zali?”
“Sasa unataka niliite nini hilo? Demu wa kizungu mtu wangu, yaani hapo uhakika wa kupata viza nje nje bila usumbufu” Richard alimwambia Gibson.
“Kwa hiyo unataka nifanyeje?”
“Swali la kitoto hilo wewe. Mchukue tu. Lala nae. Yeye si ndio anavyotaka. Kula mshiko wewe” Richard alimwambia Gibson.
“Ushauri wako unaonekana kutokuniingia”
“Tatizo lako moja. Yaani unataka mpaka Mungu akutokee usiku akwambie kwamba hiyo ni nafasi yako ya kwenda Marekani na kuutoka umasikini. Acha hizo Gibson. Wakati mwingine baraka za Mungu zinakuja kimafumbo. Kama ukiiacha hii, haiji mara mbili” Richard alimwambia Gibson.
“Lakini si unajua ninaishi na mpenzi wangu, Prisca ambaye ni mjauzito?”
“Ndio. Ila ukiwa na huyu mzungu, Prisca atajua? Sikiliza Gibson, ngoja nikueleze kitu kimoja. Wasichana wa Kibongo si wa kuwawekea dhamana. Unaweza ukagoma kumchukua huyo mzungu kwa ajili yake, halafu huyo huyo Prisca baadae anakuja kutembea na mshikaji mwingine. Hii ndio nafasi. Wazungu wanasema ‘Nafasi ya dhahabu haiji mara mbili’. Yaani hata misemo ya wahenga umeisahau. Kama hautaki, basi acha ila baadae usije ukajuta tu” Richard alimwambia Gibson.
Maongezi yao yalikuwa yakiendelea zaidi na zaidi, muda wote Richard alikuwa akimwambia Gibson kuanza uhusiano na Katie. Ingawa maneno yale yalikuwa hayamuingii kabisa akilini, lakini kadri Richard alivyokuwa akimwambia na ndivyo ambavyo yakaanza kumingia akilini.
“Mmmh! Lakini inawezekana bwana kwamba Mungu ameamua kunipa baraka kimafumbo. Ngoja nami niitumie nafasi hii” Gibson alisema katika kipindi ambacho alikuwa akiitwa kwenda kuwachukua wazungu wale kuwaingiza ndani ya mbuga huku Katie akiachiwa nafasi ya mbele kabisa kukaa na dereva, Gibson.
****
Muda mwingi Gibson alikuwa akiyaangalia mapaja ya Katie ambaye alikuwa amekaa pembeni yake ndani ya gari lile. Kwa wakati huo, akili yake haikuwa mahali hapo tena, ilikuwa ikifikiria ngono tu. Tayari akajiona akianza kuvutwa katika himaya ya msichana yule ambaye alikuwa mcheza filamu za ngono mkubwa ambaye alikuwa akijulikana sana na watazamaji wa filamu zile.
Katie alijifanya kutulia huku akimuangalia Gibson kwa macho ya wizi, tayari akajiona kufanikiwa juu ya lile lengo lake ambalo alikuwa amejiwekea la kumteka kimapenzi Gibson. Katie akashindwa kujizuia, akaanza kumgusa gusa Gibson begani mwake, yaani wakati wote alikuwa akimgusagusa tu.
Walipofika mbugani, wote wakaanza kupitishwa huku na kule huku wakiangalia wanyama mbalimbali. Kwa wakati huo kichwa cha Gibson kilikuwa kikifikiria fedha, tayari akaonekana kugundua kuwa kama angekubali kuwa na Katie, kwa kiasi fulani angekuwa akipata fedha kutoka kwa msichana huyo.
Japokuwa Katie alikuwa akipenda wanyama na wazo la kwenda mbugani lilikuwa lake lakini kwa wakati huo hakuwa na habari na wanyama, kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuwa pamoja na Gibson tu.
“Will you be ready? (Utakuwa tayari?)” Katie aliuliza.
“For what? (Kwa lipi?)”
“I need you tonight in my bedroom (Ninakuhitaji usiku wa leo chumbani kwangu)” Katie alimwambia Gibson.
Mawazo ya Gibson yakahama kwa wakati huo, akaanza kumkumbuka Prisca wake ambaye alikuwa amemuacha nyumbani akiwa mjauzito. Maneno yale ambayo aliyaongea Katie yalikuwa na maana kwamba kama alikuwa tayari kumsaliti Prisca usiku wa siku ile. Kichwa chake hakikuweza kutulia, alimpenda sana Prisca na alimpa ahadi nyingi huku miongoni mwa ahadi hiyo ikiwa ni ya kutokumsaliti katika maisha yake yote.
“Haiwezekani” Gibson alijisemea moyoni.
Huku akiwa amelifikiria jibu hilo, mara kumbukumbu ya rafiki yake Richard ikaanza kujirudia kichwani mwake. Maneno mengi ya Richard ambayo yalikuwa yakimtaka kutokuacha kumkubali Katie yalikuwa yakijirudia kichwani mwake.
Maneno yale bado yalikuwa yakijirudia kwamba ile ilikuwa ni bahati ambayo Gibson alikuwa ameipata na kamwe asikubali kuipoteza kwani kama angeipoteza kamwe isingeweza kurudi tena mikononi mwake.
Tayari hapo akatengeneza jibu la kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya na ambacho kilionekana kuwa uamuzi sahihi kutoka moyoni mwake. Hakukuwa na kingine alichokifikiria zaidi ya kukubali kile ambacho kilikuwa kikitakiwa kufanyika na Katie.
“Kwani Prisca atajua? Hawezi jua bwana. Kwanza kufanya mapenzi na mwanamke wa kizungu bahati kwa sisi wenye ngozi nyeusi tuishio Afrika” Gibson alijisemea.
Akayarudisha macho yake usoni mwa Katie na kisha kuachia tabasamu pana ambalo lilionyesha kukubaliana na kile kitu ambacho alikuwa amezungumza Katie. Matembezi ndani ya mbuga ile yaliendelea zaidi na zaidi mpaka ilipofika saa kumi na mbili, muda ambao walitakiwa kurudi hotelini.
Kitu cha kwanza alichokifanya Gibson mara baada ya kufika hotelini ni kuanza kumtafuta Richard na kisha kumwambia uamuzi ambao alikuwa ameupanga na ambao aliuona kufaa kwa kipindi hicho.
“Kama umekubali hapo sawa. Wanawake kama hao ambao wanakuja kuja wewe chukua tu” Richard alimwambia Gibson.
“Ila kitu hii nataka kibaki siri kati yangu na wewe”
“Usijali. Yule mjauzito hatojua” Richard alimwambia Gibson.
“Baadae ndio naenda chumbani kwake”
“Safi sana. Ila kuna kitu nataka ukifanye”
“Kitu gani?”
“Mkamue hasa ukifika nae kitandani. Yaani mkamue hadi aite mama” Richard alimwambia Gibson.
“Du!”
“Usishangae wala kushtuka. Kama ukimkamua haswa, hata akifika Ulaya atakukumbuka na atakuwa akitamani kukutana nawe kimapenzi zaidi. Ila ukipiga rasharasha, hatorudi tena” Richard alimwambia Gibson ambaye akaonekana kuyakariri maneno yote.
Ilipofika saa tatu usiku, akashtuliwa simu na kwamba alikuwa akihitajika chumba namba ishirini na mbili. Kitendo cha kuitwa tu, tayari hamu ya kufanya mapenzi ikamshika, akaanza kupiga hatua za haraka haraka kuelekea katika mlango wa kuingilia chumba kile, alipoufikia, akapiga hodi na kuingia ndani.
Katie alikuwa amejilaza kitandani huku akiwa na nguo ya ndani tu. Mapigo ya moyo ya Gibson yakaanza kudunda, alipokikodolea vizuri kifua, kilikuwa kile ambacho alikuwa akikipenda sana na si kama cha Prisca ambacho kilikuwa kikiendelea kujaa tayari kwa kunyonyesha.
Akaanza kusogeza pale kitandani. Akapokelewa kwa mikono miwili na kuanza kuvuliwa nguo. Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa Gibson kumsaliti Prisca. Kadri alivyokuwa akiucheza mchezo ule na ndivyo ambavyo kichwa chake kilivyozidi kumkumbuka Prisca.
Walichukua masaa matano, wakawa wamekwishamaliza, wakaenda bafuni kuoga na kisha Gibson kuondoka chumbani mule huku mfukoni mwake akiwa amewekewa kiasi cha zaidi ya dola za Kimarekani elfu mbili mfukoni mwake bila kujijua.
Ilikuwa ni saa tisa usiku katika kipindi ambacho Gibson alikuwa akirudi nyumbani kwake kwa kutumia bajaji ambayo ilimpeleka salama. Alipofika nyumbani, akagonga hodi, mfanyakazi wa ndani, Hilda akaja na kuufungua mlango.
Prisca bado hakuwa amelala, muda wote huo alikuwa macho akimsubiria mpenzi wake. Usingizi kwake wala haukupatikana kabisa, mawazo kibao yalikuwa yamemsonga kichwani mwake. Moyo wake haukujisikia amani kabisa, alikuwa akimkumbuka mpenzi wake kupita kawaida.
Katika kipindi ambacho Gibson aliingia chumbani mule, akakaribishwa na kumbatio la nguvu na mabusu mengi mashavuni mwake. Kwa jinsi alivyoonekana kuwa na furaha, Prisca akashindwa kuvumilia, akajikuta akitokwa na machozi.
“Nimerudi mpenzi. Usilie, niko salama” Gibson alimwambia Prisca huku moyo wake ukijihukumu kwa kile ambacho alikuwa amekifanya hotelini.
“Nakupenda mpenzi. Nilikuwa na wasiwasi mpenzi” Prisca alimwambia Gibson.
“Usijali. Niko salama. Nimekumisi pia” Gibson alimwambia Prisca huku nae akianza kumbusu.
“Mbona ulizima simu mpenzi?”
“Iliisha chaji. Niliiacha ofisini nikiichaji huku mimi nikiwa nimewapeleka wazungu mbugani. Ila wazungu wa leo walikuwa wanazingua sana. Yaani mpaka wakatuchelewesha” Gibson alimwambia Prisca.
“Pole na kazi mpenzi. Vumilia, hayo ndio maisha” 
“Usijali. Nitafanya kila liwezekanalo kwa ajili yako” Gibson alimwambia Prisca na kisha kumbusu.
Prisca akatoka nje ya chumba kile na kwenda kumuandalia mpenzi wake chakula. Muda wote ambao Gibson alikuwa akimwangalia Prisca, alikuwa akiendelea kujuta moyoni mwake. Alijuta kufanya mapenzi na Katie, alikosa amani kwa sababu alikuwa amemsaliti mpenzi wake.
“Sifanyi nae tena. Sitokubali kumsaliti mpenzi wangu kwa mara ya pili” Gibson alijisemea huku akionekana kujuta.
Akavua suruali yake. Huku akitaka kuitundika katika mbao ya kutundikia nguo, akajikuta akigusa kitu kama karatasi mfukoni mwake jambo lililomfanya kuuingiza mkono mfukoni mwake. Kiganja chake kikagusa karatasi kadhaa, alipozitoa zilikuwa dola.
Akazihesabu haraka haraka, zilikuwa ni dola elfu mbili ambazo zilikuwa zaidi ya milioni tatu. Uso wake ukaonyesha tabasamu, akaonekana kufurahi kupita kawaida. Akatamani kuruka ruka kwa furaka, akajikuta akijilaza kitandani.
“Haya ndio maisha bwana. Kwa staili hii, wala siwezi kumuacha, kesho nampa dozi zaidi” Gibson alisema huku akitabasamu.

Je nini kitaendelea?
Je nini kitatokea Gibson atakapoendelea zaidi kutembea na Katie?
Je Prisca atajua?
Na je Katie atajua kama Gibson ana mchumba mjauzito?
Itaendelea kesho saa nne usiku

IMEDHAMINIWA NA DICK SOUND,NA FACEBOOK TAKE AWAY wauzaji wa chips tamudar es salaam.

No comments:

Post a Comment