Kila
mmoja alionekana kuchanganyikiwa, kutokumkuta mtu yeyote ndani ya chumba kile
kuliwachanganya zaidi. Gibson hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa akikiona,
hakuamini kama mke wake, Prisca pamoja na mtoto wake, Genuine hakuwa ndani ya
chumba kile. Kila mmoja alikuwa akijiuliza mahali ambapo walikuwepo watu hao
lakini hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na jibu.
Kitu walichokifanya ambacho
kilikuwa ni cha haraka sana ni kuwasiliana na polisi na kisha kuwaelezea kila
kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Ni ndani ya dakika kumi, mapolisi wa kituo cha
Masaki wakafika mahali hapo huku wakiongozana na polisi wa kituo cha Oysterbay.
Dokta akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea hospitalini hapo
kuhusiana na wazungu hao ambao walikuwa wamefika mahali hapo kama madaktari
ambao walifika mahali hapo kwa ajili ya kutoa chanjo kwa watoto wadogo walio
chini ya miaka mitano.
“Unasema walitoka wapi?” Gibson aliuliza.
“Nchini
Marekani” Dokta alijibu.
Tayari Gibson akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi
mahali hapo, kichwa chake kikawa kama kimekwishahisi kitu fulani ambacho
kilikuwa kimeendelea mahali hapo. Gibson akaondoka na kwenda kukaa pembeni
kabisa ya polisi wale huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo.
“Vipi?” Dokta
alimuuliza mara baada ya kumuona akiwa ameelekea kule pembeni.
“Mke wangu na
mtoto wangu”
“Usijali. Tumekwishatoa taarifa polisi, wanalifanyia kazi” Dokta
alimwambia Gibson.
Polisi hawakutaka kulala, mtu ambaye alikuwa akilalamika
kwamba mke wake na mtoto wake walikuwa wametekwa na watu kutoka nchini Marekani
na ambao walijifanya kama madaktari walikuwa wakimfahamu sana. Gibson alikuwa ni
tajiri mkubwa nchini Tanzania ambaye alikuwa akisaidia watu mbalimbali nchini
hasa wale ambao walikuwa na matatizo mbalimbali.
Ni ndani ya dakika arobaini,
waandishi wa habari wakafika mahali hapo na kuanza kupewa maelezo juu ya kile
ambacho kilikuwa kimetokea. Muda wote Gibson hakuwa muongeaji, alikuwa kimya
huku akionekana kuwa mwingi wa mawazo.
“Ni Katie. Huyu atakuwa Katie tu”
Gibson alijisemea.
Mawasiliano yakaanza kufanyika, tayari polisi
walikwishajua kwamba watekaji hao bado wangekuwa ndani ya jiji la Dar es Salaam
tu. Simu zikaanza kupigwa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ulinzi huku
aina ya gari lile ambalo walikuwa wameondoka nalo likiwa linatolewa taarifa kwa
kila aliyeambiwa japokuwa namba zake hawakuwa wakizifahamu.
Walichokiona kwa
wakati huo, walijua fika kwamba watu hao walikuwa na uwezekano wa kuondoka
kuelekea Bagamoyo, Barabara ya Morogoro au ile ya kwenda Mtwara. Kitu walichoona
kuwa cha maana ni kuwasiliana na polisi wote ambao walikuwa katika sehemu hizo
na kuwaambia kwamba ulinzi na upekuzi wa magari ulikuwa ukihitajika kufanyika
tena kwa haraka sana.
Vyombo vya habari hasa televisheni na redio vikaanza
kutangaza kile ambacho kilikuwa kimetokea, kila mtu akaonekana kushangaa,
taarifa ile ilionekana kuwashtua kupita kawaida. Kila mtu akalaani kitendo kile
ambacho kilikuwa kimetokea, utekaji ulionekana kuwa kitu kigeni sana kutokea
nchini Tanzania.
“Watekaji ni lazima wakamatwe na mateka ni lazima wapatikane
wakiwa hai” Kamanda mkuu wa jeshi la polisi, Oswald aliwaambia waandishi wa
habari huku mapolisi wakiwa wamekwishaanza kazi yao.
****
Taarifa ile
ilikuwa ikiendelea kusambazwa kama kawaida na ilivuma kwa kasi hata zaidi ya
upepo. Kila mtu ambaye alikuwa akisikia alionekana kutokuelewa ni kitu gani
ambacho kilikuwa kimetokea mpaka Prisca na mtoto wake kutekwa manyara.
Polisi
wakaanza kuzunguka ndani ya jiji la Dar es Salaam huku lengo lao likiwa ni
kulitafuta gari lile ambalo lilikuwa linaendeshwa na watekaji wale. Kila kona,
polisi walikuwa wakizunguka zunguka, watu ambao walikuwa wakisafiri kwa kutumia
ndege, safari zilikuwa zimesimamishwa kwa muda, msako ulikuwa ukiendelea kila
kona.
Kwa wakati huo, Gibson pamoja na dokta mkuu wa hospitali ya Masaki,
dokta Philip walikuwa wamekwishafikishwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya
maelezo zaidi. Kila mmoja alikuwa akitoa maelezo yake juu ya kila kitu ambacho
kilikuwa kimetokea.
“Ina maana hamna uhakika kwamba watu hao walikuwa
madaktari?” Manase ambaye alikuwa polisi aliyehusika zaidi kwenye kuhoji watu
alimuuliza dokta Philip.
“Sikuwa na uhakika lakini kila nilipoona vibari
vyote walivyokuwa navyo, niliridhika nao na wala sikutaka kuhoji maswali zaidi”
Dokta Philip alijibu.
“Kwa hiyo walikuwa na vibali
vyote?”
“Ndio”
Manase hakutaka kuendelea kubaki ndani ya chumba kile,
akawaacha na kisha kuelekea nje ambako huko akaanza kuongea na polisi wengine,
simu zikaanza kupigwa sehemu mbalimbali na kisha kurudi tena ndani ya chumba
kile.
Hadi kufikia wakati huo, hali ilionekana kuwachanganya kupita kawaida.
Ni kweli walikuwa na uhakika kwamba watu wale hawakuwa madaktari lakini
walivipata wapi vibali ambavyo viliwaonyesha kwamba wao walikuwa
madaktari?
Kila swali ambalo walikuwa wakijiuliza lilionekana kuwachanganya
kupita kawaida, kwao, watu hao wakaonekana kujiandaa kupita kawaida katika
kufanya kila kitu ambacho walikuwa wamepanga kukifanya kwa wakati
huo.
“Unahisi kitu chochote kile?” Manase alimuuliza
Gibson.
“Ndio”
“Kitu gani?”
“Kuna mtu amehusika katika tukio
hili”
“Mtu gani?”
“Kuna mwanamke mmoja amehusika”
“Mwanamke
yupi?”
“Katie”
“Ndiye nani huyo?”
“Mcheza filamu za ngono aishiye
nchini Marekani”
Manase na dokta Phillip wakaonekana kushtuka, jibu ambalo
alilitoa Gibson likaonekana kuwashangaza sana. Hawakujua ni kwa nini Gibson
aliwaamba maneno yale, hawakujua kama Gibson alikuwa na uhakika juu ya kile
ambacho alikuwa amekisema au la.
“Unatuchanganya. Ndiye nani huyo?” Manase
aliendelea kuuliza.
“Mcheza filamu za ngono” Gibson alijibu.
Hapo ndipo
Gibson alipoanza kuelezea kila kitu kilichotokea katika maisha yake huku
akizungumzia kwa undani kila kitu ambacho alikuwa amekifanya pamoja na Katie.
Kila mmoja alikuwa makini akimsikiliza, mpaka anamaliza, kila mmoja alikuwa na
uhakika kwamba Katie alikuwa amehusika katika mchezo mzima.
“Amehusika katika
hili” Manase alimwambia Gibson.
Manase akatoka ndaniya chumba kile na kisha
kuanza kuongea na wenzake kuhusiana na kila kitu ambacho alikuwa ameambiwa na
Gibson. Taarifa zikaanza kutolewa sehemu mbalimbali ila kitu kikubwa ambacho
kilikuwa kikihitajika kwa wakati huo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba watekaji wale
wanakamatwa na hatimae kumtaja mhusika aliyewatuma kufanya utekaji ule.
“Kuna
tetesi zozote?”
“Ndio. Watu wa Chalinze walisema kwamba waliliona gari hilo
likipita kwa kasi”
“Kuelekea wapi?”
“Kama si Kilimanjaro, basi itakuwa
Tanga”
“Sawa sawa. Wapigieni simu polisi wa Segera na kuwaambia kwamba
inawapasa kuangalia kwa makini magari yote yatakayopita huku sisi tukianza
safari kwenda huko” Manase aliwaambia na kisha kutoka nje ya ofisi ile pamoja na
Gibson na dokta Manase na kisha kuanza kuelekea Segera ambako walijua fika
kwamba watekaji wale wasingeweza kuvuka salama bila kukamatwa.
“Chochote
kitakachotokea kwa familia yangu. Nitawaua wote waliohusika” Gibson alisema huku
akionekana kuwa na hasira.
****
Mara baada ya kutoka katika hospitali ya
Masaki moja kwa moja safari ya kuelekea Tanga ikaanza huku wakiwa
wamekwishajikamilisha kwa kila kitu. Andrew ambaye alikuwa katika usukani
akiliendesha gari lile wala hakutaka wachukue muda mwingi kuchelewa njiani, kila
alipoona kwamba hakukuwa na magari mengi barabarani, alikuwa akiendesha kwa
mwendo wa kasi.
Prisca bado alikuwa amelala usingizi mzito huku mtoto wake,
Genuine akiwa analia kupita kawaida kiasi ambacho akaanza kuonekana kuwa kero
kwa watekaji wote ambao walikuwa ndani ya gari lile. Kadri Genuine alivyokuwa
akizidi kulia na ndivyo ambavyo kelele zile zilionekana kuwa kero
zaidi.
Hawakujua ni kitu gani ambacho walikuwa wakitakiwa kukifanya kwa
wakati huo, vichwani mwao kulikuwa kukifikiriwa vitu viwili tu, ilikuwa ni
lazima wamtupe mtoto huyo barabarani au kama walikuwa wakitaka kwenda nae basi
ilikuwa ni lazima kufanya kitu ambacho kingemfanya mtoto yule kutokulia kwa
sauti kubwa kama ilivyokuwa.
“What should we do? (Tunatakiwa tufanye nini
sasa?)” Filbert aliuliza.
“Open the window (Fungua dirisha)” Reuben
alimwambia Filbert.
“What for? (Ili iweje?)” Filbert aliuliza huku akionekana
kushtuka.
“I want to do something (Nataka kufanya kitu)” Reuben alimwambia
Filbert.
“This is crazy Reuben, dont dare to do what you want to do (Huu ni
upuuzi Reuben, usithubutu kufanya hicho unachotaka kukifanya)” Filbert
alimwambia Reuben.
“I have to do this Fil. If I ain’t do this, then, we are
going to die (Inanibidi nifanye hiki Fil. Kama sitofanya hivi, tunakwenda kufa)”
Reuben alimwambia Filbert.
Mtafaruku bado ulikuwa ukiendelea ndani ya gari
huku Andrew akiwa bize kuendesha gari kwa kasi. Kitu ambacho alikuwa akikitaka
Reuben kilikuwa ni kumtupa mtoto Genuine dirishani huku gari likiwa kwenye
mwendo ule wa kasi lakini Filbert hakutaka kuona kitu hicho kikitokea.
Walikuwa wamekwishafika Kimara, sehemu ambayo magari mengi yalikuwa
barabarani huku hata idadi kubwa ya watu ikiwa pembezoni mwa barabara. Kitu
alichokuwa akikitaka Filbert ni kumtupa Genuine katika eneo ambalo halikuwa na
wakazi wengi kwani kama wangefanya vile mahali pale basi ilikuwa ni lazima
kugundulika tu.
Safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida, hakukuwa na mtu
yeyote ambaye alikuwa akilitilia mashaka gari lile ambali bado lilikuwa
likiendelea na safari ya kuelekea Tanga. Kutokana na mwendo wao kuwa mkali,
walichukua dakika arobaini wakawa wamekwishafika Chalinze.
“Twende kulia”
Reuben alimwambia Andrew ambaye akakata kulia. Ramani ambayo walikuwa nayo
mikononi mwao ndio ambayo ilikuwa ikiwaongoza katika kila njia ambayo walikuwa
wakienda kwa wakati huo. Lengo lao kubwa kwa wakati huo lilikuwa ni kufika Tanga
ambapo huko wangeonganisha mpaka Mombasa na kuelekea Nairobi na kisha kuchukua
ndege na kurudi nchini Marekani hasa mara baada ya kukamilisha kumuua
Prisca.
Walitembea na gari lao kwa muda wa dakika thelathini, wakaanza kufika
katika maeneo mengi ambayo hayakuwa na makazi, maeneo ambayo yalikuwa na miti
mingi sehemu zilizoonekana kuwa kama pori. Hapo ndipo makubaliano yale
yakafikiwa muafaka, walitakiwa kumtupa Genuine kupitia dirishani huku gari
likiwa katika mwendo ule ule wa kasi.
Huku wakiwa wamekwishakubaliana kitu
cha kufanya, ghafla Prisca akaamka kutoka katika usingizi na kuanza kushangaa
mahali ambapo alipokuwa. Fahamu zilivyomjia vizuri, akaonekana kukumbuka kila
kitu.
Kitu cha kwanza akaanza kumtafuta mtoto wake, tayari alikuwa katika
mikono ya Reuben ambaye alikuwa akijiandaa kumtupa nje Genuine kupitia katika
dirisha lile huku Filbert akiwa amekwishafungua dirisha.
Hata kabla Prisca
hakuongea kitu chochote kile, Reuben alikifanya kitu kimoja tu, akamtupa Genuine
nje kupitia dirisha huku gari likiwa katika mwendo mkali wa kilometa 120 kwa
saa. Kilichosikika ni sauti ya Genuine tu ambaye akajigonga katika miti kadhaa,
damu zikatapakaa katika kila mti aliojiginga na kuwa mwisho wake.
Lilikuwa ni
tukio kubwa na baya katika macho ya Prisca, hakuamini kile ambacho alikuwa
amekiona kwa wakati ule. Akapiga uy owe mmoja tu, akajikuta akipoteza fahamu,
tukio ambalo alikuwa amelishuhudia kutupwa kwa mtoto wake lilionekana kumshtua,
kumuumiza kupita kawaida.
Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuonekana kujali,
kitu ambacho walikuwa wakikitaka mahali hapo ni kufika Tanga ambapo
wangeonganisha mpaka Mombasa, ila kabla ya kufika Mombasa, ilibidi wamuue Prisca
na kisha kuendelea na safari ya kuingia Mombasa.
“Kuna tatizo mbele yetu”
Andrew aliwaambia huku wakiwa wamekaribia kufika Segera, njia panda ya kuendea
Kilimanjaro na Tanga.
“Kuna nini?”
“Kuna magari mengi yanaonekana
kusimamishwa, nafikiri kuna kitu kinaendelea” Filbert alijibu.
“Tumia mpango
B” Reuben alimwambia Andrew huku akiangalia ramani aliyokuwa
ameishika.
“Usijali. Nimekusikia kiongozi” Andrew
aliitikia.
****
Mpango B ukafanyika mahali hapo, Andrew akakata kona kulia
na kuingia kichakani. Mwendo ulikuwa ni wa kasi sana, katika kipindi hicho
tayari walikuwa wamekwishashikwa na wasiwasi kwamba polisi walikuwa
wamekwishagundua na hivyo walikuwa katika kila njia kuhakikisha
wanakamatwa.
Bado Andrew alikuwa akiendesha gari kwa kasi, katika kipindi
hicho walidhamiria kuingia mkoani Tanga ambako wangeanza kuelekea Zigaya ambako
wala hakukuwa mbali sana kuingia Mombasa nchini Kenya.
Kila mtu aklini mwake
alikuwa akifikiria lake kwa wakati huo, ni kweli kwamba walikuwa wakitamani sana
kufika nchini Kenya ambako huko wangechukua ndege na kuelekea nchini Marekani
lakini uwepo wa Prisca ndani ya gari uliwafanya kuchanganyikiwa.
Lengo kubwa
hasa ambalo lilikuwa limewaleta nchini Tanzania lilikuwa ni kumuua Prisca lakini
cha kushangaza, mpaka muda huo hawakuwa wamekamilisha kile kilichokuwa
kimewaleta nchini Tanzania japokuwa Prisca walikuwa nae.
Safari ilikuwa
ikiendelea zaidi huku ramani ambayo walikuwa nayo ndio ambayo ilikuwa
ikiwasaidia katika kuwaongoza kule ambako walikuwa wakiendelea kwenda mbele.
Kwanza kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo kilikuwa ni kuingia Tanga
mjini ambako wangeongeza mafuta kwenye gari lao na kisha kuendelea na safari yao
kama kawaida.
Masaa mawili yakakatika huku wakiwa bado wakitembea porini na
ndipo wakaamua kuingia barabarani. Hapo, Andrew akaongeza mwendo zaidi,
walijiona kuwa nyuma ya muda, walikuwa wakitaka kufika haraka iwezekanavyo ili
kazi yao izidi kuwa nyepesi zaidi.
Wakaingia Tanga mjini saa sita kasoro
mchana na moja kwa moja kuanza kuelekea katika kituo cha mafuta kwa ajili ya
kuongeza mafuta kabla ya kuendelea na safari yao zaidi. Hakukuwa na mtu ambaye
alikuwa na wasiwasi wowote ule, wakazi wengi wa Tanga hawakuonekana kulitilia
umakini tangazo ambalo lilikuwa limetolewa katika vyombo mbalimbali vya habari
juu ya utekaji ambao ulifanyika jijini Dar es Salaam.
“Lets make hurry
(Tufanyeni haraka)” Filbert aliwaambia.
“Dont worry. We are safe in here
(Usihofu. Hapa tupo salama)” Reuben alimwambia Filbert huku akionekana kutokuwa
na wasiwasi wowote ule.
“There is no more peace. I have seen the news on the
television about us (Hakuna amani hapa. Nimeona habari kwenye runinga kuhusu
sisi)” Filbert aliwaambia.
“Thats not true. When did you learn to undrestand
Swahili language? (Hiyo si kweli. Umejifunza lini lugha ya Kiswahili?)” Reuben
aliuliza huku uso wake ukiwa na tabasamu.
“I saw Gibson on the television,
then tell me what do you think is goin on (Nimemuona Gibson runingani, aya
niambie unafikiri nini kinaendelea?)” Filbert alikuwa akijitahidi kuelezea kila
kitu ambacho alikuwa amekiona kwenye televisheni lakini hakukuwa na mtu yeyote
ambaye alionekana kumuamini, wote walimuona Filbert kuwa mtu muoga sana.
Kitu
ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kula chakula hata kabla safari yao
haijaendelea zaidi na zaidi. Wakaenda hotelini na kuingia ndani, wakala chakula
na kisha kuendelea na safari yao.
Muda wote huo, Prisca alikuwa amepoteza
fahamu, mshtuko mkubwa ambao alikuwa amekutana nao ulikuwa ulimfanya kuwa katika
usingizi mzito mpaka katika kipindi hicho. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana
kujali, kupoteza fahamu kwa Prisca kulionekana kuwa nafuu kwao kwa kuamini
kwamba hakukuwa na usumbufu wowote kwa wakati huo ndani ya gari.
Wakaanza
kushika barabara ya kuelekea Mombasa, daladala nyingi zilikuwepo njiani, idadi
ya watu ilikuwa kubwa barabarani huku kila sehemu kukionekana kuwa na uchangamfu
mkubwa. Kitu ambacho walikuwa wamekifanya kwa wakati huo, waliandaa fedha za
kutosha kwa kuamini kwamba kama wangefika mpakani, wasingeruhusiwa kuvuka ila
kwa kutumia dola ambazo walikuwa nazo, wala kusingekuwa na tatizo lolote
lile.
Safari iliendelea mbele zaidi na zaidi, tayari walikuwa wamekamilisha
asilimia themanini ya kazi ambayo walikuwa nayo na zilibakia asilimia ishirini
tu, za kuingia Mombasa, kusafiri mpaka Nairobi na kisha kuchukua ndege na kurudi
nchini Marekani huku wakiwa na ushindi mkubwa mioyoni mwao kitu ambacho
kingekuwa furaha kubwa kwa Katie ambaye alikuwa amewatuma nchini
Tanzania.
“Tufanyeni kitu kimoja” Filbert aliwaambia.
“Kitu gani?” Reuben
aliuliza.
“Tumuueni huyu mwanamke kabla hatujaingia nchini Kenya. Yaani
namaanisha kabla hatujafika mpakani”
“Wazo lako zuri. Nafikiri umeona kwamba
anaweza kutuletea matatizo hapo mpakani”
“Hilo ndilo nililolifikiria” Filbert
aliwaambia.
Wazo ambalo lilitolewa na Filbert likaonekana kufaa sana,
walichokifanya kwa wakati huo ni kukata kona na kisha kuanza kuingia porini,
sehemu ambayo wangeweza kumuua Prisca huko na kisha kuendelea na safari yao ya
kuelekea mpakani.
Ghafla, Prisca akarudiwa na fahamu, akabaki akimwangalia
kila mtu ndani ya gari lile. Kwa mara ya kwanza hakuonekana kukumbuka kitu
chochote kile ila baada ya sekunde kadhaa, akakumbuka mambo mengi, likiwepo lile
la kutupwa kwa mtoto wake, Genuine.
Prisca akaanza kulia, akamvamia Reuben
kwa lengo la kupambana nae kwa kile kitendo cha kumtupa mtoto wake nje ya gari
na wakati gari hilo lilikuwa kwenye mwendo wa kasi. Reuben akafanikiwa
kumdhibiti Prisca ambaye akalazwa kitini huku akiwa amekandamizwa na kiganya cha
Reuben.
Walipofika porini zaidi, gari likasimamishwa na kisha Reuben kumtoa
Prisca nje ya gari huku akiwa amemshika shingoni. Prisca alikuwa akilia kama
mtoto, akili yake kwa wakati huo ilikuwa kama imechanganyikiwa, hakumpenda
Reuben hata kidogo, alikuwa akimchukia kupita
kawaida.
“Niachieeeeee....niachieeee” Prisca alikuwa akipiga kelele lakini Reuben hakuweza
kumuachia.
Kila kitu kwa wakati huo kikaonekana kuwa na amani, mazingira
yalionekana kumridhisha kila mtu. Kitendo kilichokuwa kikitakiwa kufanyika
mahali hapo kilikuwa ni kumuua Prisca na kisha kuondoka kuelekea
mpakani.
Alichokifanya Reuben kwa wakati huo ni kuanza kumkaba roba kali
Prisca. Prisca akabaki akitoa milio ya tofauti tofauti huku akijitahidi kutaka
kuitoa mikono ya Reuben shingoni mwake lakini wala hakuweza kufanikiwa hata
kidogo. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Reuben alivyomkaba
zaidi na zaidi.
Ghafla, Prisca akaanza kuona kizunguzungu huku giza la mbali
likianza kuonekana mbele yake. Tayari kwa wakati huo alikuwa amebakisha muda
mchache sana wa kuwa hai, muda ambao wala haukuzidi hata dakika mbili. Giza lile
alilolkuwa akiliona kwa mbali likaanza kumsogelea zaidi na zaidi, baada ya hapo,
akayafumba macho yake huku akihisi mtoa roho akiwa amekwishamfikia kwa ajili ya
kuichukua roho yake.
Je nini kitaendelea mahali hapo?
Je Prisca
amekufa?
Je watekaji watakamatwa?
No comments:
Post a Comment