Pages

Sunday, May 12, 2013

MCHEZA FILAMU ZA NGONO SEHEMU YA 2.


 


Ndani ya ndege kila mtu alionekana kuwa na furaha, waigizaji walikuwa wakipiga stori huku safari ikiendelea. Hiyo ndio iikuwa safari ya kwanza kuja Afrika kwa kazi ya kuigiza. Kwao, safari hii ilionekana kuwa na baraka nyingi na walitumaini kuuza kazi hiyo zaidi ya kazi zote ambazo zilikuwa zimepita.
Katie alikuwa bize na kusoma jarida maalumu ambalo lilikuwa likielezea nchi ya Tanzania kuanzia uoto wa asili na mambo mengine mengi. Maeneo mengi yakaonekana kumvutia, tayari akilini mwake ikajengeka picha kwamba nchi ya Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi zilizokuwa na mazingira mazuri hasa kimisitu.
Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na waigizaji wote ambao walikuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kuigiza filamu hiyo ya ngono ambayo waliipa jina la MY NEIGHBOURHOOD CHICKS. Katika kipindi hicho walikuwa na kila kitu, kamera kubwa zilizokuwa na uwezo mkubwa, wapiga picha na waongozaji, wote walikuwa ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo wala haikupitia jijini Dar es Salaam. Kwa kuwa ilikuwa ni ndege yao wenyewe, ndege ya kampuni yao, ikapita moja kwa moja mpaka katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, Zanzibar.
Hali ya hewa kwao ikaonekana kuwa nafuu. Nchini Marekani, baridi lilikuwa likiwapiga kila siku, hawakuipenda hali ile ya hewa lakini walikubaliana nayo. Joto ambalo walikutana nalo nchini Tanzania likaonekana kuwafurahisha.
Kila kitu kilikuwa kimekwishapangwa. Mara baada ya kushuka kutoka ndani ya ndege, wakapanda kwenye magari maalumu ya hoteli ya Green Horse na kisha kuanza kwenda katika hoteli hiyo.
Njiani, kla mmoja alikuwa akiangalia nje, majengo ya kizamani ambayo yalikuwa yametumiwa enzi za ukoloni yakaonekana kuwa na mvuto machoni mwao. Kila wakati walikuwa wakitabasamu, hawakuamini kama kulikuwa na majengo mazuri kama yake.
Gari lile likafika katika hoteli ya Grean House ambayo ilikuwa pembezoni mwa bahari ya Hindi na kisha kuingia ndani. Muonekano wa hoteli ile ulikuwa sawasawa na hoteli ambazo zilikuwa zimejengwa nchini Marekani. Upepo mwanana wa bahari ambao ulikuwa ukiwapiga ukaonekana kuwafurahisha.
Wakachukua vyumba ndani ya hoteli hiyo, kwa kuwa walikuwa na fedha za kutosha, kila mmoja akakabidhiwa chumba chake ila kwa wale ambao walitaka kulala wawili wawili walikuwa wakiruhusiwa.
Katie akatulia kitandani kwake, akachukua kitabu cha Atlas ambacho kilikuwa mezani na kisha kuanza kukifungua na kuangalia mambo mbalimbali kuhusiana na nchi ya Tanzania. Hapo ndipo alipogundua kwamba pale walipokuwa walikuwa katika moja ya kisiwa cha Unguja.
Moyoni mwake, Katie akaanza kuvutiwa, akatamani kuziona zile mbuga za wanyama ambazo zilikuwa zikionekana katika ramani ya nchi ya Tanzania. Alichokifanywa kwa wakati huo ni kuifuata kompyuta ya mezani na kisha kufungua Internet na website ya Google na kisha kuandika ‘Mikumi National Park’
Picha za mbuga hiyo zikatokea, Katie akabaki akitabasamu tu. Hamu ya kutamani kuelekea katika mbuga ile ikaonekana kumkamata kupita kawaida. Katie hakuishia hapo, bado aliendelea kuangalia zaidi na zaidi, akaandika Kilimanjaro.
Mlima mkubwa wa Kilimajaro ukatokea katika kioo cha kompyuta ile. Akaanza kuuangalia mlima ule ambao juu ulikuwa na barafu jingi. Katie akaachia tabasamu pana zaidi, alichokuwa akikitaka ni kuchukua picha za mlima ule. 
Akaenda kitandani na kisha kufungua begi lake na kutoa kompyuta yake ya mapajani na kisha kuiunganisha na Internet isiyotumia waya iliyokuwa katika hoteli ile. Akafungua website ya Google na kisha kuandika Kilimanjaro. Ulipotokea mlima Kilimanjaro, akaanza kuzichukua zile picha na kisha kuziweka katika kompyuta yake.
Baada ya siku mbili kupita, filamu hiyo ambayo walipanga kuuigiza ikaanza. Kwao ikaonekana kuwa filamu nzuri, kila miuigizaji ambaye alikuwa amepangwa kuigiza katika filamu hiyo alikuwa akiigiza kwa umakini mkubwa na kujitolea hasa.
Kwa sababu Katie ndiye alikuwa muigizaji mkuu, aliigiza kwa ustadi mkubwa kiasi ambacho hata muongozaji akashangaa. Filamu hiyo wala haikuwa ndefu sana, walichukua kipindi cha mwezi mmoja ikawa imekamilika.
Ni matukio ya ngono ndio ambayo yalikuwa yametawala ndani ya filamu hiyo ambayo ingeonekana kuwavutia wale wote ambao walikuwa wakipenda kuangalia filamu za aina hiyo duniani.
Baada ya kumaliza kuigiza filamu hiyo, Katie akatoa wazo ambalo lilionekana kumvutia kila mtu. Alichoona yeye ilikuwa ni vizuri kwa wao wote kuelekea katika mbuga yoyote ile ya wanyama kwa lengo kubwa la kuona wanyama.
Kila mmoja akaonekana kuridhika na wazo lile, lilionekana kuwa wazo zuri ambalo liliungwa mkono na kila mtu. Siku iliyofuata, safari ya kuelekea Morogoro ikaanza huku wakitaka kuingia katika mbuga ya wanyama ya Mikumi na kuangalia wanyama.
Kwa kuwa walikuwa wametumia ndege, walichukua dakika arobaini na tano wakawa wamekwishafika Morogoro ambapo wakakutana na magari ya mbuga hiyo na moja kwa moja kuanza kupelekwa katika mbuga hiyo iliyokuwa na wanyama wengi na wa aina mbalimbali.
Walipofika mbugani, wakapelekwa katika hoteli ya MIKUMI NATIONAL PARK na kisha kuchukua vyumba katika hoteli hiyo. Siku iliyofuata, wakachukuliwa na magari ya mbugani na kisha kuanza kupelekwa sehemu mbalimbali katika mbuga hiyo.
Muda mwingi Katie alikuwa kimya ndani ya gari lile, macho yake yalikuwa yakimwangalia dereva ambaye alikuwa akiliendesha gari lile, Gibson. Gibson kwake alionekana kuwa kijana wa tofauti, umbo lake kubwa lilimvutia Katie.
Kwake, Gibson alionekana kuwa kijana mwenye mvuto, fulana yake aliyokuwa ameivaa ambayo ilimbana sana mwili ilimfanya mwili wake uliojazia kuonekana vizuri kabisa. Muda mwingi Katie alikuwa akiendelea kuutumia muda wake kumwangalia Gibson ambaye alikuwa bize akiwatembeza huku vijana wengine wawili wakitumia muda huo kuwaelekeza wazungu wale sehemu mbalimbali na kuwaonyeshea wanyama mbalimbali.
Akili ya katie haikuwa sawa katika wakati huo, mvuto ambao alikuwa nao Gibson ukaonekana kuusumbua moyo wake. Ni kweli kwamba alikuwa amewaona wanaume wengi na kufanya mapenzi na wanaume wengi pia lakini kwa Gibson hali ikaonekana kuwa tofauti sana.
Kwake, mwanaume huyo alikuwa na mvuto mkubwa, kifua kipana kilionekana kumchanganya kupita kawaida. Ingawa waigizaji wengine walikuwa bize kuwasikiliza vijana ambao walikuwa wakiwaelekeza mambo mengi lakini kwa Katie muda wote macho yake yalikuwa yakimwangalia Gibson.
Katie akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni kuanza kupiga hatua kumfuata Gibson, alipomfikia, akaamua kumsogelea karibu zaidi. Gibson hakuonekana kuwa na wasiwasi, kwake, wazungu walionekana kuwa watu wa kawaida sana kiasi ambacho ilimjia vigumu sana kumtambua msichana wa kizungu kama alikuwa ameangukia katika mapenzi.
“Hi” Katie alimsalimia Gibson huku tabasamu pana likiutawala uso wake.
“Hi” Gibson aliitikia.
Katie akaanza kujiumauma. Wakati mwingine alikuwa akijishikashika kiuno, mara akiikutanisha mikono yake na kujishika huku akijipindapinda, kwa wakati huo alikuwa akijitahidi kuleta mapozi mengi ya kizungu ili Gibson aweze kuelewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.
“Can I ask you something? (Naweza kukuuliza kitu?)” Katie alimuuliza.
“Yeah” Gibson alimwambia Katie.
Huo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yao. Katika kila hatua ambayo ilikuwa ikiendelea kati yao, Gibson alikuwa akichukulia kawaida tu japokuwa muda mwingi Katie alikuwa akionyesha dalili zote kwamba alikuwa akimhitaji Gibson kwa kipindi hicho.
Dakika ziiendelea kwenda mbele, Gibson akaja kugundua kwamba Katie alikuwa kwenye hisia kali hasa mara baada ya kufanya tukio ambalo lilionekana kumshtua, kushika maeneo ya zipu yake. 
Gibson alibaki akitetemeka, hakuamini kile ambacho Katie alikuwa amekifanya. Kwa mara ya kwanza alifikiri labda ilikuwa ni bahati mbaya lakini baada ya kuyapeleka macho yake usoni mwa Katie, msichana yule alikuwa akitabasamu tu.
“Mmh!” Gibson aliguna.
Kuanzia muda huo Katie hakutaka kuficha kitu chochote kile, akaanza kujionyesha dhahiri kwamba alikuwa ametekwa na mapenzi ya mwanaume huyo. Japokuwa Gibson alijitahidi sana kuzuga ili wazungu wengine wasiweze kuelewa kilichokuwa kinaendelea lakini hali ikaonekana kushindikana kabisa, kila mtu akafahamu.
Kwa sababu maisha yao yalikuwa ni ya kawaida, Katie hakutaka kujificha, akaamua kuwaambia wenzake kwamba kwa kipindi hicho moyo wake ulikuwa umetekwa kwa asilimia mia moja na Gibson. Gibson hakuongea kitu, muda wote alikuwa akijisikia aibu.
Muda wa kurudi hotelini ulipofika, wakaanza kurudi huku Katie akiwa kiti cha mbele kabisa. Katika kipindi hicho alikuwa akihakikisha kwamba anafanya kila liwezekanalo mpaka mwanaume huyo, Gibson anakuwa wake bila kujua kwamba Gibson alikuwa na mchumba aliyeitwa Prisca, ambaye alikuwa akimpenda kuliko mwanamke yeyote huku tumboni mwake akiwa na kiumbe alichosaidiana kutengeneza na Gibson, ujauzito.
****
Kijana Gibson alikuwa akijulikana sana katika mtaa wa Mwembechai sehemu ambayo alikuwa akiishi ndani ya jiji la Dar es Salaam. Maisha yake yalikuwa ni maisha ya kawaida sana, utafutaji wake ambao alikuwa akiufanya kila siku ndio ambao ulikuwa ukimuweka hapa mjini kila siku.
Gibson alimaliza Elimu ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mbezi High iliyokuwa maeneo ya Mbezi ile ya kuelekea Kibaha. Katika maisha yake ya shuleni ndani ya shule hiyo, Gibson akafanikiwa kupata marafiki wengi ambao walikuwa wakivutiwa nae kutokana na ucheshi mkubwa ambao alikuwa nao.
Wasichana nao hawakuwa nyuma, walikuwa wakimpenda sana Gibson kiasi ambacho kila msichana akatamani kuwa nae. Gibson hakutaka kujirahisisha kabisa, kwa kipindi hicho maisha yake yalikuwa yakifikiria elimu tu.
Hakujua ni wapi alipokosea mpaka msimamo wake wa kutokutaka kuwa na msichana kupotea, akajikuta akiangukia katika mapenzi ya msichana Prisca. Uhusiano wao wa kimapenzi ukaanzia hapo. Mara kwa mara walionekana kuwa pamoja, wanafunzi wakaufahamu uhusiano huo japokuwa wao wenyewe walijaribu kuuficha ukweli.
Miezi ikaendelea kukatika mpaka pale ambapo wakamaliza elimu ya kidato cha sita na kukaa nyumbani kwa ajili ya kusubiria matokeo. Kwao, kumaliza kule kulionekana kuwa na unafuu, wakaanza kujiachia vya kutosha, walikuwa wakifanya mapenzi mara kwa mara hasa katika kila kipindi ambacho msichana Prisca alipokuwa akienda kumtembelea Gibson.
Miezi ikakatika na matokeo kutoka, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa amefanya vizuri, wote walikuwa wamefeli mitihani yao. Wote wakaonekana kuumia, hawakuamini kile ambacho kilikuwa kimetokea lakini ikawabidi kukubaliana na ukweli kwamba walikuwa wamefeli mitihani yao.
Maisha ya mitaani yakaanza. Kwa kuwa kila siku alikuwa akishinda sana nyumbani, akaanza kuonekana kuwa mzigo kwa wazazi wake. Mzee Lyimo ambaye alikuwa baba yake, akaamua kumpa kiasi cha shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya kwenda kuanzisha biashara.
Gibson akazitumia fedha zile vilivyo, akaanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zikaanza kukua kila siku na kuanza kumuingizia fedha japokuwa hazikuwa nyingi sana. Bado uhusiano wake na Prisca ulikuwa ukiendelea kama kawaida.
Kila siku walikuwa wakitumia kinga. Mioyoni mwao hawakuwa na wasiwasi na magonjwa ya zinaa au UKIMWI bali walikuwa na wasiwasi na mimba tu. Ndani ya chumba cha Gibson, mipira ya kufanyia mapenzi ilikuwa mingi na alikuwa akiitumia katika siku ambazo Prisca alikuwa akija nyumbani hapo.
“Mmmh! Hili baridi” Gibson alimwambia Prisca huku manyunyu yakimwagika nje.
“Limefanya nini tena?” Prisca aliuliza.
“Linanipa hali fulani ya kuhitaji joto” Gibson alimwambia Prisca.
“Ngoja nikupe sweta” Prisca alimwambia Gibson huku akiachia tabasamu.
“Hapana. Hebu njoo karibu yangu” Gibson alimwambia Prisca ambaye akamsogelea pale kitandani na kisha kumkumbatia.
Hali ile ndio ambayo ikaonekana kuwa na unafuu kwa Gibson, kwa mbali akaanza kuhisi joto kutoka katika mwili wa Prisca. Gibson hakuona hali ile kutosha, akaamua kuipitisha mikono yake katika kiuno cha Prisca. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Gibson alivyozidi kuipeleka mikono yake zaidi na zaidi katika mwili wa Prisca, baada ya dakika chache, Prisca alikuwa mtupu.
Hilo ndilo lilikuwa lengo la Gibson, kilichofuata mahali hapo ni kuanza kumchezea Prisca. Aliendelea na mchezo ule mpaka pale alipoona ameridhika. Akaupeleka mkono wake katika boksi la mipira, hakukuwa na mpira hata mmoja.
“Da! Kumbe yote iliisha!” Gibson alijisemea moyoni.
Hakuwa na jinsi. Kwa hali ambayo alikuwa nayo mahali pale ilikuwa ni vigumu kuinuka na kuelekea duka la madawa kununua mipira, alichokifanya ni kufanya mapenzi na Prisca bila kutumia mpira wowote.
Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya mapenzi na Prisca bila kutumia mpira, hiyo ndio ilikuwa siku ambayo ikamsababishia Prisca kuanza kutapika na kujisikia kichefu chefu, siku hiyo ndio ambayo ilimfanya Gibson kujiandaa kuitwa baba.
Prisca akawa na ujauzito. Marafiki zake Gibson walikuwa wakimshauri mara kwa mara kwamba amwambie Prisca aende akautoe ujauzito ule lakini Gibson hakuonekana kukubali. Moyo wake ulikuwa ukimpenda sana mtoto wake ambaye alikuwa tumboni mwa mpenzi wake, Prisca.
Kutokana na kuwa bize na ujauzito wa Prisca, biashara zake zikaanza kuyumba. Faida aliyokuwa kipata alikuwa akiitumia kumtunza Prisca ambaye alionekana kuwa kwenye wakati mgumu. Kwa kuwa kipindi hicho alikuwa amepanga, hakutaka wazazi wake wafahamu kitu chochote kile.
Tayari Gibson alikwishaona kwamba mambo yalikuwa magumu. Kiasi cha fedha ambacho alikuwa amebaki nacho, akaamua kujifunza udereva. Alisoma kwa muda wa mwezi mmoja, alipoona amekuwa tayari, akaamua kwenda kusoma NIT ili aweze kuendesha magari ya viongozi mbalimbali wa Serikalini.
Gibson akawa dereva mzuri, masomo yake akawa amemaliza kwa kufanya vizuri mpaka pale ambapo alipewa cheti tayari kwa kuanza kazi pale ambapo angeipata. Kwa wakati huo, kiasi ambacho alikuwa amebaki nacho kilikuwa kidogo sana, akaamua kukibana hivyo hivyo mpaka pale kilipokwisha.
Kazi zikaonekana kuwa ngumu kupatikana. Aliangaika kwa muda wa miezi mitatu na ndipo alipoona kwenye gazeti kwamba kampuni ya Utalii ya Filbert Royal Tourism iliyokuwa Morogoro katika mbuga ya Mikumi ilikuwa ikitafuta madereva.
Gibson hakutaka kupuzia, japokuwa alikuwa amejaribu kuomba kazi sehemu nyingi na kukosa, hapo napo akaamua kujaribu. Baada ya wiki moja, akaitwa kwa ajili ya kufanyiwa usaili na alipoonekana kustahili, akaanza kazi.
Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake. Mshahara wake wa kwanza, akamsafirisha Prisca na kuishi nae mkoani Morogoro huku wazazi wa binti huyo wakiwa wameridhia kwa kila kitu. Ukaribu ambao alikuwa nao kwa mpenzi wake ulikuwa mkubwa, kila alipokuwa akitoka ofisini, moja kwa moja alikuwa akielekea nyumbani na kukaa na mpenzi wake, Prisca.
Maisha yaliendelea kila siku. Tumbo la Prisca kwa kipindi hiki lilikuwa kubwa. Alichokifanya Gibson ni kumuajiri mfanyakazi wa ndani kwa ajili ya kumwangalia mpenzi wake na kumfanyia kazi nyingine.
Simu ndio kilikuwa chombo ambacho alikuwa akipenda sana kukitumia kuwasiliana na Prisca kila alipokuwa mbali nae. Hakujisikia raha kama yalipita masaa mawili bila kuwasiliana na Prisca. Prisca, kwake alikuwa kila kitu, alimpenda kuliko msichana yeyote katika dunia hii.
Wasichana wa Morogoro wakaonekana kuvutiwa sana na Gibson ambapo mara kwa mara walikuwa wakimtaka kimapenzi. Gibson hakuonekana kukubaliana nao, hakuwa tayari kumsaliti Prisca kwa msichana yeyote yule, mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa Prisca yalikuwa ni makubwa sana.
“Ninakupenda sana mpenzi wangu” Gibson ailimwambia Prisca.
“Ninakupenda pia”
“Ulikumbuka kwenda hospitali leo?” Gibson alimuuliza.
“Ndio”
“Dokta amesemaje baada ya kukupima?”
“Otea”
“Wa kike” Gibson alimwambia Prisca.
“Hapana”
“Kwa hiyo ni wa kiume?”
“Ndio” Prisca alijibu na kutoa tabasamu kali.
“Asante Mungu. Nilikuwa na kiu ya kupata mtoto wa kwanza awe wa kiume. Mungu amejibu maombi yangu” Gibson alimwambia Prisca.
“Kwa nini haukuomba wa kike?”
“Ninataka kwanza niwe na mlinzi wa nyumba yangu. Wa pili akiwa wa kike, nitafurahi zaidi. Hata kama baadae watakua, huyu wa kike inabidi awe na heshima kwa kaka yake” Gibson alimwambia Prisca.
“Kwani akiwa wa kwanza wa kike hatokuwa na heshima?”
“Hilo jibu niachie moyoni mwangu. Si unajua nyumbani kwetu wa kwanza ni wa kike! Niachie tu jibu langu kwani naamini mwenyewe umeshaona sana ulipokuwa ukija nyumbani” Gibson alimwambia Prisca.
Kwa wakati huo walikuwa wakipiga stori ambazo kwa mtu mwingine zingeonekana kuwa za kijinga lakini kwao zilikuwa ni stori nzuri ambazo zilimvutia kila mmoja. Waliendelea kuongea usiku kucha mpaka katika kipindi ambacho wote wakapitiwa na usingizi.


Je nini kitaendelea?
Je Katie ataweza kumpata Gibson?
Je Prisca ataweza kujifungua salama hapo baadae?
Kuna mengi yatatokea katika hadithi hii, yatakuhuzunisha sana, yatakufurahisha sana ila mwisho wa yote, hadithi hii itakuburudisha sana.
Itaendelea KESHO SAA 1 USIKU.
inamuendelezo na marudio kama MARACLARA.

No comments:

Post a Comment